Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Katekesi siku ya Jumatano

Uzinduzi wa Kampeni ya Caritas kwa ajili ya kushirikishana safari

Baba Mtakatifu Francisko baada ya katekesi amezindua Kampeni ya Caritas kwa ajili ya kuhamasisha huduma ya Binadamu katika jamii

27/09/2017 16:07

Mara baada ya Katekesi yake, Baba Mtakatifu amewakaribisha kwa namna ya pekee wawakilishi wa Catritas Internatinalis katika uzinduzi rasmi wa Kampeni ya kushikirishana safari . Baba Mtakatifu anasema kauli mbiu ya kampeni yao ni jina zuri ambayo amependelea iwe sambamaba na katekesi hiyo. Amewakaribisha wahamiaji, wanaomba hifadhi na wakimbizi ambao pamoja na Caritas ya Italia na Taasisi mbalimbali katoliki kuwa ni ishara hai katika Kanisa. Wanatafuta kuwa wazi na kujufungua wazi kwa wale walio baguliwa na kuwakaribisha.

Anawashukuru kwa jitihada zao   za huduma bila kuchoka.  Katika jitihada za kila siku anaongeza Baba Mtakatifu, wao wanakutana na Kristo mwenyewe anaye wakumbusha kwa namna ya pekee,  kuwa karibu na  ndugu kaka na dada kwa kufungua mikono wazi. Maana mikono ikiwa wazi na hakika ni kama izile nguzo zilizozunguka uwanja wa Mtakatifu Petro zikiwakilisha Kanisa mama linalokumbatia wote na kushirikishana safari ya pamoja. 
Baba Mtakatifu aidha anawakaribisha wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali  za jamii ya umma wakijihusisha katika kuwatunza wahamiaji na wakimbizi, pamoja na Caritas ambao pia wamekusanya sahini nyingi za kampeni ya sheria mpya ya wahamiaji katika mantiki ya hali halisi ya sasa.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

27/09/2017 16:07