2017-09-23 13:28:00

Mwenye Heri mpya Padre Rother huko Oklahoma kati ya watu wake hadi mwisho


Walikuwa hawataki kumruhusu kupata daraja Takatifu la Upadre, kwasababu alikuwa mdhaifu katika taaluma, lakini baada ya kupata daraja lwa upadre, alionesha ujasiri mkubwa na kuwa padre wa kweli katika urafiki na ndugu wote zaidi wale masikini.
Utume wake ulianzia kwa  watu asili wa tzutuhil nchini Guatemala, watu ambao hawakuwa na maisha bora, walikuwa wametengwa , hawakuwa na elimu na mambo muhimu ya kuweza kuishi. Padre A’plas, kama alivyoitwa na watu wa asili, kwa jina la ubatizo ni Francis Stanley Rother (1935-1981) aliyelipa maisha yake katika kujitoa kutangaza Injili kwa watu hao.Kwa bahati mbaya mikononi mwa watu watatu wakakatisha uhai wake tarehe 28 Julai 1981 akiwa katika  nyumba yake ya parokia. Kabla ya kuwawa alikwa ameshauriwa akimbie kuacha nchi ya GUATEMALA, lakini kama mchungaji mwema alitaka kubaki na zizi lake hadi mwisho.

Ni kutokana na ujasiri huo ambapo Kanisa Katoliki limetambua karama za utakatifu wakea  na kwa njia hiyo tarehe 23 Septemba 2017  mji wa Oklahama, Marekani Kardinali Angelo Amato, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya mchakato wa watakatifu  akiwakilisha Baba Mtakatifu Francisko anamtangaza Mwenye Heri  Mfiadini. Historia ya mashia yake: Padre Francis Stanley Rother alizaliwa tarehe 27 Machi 1935 na Baba Franz na mama Getrude Katherine Smith katika Jumuiya Katoliki kutoka  Ujerman kwenye mji wa Okarche huko Oklahoma. Alikulia katika mazingira yenye misingi mikuu ya dini Katoliki. Septemba 1953 alijiunga na Seminari ya Mtakatifu Yohane, baadaye alihamia katika Seminari ya Kupalizwa Mbinguni katika Mji wa Texas.

Baada ya kushindwa kufuzu baadhi ya masomo, Askofu Victor Reed  wa Jimbo la Oklahoma na Tulsa alimpatia fursa ya pili kuendelea na masomo. Juni 1959 alitumwa kuendelae na masomo ya kiada wakati wa kiangaza kwenye Seminari ya Mkingiwa dhambi ya asili, huko Missouri ili kujiendelea kwenye lugha ya kilatini. Baadaye akatumwa tena  kurudia masomo ya Taalimungu Katika Seiminari ya  Emmitsburg huko Maryland. Gombera wa seminari hiyo aliweza kutambua mara moja, uwezo wake wa akili ya kawaida lakini zaidi uadilifu, juhudi zake katika maisha ya  sala na kazi, kwa njia hiyo Askofu Reed akampa daraja Takatifu la upadre tarehe 25 Mei 1963. 

Kwa miaka 5 ya kwanza Padre Rother alihudumia Parokia tofauti huko Durant, Tulsa  na Oklahoma, akionesha kwa namna ya pekee ule uwezo wa mahusiano mazuri na jirani , hasa uwepo karibu na watu masikini na walio baguliwa. Watu walianza kuzungumzia kuwa padre huyo alikuwa mkarimu na mwema. Mwaka 1968 alipelekwa katika utume wa Jimbo la Oklahoma ambao walikuwa wamezindua huko  Santiago Atitlán nchini Guatemala. Mji ulikuwa kando ya ziwa la Atitlán na maarufu kwa ajili ya uzuri wake wa asili, vilevile ulikuwa unajulikana ni mji wa watu maskini kiroho, na kimwili. Walikuwa ni watu wa asili ya  tzutuhil wasio kuwa na chakula na walikuwa wanateseka na ukosefu wa elimu na magonjwa mbalimbali. Akiwa kijana padre kutoka Marekani alianza jiitihada nyingi ikiwa ni  ujenzi wa Kanisa, nyumba ya mapadre, siyo hayo  tu bali hata kuanza kuelimisha makatekista, na ujenzi wa kituo cha afya huko  Panabaj. Vilevile  alianzisha kituo cha matangazo ya radio kwa kuendesha vipindi vinavyohus  mafunzo ya dini na kijamii, ambapo mpango huo wa elimu ya dini na jamii uliweza kuongeza kwa kiwango kikubwa cha maisha katika sekta ya kilimo na lishe.

Kwakuwa wakazi wengi walikuwa wanatumia lugha mbalimbali Padre Stanley, kwanza  alijifunza lugha ya Kihispaniola kisha lugha ya asili ili aweze kuhubiri, kuwaongoza katika uongofu, kufundisha na kutoa sakramenti. Pamoja na wahudumu wengine katika utume wake, alianza kutafsiri Neno la Mungu la Agano jipya ili kuweza kuadhimisha misa ya kawaidi katika lugha ya asili. Katika  juhudi hizo za kuwa na ukarimu na unyenyekevu watu walimpenda sana na kumpa jina la Padre A’plas. Katika eneo hili ambalo lilikuwa masikini bila kuwa na simu au zana zozote za mawasiliano, Padre Rother alifanya juhudi pia ya kuanzisha mambo mengi ikiwa ni pamoja na mafunzo ya watu mahalia na kutafuta makatekista na watu wenye uwezo wa kuendesha kituo cha radio.

Mwaka 1975 akawa paroko wa utume wa Santiago ya Atitlán na alikuwa padre mmoja tu aliyekuwapo katika parokia hiyo. Lakini wakati hu huo huo nchini Guatemala ukazuka mgogoro wa kisiasa na  kuangu kwa kwa  urais wa nchini  Jacobo Arbenz Guzmán. Ni kipindi kilichotokea  machafuko makubwa. Mwanzoni mwa 1981, padre Rother alipata taarifa kuwa jina leke lilikuwa kwenye orodha ya wale waliokuwa katika hatari ya kifo na walimshauri aondoke haraka kuacha nchi hiyo.

Pamoja na  hayo alikuwa ameamua kurudi Marekani Januari 1981 na  kabla  kuondoka alikuwa amepata  hata visa ya rafiki yake padre Pedro Bocel. Lakini Aprili 1981 Padre Rother alijisikia kutokuwa  mbali na utume wake na ndipo aliamua kurudi Guatemala. Pamoja na kwamba alishauriwa kutokanyaga eneo  la Santiago alijisikia kuendelea kutumikia Parokia yake kwa maana alisema mchungaji haweza kukimbia na kuwacha mifugo yake katika hatari. Tarehe 28 Julai 1981 maaskari walifika wakiwa wameziba nyuso zao waliingia katika nyumba yake na kumuua kwa risasi. Kwa namna hiyo ilitimilizika shahuku yake ya kutoa maisha yake yote hadi mwisho kwa ajili ya kutumikia Mungu kwa watu wa tzutuhil. Mwili wake ulikuwa kwanza umelazwa katika Kanisa Kuu la Mama yetu wa msaada huko Oklahoma,  lakini kwa maombi ya wanaparokia wa  Guatemala, masalia yake yalihamishwa katika Kanisa la Parokia ya Santiago Atitlán.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
 








All the contents on this site are copyrighted ©.