2017-09-29 17:24:00

Patriaki Sako:Elimu ni msingi dhidi ya mapambano ya itikadili kali


Kutoka milioni  1,5 ya wakristo waliokuwa wanaishi, leo hii  chini Iraq wamebaki wakristo  laki tano tu. Ni mauaji ya kimbari ya kweli . Ni maneno ya Patriaki Loius Raphael I Sako wakati wa kutoa hotuba yake kwenye Mkutano ulifunguliwa tarehe 28 Septemba 2017 mjini Roma, kuhusu mada ya  Ujenzi mpya wa vijiji vya wakristo vya Bonde la Ninawi nchini Iraq.

Katika hotuba yake anasema, hiyo yote imetokana na mangilio ya Serikali ya Kiislam katika Bonde la Ninawi mnamo mwaka 2014 na kusababisha watu 150, 000 ya wakristo kukimbilia maeneo ya Kurdistan Iraq.  Lakini kwa sasa , Bonde la Ninawi ni huru ambapo  watu karibia 14,000 wameanza  kurudi katika vijiji vyao,  shukrani kwa Shirika la Kipapa kwa Kanisa  hitaji na mashirika mengine ya Acs ambayo yamesaidia hatua hiyo.
Wakristo hawako peke yake na ujenzi wa mahali pa kuishi katika eneo hilo hautoshi kwa maana inahitaji ushuhuda wa imani yetu yote ,kwa maana  hiyo ndiyo utume wa kuwasaidia wakristo na waislam wafungue mioyo yao.Lakini anaongeza kwa bahati mbaya bado kuna hatari zinazoashiria kanda hizo.

Tishio la vita mpya inakaribia anasema, Patriaki Sako, kwa maanaipo vitutano ya hapa na pale bado  kati ya nchi na kanda, kati ya Serikali ya Kikurdi na ile ya Baghdad. Lakani watakao lipa katika vita hivyo bado ni wakristo na badhi ya madhehbu mengine madogo wakati huo huo kwa upande wa wakristo hawana uwezo wa kutangaza na kuomba  haki zao mbele ya serikali hizi. Patriaki Sako anasema tena kwa masikitiko makubwa kuwa, kuna wasiwasi mkubwa  kuhusu ulinzi , ndiyo maana wakristo wengi waliokimbia Iraq wanawakilisha  kupoteza jamii ambao haitakuwapo tena ya kuwa binadamu anaye penda amani na mariadhiano.

Halikadhalika , Patriaki Sako katika hotuba yake anahimzia  nchi ya Marekani kuchukua hatu kwa hali  katika uwajibikaki na kufanya tathini ya hali halisi,. Hiyo ni katika kutafuta njia za kupitia ili nchi ya Iraq iweze kumaliza migogoro hii  ya kivita mabayo imedumu kwa miaka mingi na kuweza kushinda itikadi kali za kigaidi ambazo zinaashiria pia kuingia katika bara la Ulaya.
Patriaki Sako I anasema, kusaidia katika kuelimisha jamii ni msingi mkubwa dhidi ya mawazo potofu ya itikadi kali ambazo zimesambaa katika makabila. Hizo itikadi zinahusu mara nyingi kutumia nguvu, kulipiza visasi na vurugu. Kwa njia hiyo elimu inaweza kukuza mazungumzo ya kisiasa , kiutamaduni na dini tofauti, aidha hata nchi kufanya kazi kwa juhudi ya kuzingatia Katiba imara  ambayo inathibitisha haki za uraia kwa wote na kuendelea kutoa misaada ya kibinadamu. 

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.