Leo hii ninapendelea kuongelea juu ya maadui wa matumaini, kwasababu matumaini
kama kila aina ya wema wa ulimwengu huu yana maadui wake.
Wakati wa maandalizi ya katekesi nimeijiwa wazo la historia ya kizamani ambayo chungu
kilifunguka ikatokeza balaha kubwa la kihistoria katika ulimwengu. Lakini watu wengi
wanakumbuka sehemu ya mwisho ya historia hiyo ambayo inayofungua mwanga, kwamba mara
baada ya ubaya wote kutoka mdomo wa kile chungu, zawadi ndogo ilijitokeza na kushinda
ubaya wote uliokuwa umesambaratika . Pandora ambaye mwanamke aliyekuwa analinda chungu
hicho aliigundua hiyo mwishoni yaani wagiriki waliita Elpis ikiwa na maana ya matumaini.
Ni maneno aliyo anza nayo Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Katekesi yake ya Jumatano tarehe 27 Septemba 2017 katika uwanja mkubwa wa Mtakatifu petro mjini Vatican. Akiendelea, historia hiyo ni muhimu kwasababu ya binadamu katika matumani. Watu wamezoea kusema palipo na maisha kuna matumaini , lakini ni kinyume na mawazo hayo, kwani anasema, ni matumaini yanayosimamisha miguu, yanalinda, yanatunza na kukuza. Iwapo binadamu hasingeweza kukuza matumaini, ina maana binadamu hasingeweza kuwa na fadhila hii, asingeweza kutoka katika shimo la andaki , aidha hasingeweza kuacha alama yoyote ya historia katika dunia hii.
Mshahiri mmoja wa kifaransa, Baba Mtakatiu naendelea Charles Péguy ameacha kurasa zake nzuri za matumaini. Kwa maana katika shahiri lake anasema Mungu hatoi mshangao tu wa imani ya kuwa mwanadamu, hata katika upendo lakini kile kitoacho mshangao wa hajabu ni matumaini: kwa wale watoto wasikini ambao wanaona mambo yanavyokwenda wanaamini kwamba kila kitu kitaenda vema kesho yake. Aidha anasema, mshahiri huyo anatoa mwaliko wa kutazama nyuso za watu wengi wanaopitia katika dunia hii, wazalendo, masikini wafanyakazi , wahamiaji watafutao maisha bora ya baadaye, ambao wanapambana kila siku pamoja na uchungu wa maisha magumu ya leo , wakiwa na majaribu ya kila aina, lakini ndani ya mioyo yao ni watoto ambao wanamatumani ya kupata maisha mapya yenye haki na utulivu.
Matumaini ni msukumu wa moyo kwa yule nayesafiri kuacha nyumba, ardhi , wakati mwingine familia na ndugu kwa ajili ya kutafuta maisha bora, yenye hadhi kwa ajili yake na ndugu zake. Vile matumaini yanatoa msukumo wkatika mioyo ya yule anayepowakea, akiwa na shahuku ya kukutana, kujuana na kuzungumza . Matuamani ni msukumo wa kushirikishana safari ya maisha kama inavyokumbusha leo hii Kampeni ya Caritas ambayo leo hii inazinduliwa rasmi. Baba Mtakatifu anasema ndugu wote wasiogopte kushirikishana safari!. Daima safari inafanyika kwa watu wawili : wale ambao wanakuja katika ardhi yetu, na sisi tunaokwenda katika nchi zao , ili kuweza kuwatambua tamaduni na lugha zao. Ni safari ya wawili , lakini bila matumaini safari hiyo haiwezekani kutendelea.Anasisitiza Matumaini ni msukumo wa kushirikishana katika safari.
Matumaini siyo wema wa watu waliojaza tumbo lao. Na ndiyo maana masikini daima
wamekuwa mstari wa mbele katika matumanini. Na kwa maana hiyo tunaweza kusema ni masikini
hata wale ombaomba na ndiyo wako mstari wa mbele katika historia. Ili Mungu aweza
kuja duniani , alihitaji wao. Baba Mtakatifu anatoa mifano kwamba, tazama Yosefu na
Maria, na wachungaji wa Betlehemu. Usiku wa Krismasi ya kwanza dunia yote ilikuwa
imelalia utajiri wake na mali zake, Wakati huo wanyenyekevu walikuwa wakiandaa kwa
kimya mapinduzi ya wema. Walikuwa masikini wa kila kitu na waliishi kimasikini, lakini
walikuwa na utajiri mkuu wa thamani ya kuishi katika ulimwengu huu wakiwa hasa na
utashi wa mabadiliko.
Baba Mtakatifu anasema, wakati mwingine kuwa na kila kitu katika maisha ni bahati
mbaya. Fikirieni kijana ambaye hakufundishwa kuwa na karama ya subira na uvumilivu,
ambaye hajawahi kutoa jasho la jambo lolote, au ambaye ameunguza hatua zake zote kabla
ya kufikisha miaka 20, anatambua dunia ya leo inakwendaje. Hii ina maana ya hatari,
kwa maana umefungia mlango wa shahuku na ndoto, utafikiri ni kijana lakini ndani ya
moyo wake amekwisha shuka katika kipindi cha vuli.
Baba Mtakatifu anfafanua, kuwa na moyo mtupu ni kizingiti kikubwa cha matumaini.
Ni hatari dhidi ya matumaini katika safari ya maisha ya kikristo.
Iwapo Mkristo anakumbana na hali hiyo, lakini anatambua namna gani ya kupambana nayo.
Mungu amemuumba kwa sababu awe na furaha tele na aondokane na mawazo ya ubaya. Ndiyo
maana kuna haja ya kuulinda moyo dhidi ya vishawishi, dhidi ya furaha ambayo kiukweli
vishawishi hivyo havitoki kwa Mungu. Iwapo vinaweza kujitokeza ndani ya moyo ukawa
na machungu, basi tunaweza daima kukimbilia jina la Yesu . Tunaweza kurudia sala
rahisi ambayo inapatika katika Injili isemayo Bwana Yesu Kristo Mwana wa Daudi unihurumie
mimi dhambi. Ni sala nzuri yenye kuwa na matumaini ya kwamaba na mwekeza Yesu amabaye
ana uwezo wa kufungua milango na ya kutoa suluhisho la matatizo na kufanya utazame
upeo wa matumaini.
Sisi si peke yetu katika kupambana dhidi ya kukata tamaa. Yesu aliushinda ulimwengiu
na anaweza kushinda ndani mwetu iwapo tutakimbilia katika wema. Iwapo Mungu yupo nasisi
hakuna anayeweza kuiba ile fadhila ambayo sisi tunahitaji ili kuishi, na hakuna anayeweza
kuiba matumaini anasema Baba Mtakatifu.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |