2017-09-30 15:35:00

Papa:jifunze utamaduni wa makutano na siyo kugeuka mnara wa Babeli


Tarehe 30 Septemba 2017 Baba Mtakatifu amekutana na kuzungumza na wawakilishi wa Shirikisho la manispaa za Kitaifa nchini Italia mjini Vatican. Wakati wa hotuba yake, Baba Mtakatifu anasema katika kurasa za Biblia kuna historia ya Mnara wa Babeli (Mw 11,1-9). Mji ulio kuwa umekamilika lakini baadaye ukabaiki  katika kumbukumbu ya binadamu na ishara ya vuruguru ,kupotea kwa kujidai na mgawanyiko. Walikosa ukosefu wa kulewana , ambapo ikatokea kutoweza kufanya jambo lolote kwa pamoja katika ujenzi wa mnara.

Baba Mtakatifu Francisko anaelezea kwamba katika Biblia lakin inafunga na kurasa za Ufunuo ambao ni tofauti na zile za historia ya  mnara wa Babeli kwa maana, katika Ufunuo ni kutazama mji mpya ambao ni dunia mpya. Sura ya ujenzi wa hema kubwa na ndania yake kuna makutano na uwezekano wa kukutana na wazalendo wote . Pamoja na kuishi humo, bado kuna zawadi kwa maana anaye ingia humo kumeundwa mahusiano ya kindugu na umoja.
Baba Mtakatifu anaendelea, Maandishi Matakatifu yana maana kubwa , kwa sababu yanatoa hali halisi ya hatima ya ulimwengu katika sura hiyo mpya. Picha ya mji na mambo yake yaliyomo, inajileleza kama jamii ya kibinadamu inayoweza kusimama tu katika msingi wa mshikamano wa kweli. Na kwa njia hiyo hakuna nafasi ya  wivu, kupendelea hali za kidunia, roho za utofauti kwa sababu  mji wa  mshikamano hutoa hukumu dhidi ya  vurugu na ghasia hizo.
Akifafanua juu ya maana ya miji kamili, Baba Mtakatifu anasema  kuwa mji anaotaka kuwashauri na ambao wao wamekabidhiwa kuwajibika, ni mji ambao hauruhusu kuwa na mtazama wa aina moja tu kama ubaguzi, unaotamzama mambo yake binafsi au wa umma peke yake.

Ni mji ambao hauwezi kukubabaliana kwamwe na vizingiti kipofu vya ifisadi , mahali ambapo utuengeneza viota vya majeraha ya ubaguzi. Aidha anasema miji mipya ni ile isiyo tambua kuta za ubinafsi na nafasi za umma, yaani ni mji ambao unatambua kauli mbiu moja ya sisi badala ya kuweka viini macho  kuwaachia wale walio wachache. Ujenzi wa mji huu unahitaji ninyi, anasema Baba Mtakatifu , na siyo hali ya  ya kujidai na kuwa wa hali ya juu, bali  ni kujikita kikamilifu katika juhudi za unyenyekevu wa kila siku kuelekea kwa wale wanyonge wa chini. Ni ni katika kupanua viwanjia hili kutoa nafasi ya kila mmoja kuwa na uwezo wa kujikamilisha binafsi na familia yake, vilevile kujifungua katika umoja na wengine.
Ina upendo ,kubwa , ambao unajikita katika wema wa pamoja. Na huo ndiyo mtamzamo ambao unafaa kuukuza kwa watu hadhi ya kuwa wazalendo. Na kuhamasisha haki za kijamii,  huduma na fursa mbalimbali. Hiyo inaweza kutakana na kuanzisha kwa mipango mbalimbali ya kufanya watu waishi katika eneo na kulitunza, aidha kuelimisha uwajibikaji.

Mji ni kiungo kinachoishi, ni mji ambao unategemewa kuvuta pumzi , na iwapo kuvuta pumzi ni kwa shida maana yake mtu anapata hewa isiyo ya kutosha. Baba Mtakatifu mawazo yake yanamwendea kwa  wale wasio  pata huduma za kutosha, mahali ambapo umasikini na kubaguliwa unatishia jamii . Anabainisha kuwa, ni mahali ambapo mji unapaswa kuongeza juhudi lakini isiwe njia mbili , kama vile njia ya kwanza ya barabara ya kukimbia kwa haraka na njia ya pili ile ya wale ambao ni masikini wasio kuwa na ajira, familia nyingi za wahamiaji na wakimbizi wasio kuwa na mahali pa kukimbilia 
Baba Mtakatifu Francisko anaonya , hakuna kukubali mantiki hizi zinazogawanya , na kuwafanya maisha ya watu yawe  ya kifo kwa wengine na mapambano yasiyo isha, kwenye uharibifu bila kuwa na maaana ya mshikamano na ubinadam kindugu. Anawahimiza  kwenda katika vijiji na jamii za pembeni ili kuimarisha maeneno ambayo  ni shule bora ya kutambua mahitaji ya kweli na kutafuta ufumbuzo. Ni lazima kutambua hali na hata kutafuta njia zake ili kuweza kujenga jumuia mahali ambapo kila mmoja anajisikia kama mzalendo mwenye haki  kwa ajili ya wema wa kila mmoja.

Ili kuweza kukuza mtazamo huo kuna ulazima wa sera  za kisiasa na kiuchumikujikita kwa undani katika maadili. Maadili ya uwajibikaji, ya mahusiano, katika jumuiya na katika mazingira. Kwa maana hiyo kuna ulazima wa umoja wa kweli na thabiti wa kuweza kuunda uzalendo wa kudumu,t unahitaji siasa ya mapokezi , ya kushirikisha , ambayo  haiweki watu pemebeni hasa wale wanaofika katika maeneo , bali kuwaweka mstari wa mbele kwa ajili ya kuimarisha matunda ya asili ambayo kila mmoja anaweza kuchangia na kumiliki.

Baba Mtakatifu aidha anaonesha wasiwasi mkubwa na kutambua hali mbaya inayowakabili wazalendo wa Italia, hasa katika wimbi la wakimbzi na wahamiaji. Hiyo inasababisha hofu nyingi kwa wazalendo kwa ajili ya wageni hao ambao wamelazimika kuondoka katika nchi zao kutokana na kipeo cha uchumi na matatizo mengine ya kivita na majanga ya asili. Lakini hofu hizo anasema, zinaweza kutoweka iwapo  watatoa fursa  ya  makutano ya  watu wageni katika, kutambuana na kubadilishana mawazo. Kwa njia hiyo anashukuru kwa dhati kuanzishwa kwa vyama vingi vinavyo hamasisha juu ya makutano ya kiutamaduni ili kuweza kubadilisha utajiri wa kisanii na tamaduni katika kuleta utambuzi na mazungumzo kati ya jumuiya mahalia na wale wageni. Anawatakiwa kila jema katika harakait hizo ambapo wanaweza kujenga Yerusame mpya , mahali ambapo kutakuwa na wema na upendo mwingi kwa watu wote na wakati wote.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.