2017-09-30 16:25:00

Kard. Sandri:Tuwe na utambuzi wa Malaika wakuu wasaidizi wa Mungu


Ni furaha kubwa kuadhimisha Misa Takatifu katika kuadhimisha Sikukuu ya watakatifu malaika wakuu Michaeli, Rafaeli na Gabrieli.Ni maneno aliyoanza nayo katika  mahubiri ya  Kardinali Leonardi Sandri Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki  Katika Kanisa Kuu la Bucarest nchini Romania  Ijumaa 29 Septemba 2017.

Kardinali Sandri yuko ziara nchini Romania tangu tarehe 27 jioni hadi  siku ya Jumapili tarehe 1 Oktoba 2017. Ziara yake imendaliwa na Mwakilishi wa Vatican nchini humo  na mwaliko kutoka kwa Kardinali Lician Mureşan, askofu Mkuu wa di Făgăraş na Alba Iulia ya Romania katika tukio kuadhimisha miaka mia moja ya Baraza la Makanisa la Mashariki. Kardinali  Sandri anasema, mawazo pia yanaongozana na kuzisindikwazwa na Baba Mtatifu ambaye amemwomba kuwafikishia baraka zake. Ni muhimiu kukumbuka kuwa kati ya ishara za kwanza za kipapa  alizo anza nazo mara baada ya kuchaguliwa,  tarehe 5 Julai 2013 , Baba Mtakatifu alibariki sanamu ya Malaika Michaeli, katika kurabaruku Serikali ya Vatican na kuiweka chini ya Ulinzi na usimamizi wa Mkuu wa majeshi ya  Mbinguni Michaeli na Mtakatifu Yosefu mchumba wa Bikira Maria.

Katika kutafakari sura Malaika  ya Yosefu Kardinali Sandri anasema Yosefu anakubali kuwa mlinzi wa maisha ya mtoto wa Mungu, alimweka mtoto mahali pa usalama  wakati Erode anamtafuta kumuua. Malaika Michaeli ni yule anayepambana na shetani kwa ajili ya nguvu za majeshi ya  Mungiu, analinda wanajeshi wa mbingu dhidi ya ushambulizi wa shetani , inavyoelezwa katika kitabu cha Ufunuo. Joka linataka kumla mtoto anayezaliwa . Hilo  ni fumbo la ubaya dhidi ya mtoto wa Mungu. Kwa bahati lakini Neno la mwisho  Bwana bi mshindi wa maisha na ufufuko.Ni kujikabidhi kwa Bwana na kwa Maombezi ya  Mtakatifu Yosefu na Malaika Mkuu Michaeli.

 Furaha ya malaika ni ya dhahiri, lakini pamoja na unyekevu. Malaika Gabrieli alifurahi kuweza kuonesha utashi wa Mungu kwa binadamu  na hiyo inatufundisha kuona uhuru na unyenyekevu wa mtoto mchanga huko Nazareth, kwa njia ya  Mama Maria akawa mama wa Mungu . Anaongeza, hiyo ndiyo hali halisi ambayo inatakiwa kwa kila yoyte anayeejiweka tayari kuinjilisha. 
Kardinali Sandri anasisitiza kuwa kila  siku, mlio wa kengele unawaalika waamini kushiriki katika sala ya Malaika wa Bwana wakiungana pamoja na Baba Mtakatifu Francisko.

Katika utambuzi huo, jamii iweze kupeleka habari njema ya Kristo ambayo kwa wakati mwingine siyo jambo rahisi na wakati mwingine ni maneno tu bila matendo. Ni lazima kuwa na unyenyekevu na kushiriki hata sala kama ile ya Bwana aliyofanya wakati wa karamu ya mwsho ” ili wote wawe na umoja”.
Mabadiliko yanayokwenda  kasi katika bara la Ulaya yatafanya kila jumuiya ya Kanda  na nchi kutafakari kwa dhati ili kuweza kushuhudia kwa umoja ambao Yesu Kristo anazidi kutuonesha kwa njia ya Ekaristi takatifu na wokovu katika ujenzi wa mwili wake ambao ni Kanisa.Lakini katika safari,  Kania siyo peke yake maana yupo Malaika Rafaeli kwa maana hata sisi ni vipofu kama Tobia , ambao tunahitaji Malaika huyo atuongoze katika njia kuelekea  mahali ambapo kuna mwanga unao angazia watoto wa Mungu.

Malaika Miacheli yupo karibu kupamaba na mabaya yote yanayosumbua, Malaika Gabrieli yupo karibu yetu kuleta habari njema ya furaha na kushuhudia Injili inayookoa. Na Mtakatifu Rafaeli kama mafuta ya huruma ya mungu katika mioyo ya waamini waliojaa majeraha ma  waliotengana  ili kuweza kutuongoza katika mwanga wake wa umoja na Bwana wetu Yesu Kristo.

 Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.