2017-09-27 16:36:00

Papa atoa ujumbe kwa familia ya Shirika la Mt. Vincenzo de Pauli


Katika maadhimisho ya miaka 400 ya kuanzishwa maisha ya familia yenu, ninapenda kuwashukuru na kuwatia moyo kwa kuonesha thamani na maisha yanaoyoendelea katika Mtakatifu Vincezo wa Pauli. Ni maneno aliyo anza nayo Baba Mtakatifu Francisko tarehe 27 Septembwa kwa watawa wa Shirika la upendo la Mtakatifu Vincenzo wakati Kanisa linaadhimisha siku yake inayokwenda sambamba na miaka 400 ya kuanzishwa kwa Shirika hilo. Katika kueleza juu ya miaisha ya Mtakatifu Vincenzo, Baba Mtakatifu anasema aliishi daima katika safari kwa kujifungua wazi wa kumtafuta mungu na yeye mwenyewe.

Na katika tendo la kumtafuta linajikita katika neema ya kuwa mchungaji na kukutana na Yesu Mchungaji mwema katika uso wa watu maskini. Yeye alikuwa mtu aliye jawa na huruma kwa familia nyingi hasa wa mwisho. Alitambua uso wa Yesu ambao ulijitambulisha katika kuhudumia maikini bila kujibakiza.
Katika shahuku ya kumtambua Yesu kwa njia ya masikin alijitoa maisha yake yote kutangaza kwa njia ya umisinari na kuwasaidia kwa namana ya pekee mafunzo wa makuhani. Baba Mtaktifu anasema, Mtaktifu Vincenzo wa Pauli alikuwa mtu wa aina yake katika matendo na utarahi. Maneno yaliendana na matendo na kumfanya atumikie kwa ukarimu Kanisa. Kwa njia hyo mwaka 1647 kama mbegu ndogo ya aradali, alianzisha Shirika la Kimisionari , Shirika ambalo likawa na matawi mengi yaliyounda taasisi na vyama vya kitume kufanya uwe mti mkubwa.

Familia hiyo ilianza ikiwa ni mbegu ndogo ya aradali na ndiyo maana Mtakatifu Vincenzo hakuwa anataka kuwa mstari wa mbele, bali kuwa mdogo kama hiyo mbegu lakini yenye msingi wa unyenyekevu na ukarimu wa kujihusisha kutoa maisha wakti inakufa ardhini.
Hiyo ndiyo tasaufi ya Shrika la Mtakatifu Vincenzo wa Pauli kujikita kwa binadamu na jamii aliyeadhrika, aliya na majeraha na kubaguliwa. Ndiyo tasaufi ya utambuzi kwamba wanaweza kutoa huduma hali kwa wale wa maisho na wanyenyekevu.

Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko anawatakia heri ya kwamba katika mwaka huu wa kushukuru Bwana na kutafakari kwa kina karama yao ya shirika iwe fursa kwao kuchota katika chemichemi ya mwanzilishi wa shirika.Anasisitiza wasisahau kuchota ile neema itokayo katika mwamba wa upendo ambao ni mfano halisi wa upendo. Mwamba huo ni Yesu, anayewatuma waende kwa masikini na wasio kuwa na sauti. Wanapokutana na ubinadamu dhaifu, uliotengwa, wanaoishi katika maisha maigumu, watambe kuwa pale ndiyo mwamba , lakini mwamba huo unapoegemewa unatoa faraja na wala siyo kizingiti , ugumu au utofauti. 

Wao wawe ndiyo kiegemezo chepesi kwa wote wenye kuwa na matatizo ya maisha ya binadamu kama Neno la Mungu kupitia Isaya 51,1 lisemalo  “kwa maana utazameni mwamba mlimochongwa  chimbo la mawe mlimochimbuliwa”. Wameitwa kuwafikia wote katika sehemu za pembezoni ili kuweza kuwapelekea siyo tu uwezo wao wali nao  bali Roho wa Bwana na  Baba wa maskini. Ni yeye anayewatawanya kama mbegu ili iweze kuota katika ardhi iliyo kauka, au kama mafuta ya kuweza kuwatuliza wenye majeraha,  kama moto wa upendo ili kuwapa joto mioyo mingi iliyo na baridi sababu ya kubaguliwa. 

Kama Kristo aliyetumwa na Baba kutangaza Habari njema kwa masikini , Kanisa limekabidhiwa utume huu kwa wote wanao zungukwa na matatizo ya kibinadamu na  kuwatambua masikini ambao ni mfano wa Yesu kama vile mwanzilishi wa Shirika . Mtakatifu Vincenzo wa Pauli alianzisha njia mpya ambayo hata leo hii inazidi kujieleza kwa kila mmoja katika Kanisa Baba Mtakatifu anaongeza.Ushuhuda wake leo hii na daima unazidi kwenda mbele, kuwa tayari daima kwa wale ambao wanakubali mapenzi ya Bwana.

Baba Mtakatifu pia anawakumbusha na kuwaonya  wawe na lugha rahisi , wasishikilie mambo ya kiulimwengu ambayo yanaleta vizingiti katika utume wao.
Anamalizia akiomba kwa ajili ya Kanisa na kwa ajili yao ili wapate neema ya kukutana na  aliye na njaa , kiu mgeni , aliye uchi, mgonjwa mfungwa , mwenye mashaka , mjingwa , mwenye dhambi, virigu , mgomvi na kila aina ya mteswa katika Kristo kwa ajili ya kumtuliza.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.