2017-09-27 16:19:00

Telegram ya Papa katika tukio la Siku ya kupambana na Ujenzi wa Vizingiti kijamii


Telegram ya Baba Mtakatifu Francisko iliyotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin Katibu Mkuu wa Vatican kwa ajili ya tukio la  toleo la 15 kuhusu Siku ya Kitaifa kwa ajili ya kupambana na vizingiti vya kijamii katika mfumo wa ujenzi wa maendeleo ijulikanayao kwa jina la  FIABADAY itakayofanyika tarehe 1 Oktoba 2017.

Katika ujumbe wa Baba Mtakatifu anasema  fursa ya toleo la 15 la siku ya kimataifa  kwa kupambana na vizingiti vya kiujenzi ambayo inafanyika tarehe 1 Oktoba;  mawazo yake yanawaendea wote wanao jikita katika kuhakikisha zinakuwa fursa ya maisha kwa kila mtu, kulingana na hali , kimwili na kijamii, aidha kuhamasisha mabadiliko ya utamaduni unaojihusisha na kupambana na vizingiti dhidi ya maisha .

Ni matumaini ya Baba Mtakatifu  ya kwamba unakuwapo utambuzi wamisngi hiyo ambayo inaaweza kuchangia  na mani ya kikristo katika makuzi ya binadamu na jamii. Na njia hizo zinaweza kuwa chachu zaidi ya matendo ya kuhamasisha binadamu katika udugu wa mshikamano na kuheshimu hadhi ya kila binadamu , wakati huo huo anawaomba wasali kwa ajili kuombea huduma yake. Kwa maombezi ya Bikira Maria anawapa baraka kwa viongozi na wote wanaoshiri katika tukio hili la muhimu .

Na Taarifa  zaidi kutoka  Agenpress ni kwamba, tarehe 28 Septemba 2017 Katika ofisi za Baraza la Ushauri nchini  Italia utafanyika mkutano kwa vyombo vya habari kuhusiana na Siku ya Kitaifa kwa ajili ya kupambana na vizingiti vya kijamii, ni siku ijulikanayo FIABADAY ambayo inafanyika kila mwaka na saa ni mwaka wa 15. 
Siku ya kuwasilisha FIABADAY 2017 katika vyombo vya habari watatoa ripoti ya kaai iliyofanyika kwa mwaka mzima kwa ushirikianao wa mamlaka ya umma na binafsi katika usambasji wa utamdanu wa ulimwngi kuhusu fursa mbalimbali,matoke yaliyofikiwa pia malengo ya kufuata.
Kauli mbiu ya kwa mwaka huu inasema umuhimu wa mafunzo  kwa ajili ya keeleimisha uwezekano wa kila mmoja. Kwa miaka  hii mambo memngi yaneshafanyika kama vile  utoaji wa kozi za mafunzo ya walimu wa kila ngazi, na pia mafunzo mengine ya kudumu kwa walimu. Kozi za mafunzo ya wataalam, kwa ajili ya kupingana na vizingiti hivyo vya ujenzi wa jamii aidha pia kozi kwa ajili ya mafunzo ya waandishi wa habari na mafuzo mengine yanayohusu watu walemavu. 

 Kwa njia hiyo lengo ni kutaka kutoa rangi  na sura mpya katika jamii  ambayo iwe na mawazo ya kimaendeleo na kuona umuhimu wa kuhamasisha hasa katika  kuongeza ufahamu kati ya serikali za mitaa kati ya  mashirika, makampuni, vyama na raia binafsi kuhusu kukomesha vikwazo vyote, sio tu ya kimwili, bali hata  kuwashirikisha wachezaji katika miradi ya kuingizwa kwa jamii wazi na huru katika mpango huo wa FIABADAY .

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.