2017-09-25 16:03:00

Mahubiri ya Papa wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana 24 Septemba


Katika ufalme wa Mungu hakuna asiye kuwa na ajira, wote wanaalikwa kupata sehemu ya kazi, na mwisho wake kila mmoja atapata haki ya Mungu  na siyo ya binadamu kwa bahati yetu njema. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri yake siku ya Jumapili 24 Septemba 2017 wakati wa sala ya Malaika ya Bwana kwa mahujaji wote wote waliokuwapo kwenye viwanja vya Mtakatifu Petro Vatican. Ameyatamka maneno hayo akiwa anatakakari Injili ya kuhusu wafanyakazi wa siku kutoka katika Injili ya Mtakatifu Matayo Mt 20,1-16.

Baba Mtakatifu anasema mambo mawili ni lazima kuyatamza katika ufalme wa Mungu,Yesu anataka kueleza, kwanza Mungu anawaita wote kufanya kazi kwa ajili ya Ufalme wake, pili kwamba mwisho wake anataka kuwapa kila mmoja mshahara ule ule, kwa maana ya ukombozi wa maisha ya milele.
Kutokana na hiyo, haki hiyo, inasabisha lakini hali ya wivu kwa wafanyakazi wengine walioitwa tangu asubuhi na kulipwa sawa sawa na wale waliofanya kazi masaa machache. Mwenye shamba anaamua kuwapa kila mmoja mshahara ule ule, Baba Mtakatifu anaendelea, ni kwa sababu Yesu anataka kufungua mioyo yetu katika mantiki ya upendo wa Baba ambaye ni mwema na mwenye huruma.

 Na kama mantiki ya binadamu imejikunja katika ubinafsi, kwa kujifikiria wao binafsi, kama asemavyo Nabii  Isaya,  Papa anatoa ushauri kuwa ni lazima kushangazwa na mawazo ya njia za Mungu ambazo siyo mawazo yetu na wala njia zetu.
Akimaliza tafakari hilo,  Baba Mtakatifu Francisko anawakabidhi kila mmoja kwa Bwana ili aweze kusikiliza  maombi maisha yetu na hasa ya kuweza kuwa na mantiki ya upendo unao tukomboa na kuachana na mitazamo tofauti na mawazo  ya Mungu kwa wengine. Tuwe na  mawazo mema juu ya wengine na ukarimu. Aidha anawalika wote kujizatitit katika maisha ambayo ni ya kujibidisha. Hiyo ni kutokana na kwamba  Mungu hamtupi hata mmoja, anataka kila mmoja aweze kufikia maisha makamilifu na ndiyo maisha ya kweli na maisha ya Baba Yetu.

Baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu amemkumbuka Padre Mmisionari katika nchi ya Guatemala, Stanley Francis Rother aliyeuwawa mwaka 1981 akiwa na maiaka 46 tu. Padre Rother ametangazwa Mwenye heri  huko Oklahoma  Marekani tarehe 23 Septemba 2017 kwa ajili ya jitihada zake za ujilishaji na kuhamasisha maisha ya binadamu hasa kwa masikini. Mfano wake wa kijasiri anasema Baba Mtaktifu, uweze kusaidia  hata sisi kuwa wajasiri  na kushuhudia Injili, na katika  kujikita kukuza hadhi ya binadamu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.