2017-09-30 13:39:00

Ziara ya Papa Bologna:Anakuja kati yetu kuimarisha Injili hai


Katika Ziara ya Kitume ya  Baba Mtakatifu Francisko inayotarajiwa kufanyika tarehe 1 Oktoba katika Mkoa wa Emilia Romagna kwa namna ya pekee , ratiba yake inaonesha kuwa mapema asubuhi mara ya kufika atakutana na wazelendo wa Cesena ambapo katika Kanisa Kuu la Cesena, atazungumza, Mapadre, watawa, walei wa baraza la kichungaji na wahusika wote wa parokia. Kabla ya kuacha jimbo la Cesena, atafanya  mkutano mfupi na wageni wa nyumba ya mapokezi ya jimbo na wote waliofanya maadalizi ya ziara yake fupi katika jimbo hilo la Cesena. 

Ratiba ya  kutembelea Jimbo Kuu  Bologna, inajikita katika matukio ya aina sita, hiyo ni pamoja na makutano wa wahamiaji, kuzungukia barabara za kihistoria za mji  wa Bologna, Mahubiri na sala ya Malaika wa Bwana katika uwanja mkubwa, kukutana na watu maalumu na wafanyakazi.  Aidha, Baba Mtakatifu Francisko atapata chakula cha mchana na maelfu ya maskini katika Madhabahu ya Mtakatifu Petronio na kukutana na  Mapadre na watawa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Ulimwengu wa kitaaluma kwa vijana wa vyuo vikuu,  watakutana naye katika uwanja wa Mtakatifu Domeniko, kabla ya Maadhimisho ya Misa Takatifu itakayofanyika katika Uwanja wa Mpira wa Ara mjini Bologna Italia. Mara baada ya Misa Takatifu, Biblia 100,000  zitatolewa kwa watu, kama ishara ya tukio la Jumapili ya kwanza ya Neno, kwa matashi ya Baba Mtakatifu mwenyewe kwa ishara ya  matunda ya Jubileo ya Huruma.

Naye Askofu Mkuu Matteo Zuppi wa Jimbo Kuu la Bologna akihojiwa juu ya maandalizi ya mwisho ya ziara ya Baba Mtakatifu anasema, ziara hii katika hitimisho la Kongamano la Ekaristi ni tukio la aina yake kama vile yak ila kongamano za ekaristi zinazofanyika. Mwaka huu Kongamano limeongozwa na kauli mbiu “Ekaristi na Mji wa watu”, imewasaidia kugundua uwepo wa Bwana katika Ekaristi na hata kwa njia ya Ekaristi  kutazama kwa macho mapya hali halisi kwa macho ya Yesu mji wa watu kwa maana ya kuwa na mtazamo tofauti.
Askofu Mkuu Zuppi anaongeza, kwa kutazama namna mpya, umeleta  mwamko wa kutambua hali halisi ya watu. Na ndiyo wito pia wa Baba Mtakatifu anao sisitiza kwa watu wote ili waweze kutoka nje kwenda mbali na kukutana na watu wengine , kwa mfano katika eneo la HUB mahali ambapo kuna kituo cha wahamiaji na wakimbizi ambao wamefika katika nchiya Italia.

Askofu Mkuu Zuppi anaongeza kusema, wanamsubiri Baba Mtakatifu kwa hamu na furaha kubwa ya kukutana naye. Yeye atawasaidia kutambua kwa kina hali halisi ya mji, changanoto kubwa zilizomo ndani mji, lakini pia hata matarajio yake. Kwa njia hiyo kufika kwa Baba Mtakatifu katika jimbo lao ni kuhakikisha hili na kuwasaidia waweze kuishi  wakichangua hawali ya yote Injili ambayo inawasaidia kutazama hali halisi ya mji kwa macho ya Yesu.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.