2017-09-21 15:21:00

Rais Conde wa Gunea amesema inahitajika zaidi sauti ya Afrika katika


Uwepo wa idadi kubwa ya wawakilishi wa Afrika katika Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa, ni maombi kutoka katika Wakuu wa nchi za Afrika ambao wamewasilisha  kwenye Mkutano  Mkuu wa Umoja wa Mataifa tarehe 19 Septemba 2017  pia suala la mageuzi ya Shirika la Umoja wa Mataifa limejadiliwa.Pamoja na viongozi kadhaa wa nchi za Afrika kupewa nafasi ya kuzungumza kwenye jukwaa la Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York siku ya Jumanne 19 Septemba, Alpha Condé alikuwa kiongozi wa kwanza kutoka Afrika kuzungumza katika Mkutano huo.  Bwana Alpha Rais wa Guinea, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, ameomba kupewa nafasi zaidi ya uwakilishi wa  Baraza la Usalama katika Umoja wa Mataifa. 

Rais Alpha Conde anasema, Afrika haiwezi tena kubaki kwenye vikwazo vya maamuzi makubwa ya kimataifa kwa sababu bara hilo, leo imeamua kuchukua udhibiti. Afrika kwa kipindi kilichopita ilitawaliwa na utumwa, sasa imeshinda na kuamka ili kuamua kuchua hatima yake kwenye mikono yakena kuweze kuwa mtendaji mkuu wa maendeleo yake, na kuweza kukabiliana na masuala ya Kimataifa. Katika  Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa nafasi nyingine alipewa, Rais Ibrahim Boubacar Keïta wa nchi ya Mali, ambaye alisifu kuundwa kwa kikosi cha kikanda cha G5 Sahel,  kitakachopambana dhidi ya ugaidi. Ametoa wito kwa nchi zote  rafiki na mashirika ya kimataifa ili kusaidia kifedha kikosi hiki cha kikanda katika mkutano wa wafadhili wa kimataifa uliopangwa kufanyika tarehe 16 Desemba mjini Brussels. Kikosi cha G5  kinaundwa na nchi ya Mali, Burkina Faso, Ciad, Niger e Mauritania.

Rais wa Mali amesema, nguvu ya umoja ni muhimu kwa matumizi ya umma na kimataifa. Mapambano yanayoendelea katika Sahel ni Bwawa. Anaongeza Rais wa Mali; iwapo inaweza kuanguka itakuwa ni bahati mbaya kwa dunia nzima iliyostaarabika, na ambayo inashiriki maadili yetu .
Pia katika mkutano huo hata Muhammadu Buhari amezungumza siku ya Jumanne 19 Septemba. Rais wa Nigeria ambaye hali yake ya afya imedhoofika kwa maradhi ameweza kuzungumza kwa sauti ya udhaifu lakini bila kushindwa, hali inayosibu nchini mwake, lakini pia alizungumzia kuhusu migogoro na masuala ya kimataifa.

Kabla ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliahidi kuongeza sehemu ya pato la Taifa lililotolewa kwa msaada wa maendeleo rasmi. Msaada huo ulikuwa 0.38% mwaka 2016 na utafikia 0.55% katika miaka mitano ijayo. Pamoja na Rais Macron, pia  amekuwepo kiongozi wa Kidiplomasia wa Ulaya Federica Mogherini wa Italia na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ambaye alikuwa kwa mara ya kwanza kuwakilisha Marekani katika kitengo cha usalama wa ndani.

Katika suala la fedha kwa ajili ya nguvu ya kupambana na ugaidi huko Sahel, Utawala wa Donald Trump umeonyesha kujihusisha kwa kufungua dhana ya kuchangia hata kiuchumi. Umoja wa Ulaya bado haujatoa ruhusa ya euro milioni 50 kwa ajili ya nguvu ya pamoja waliyo kubaliana kuitoa kwenye vikao vilivyofanyika kwa miezi ya karibuni. Lakini ili kuweza kufanya operesheni ya kazi hiyo bado zinakosekana  milioni 515  za dola. Mkutano wa wafadhili  juu ya ajenda hiyo huko Brussels unatarajiwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.