2017-09-21 14:30:00

Miaka 25 ya Mahusiano ya Kidiplomasia kati ya Vatican na Armenia


Jumatano 20 Septemba 2017 Kardinali Leonardi Sandri Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa lwa ajili ya Makanisa ya Mashariki ameadhimisha Misa Takatifu kutokana na tukio la miaka 25 ya mahusiano ya Kidiplomasia kati ya Vatican na Jamhuri ya nchi ya Armenia. Misa hiyo ilifanyika katika Kanisa La Mtakatifu Nicola wa Tolentino kwenye Taasisi ya Chuo cha Kipapa  cha Armenia.

"Tunakutanika kwa pamoja kuadhimisha ishara kubwa ambayo tumepewa kama mahujaji katika katika ardhi hii ya kuweza kuwa washiriki katika neema ya Roho Mtakatifu, umoja halisi wa sadaka ya Kristo aliyetoa maisha juu ya msalaba. Lakini Mauti hayakuweza kabisa kutawala maisha yake aliyotoa kwa baba yake na ndugu. Yeye anaishi, amefufuka siku ya kwanza ya Juma miaka elfu mbili iliyopita ". Ni utangulizi wa mahubiri aliyo anza nayo Kardinali Sandri wakati wa maadhimisho ya misa ya kukumbuka miaka 25 iliyopita ya mahusiano kati ya Vatican na nchi ya Armenia. Kardinali Sandri anabainisha kuwa kadiri ya mtirirko wa nyakati za binadamu  unavyoipa ndiy unazidi  kujaa ukamilifu na uwepo wa uhakika wa zawadi ya yule anayeongozua watu na mataifa. Uwepo wa wote katika Kanisa pia wanashiriki kitoho na Baba Mtakatifu Francisko na viongozi wakuu  wa Kiptriaki Ghabroyan na Catholicos Karekin II.

Akielezea juu ya historia ya mahusiano hayo anasema, kwa njia ya pekee ni shukrani nyingi kwa Bwana kutokana na hatua ya hatua ya  miaka 25 ya mahusiano ya kidiplomasia ya Vatican na nchi ya Jamhuri ya Armenia. Mahusiano haya yamejaa mambo mengi kama mwanga, na kama nyota za mbinguni ambayo kila mmoja huonyesha hatua ya kukutana. Ametaja baadhi ya hayo kwa kuanza na Ziara ya Kitume  Mtakatifu Yohane Paulo II mwaka 2001 , Papa Francisko mwaka jana , ziara saba za Rais wa jamhuri ya Armenia Vatican na mambo mengine mengi tangu kuzinduliwa kwa mahusiano hayo mwaka 1992.  Ni safari ndefu, lakini kila moja ya matukio haya hutokea kwa wale ambao wameishi kumbukumbu ya kushukuru: kila hatua imetayarishwa na mikutano na majadiliano ambayo yameruhusu kuanzisha mahusiano makubwa ya kina, ya heshima na urafiki ambayo vimefanya kuwa uzuri zaidi na wenye utajiri wa kibinadamu, kimwili na kiroho, ambao ni uhusiano wa kidiplomasia.

Ni lazima kufikiria hatua za urafiki kama zawadi kweli ya Mungu , kwa njia ya kujitolea na kuwakabiribishana watu wote mbao waliokuwapo kabla: na hiyo iliwezekana kwa njia ya kutazama wafuasi wa Bwana ambaye ni mwalimu na Kristo.  ukurasa wa barua ya Mtakatifu Paulo kwa Timotheo kwa dhati ni  wimbo wa  kiliturujia ya Kanisa la kwanza, ni taaluma rahisi na madhubuti ya imani. Inajidhihirisha katika mwili wa binadamu katika  haki ya kutambuliwa kwa njia ya Roho,ameonekana na Malaika na kutangazwa kati ya mataifa, akaaminiwa  popote ulimwenguni na kuinuliwa juu katika utukufu.
Kardinali Sandri anaendelea na mahibiri yake, Neno la Mungu lilifanyika mwili na kuweka mwanga mpya wa maajabu ya utu wetu , uhusiano wa ukombozi ni dhana iliyoanzishwa kwa binadamu na kuwa chemichemi ya dhamana nyingine za kila siku ambapo wote tunaweza kuchota, kujifunza na kujitambua kwanza ile zawadi ambayo Mungu ametuumba na kutufanya tuwe walinzi na mashuhuda,vilevile kwa njia yake, sisi tumekombolewa na kuwa na mwanga. 
Kama alivyo sema Mtakatifu Yohane Paulo II alipotembelea nchi ya Armenia mwaka 2001 :  Kwa njia ya ubatizo jumuiya ya Armenia inazaliwa kwa upya ule  utambulisho wa watu ambao watafanya sehemu ya katiba isiyotengwa sehemu ya maisha ya kiarmenia.

Aidha kuwa , hakutakuwapo uwezekano wa kurifikiira kwamba miongoni mwa sehemu ya utambulisho huo, hauonekani  imani katika Kristo kama kipengele muhimu. Urithi huo pamoja  na kujivunia yaliyopita inaweka kifet mioyo ya maisha ya watu wa Armeni wa nyakati na kama wa nyakati za watu wote. 
Mwisho Kardinali Sandri anawataka wote wawe na uaminifu katika wito na kuwa na  matumaini; kufanya kumbukumbu  za wakati uliopita lakini katika mzizi endelevu ya Mungu. Mizizi hiyo endelevu ni ile ya haki , mapatano na amani.

Katika misa Takatifu wameshirikiana na Askofu Mkuu Boutros Maryati wa kiarmeni kutoka Aleppo Siria. Monsinyo Giorgio Chezza muhusika katika mahusiano ya Ubalozi wa Vatican Italia, Padre Lorenzo Lorusso Katibu msaidizi wa Baraza la Kipapa kwa akji ya Makanisa ya Mashariki ya, Gombera wa Chuo cha Kipapa cha Waremenia na mapadre wengine.  Baada ya maadhimisho hayo Balozi wa Armenia mjini Vatican, Askofu Mkuu Minasyan, ametoa salam zake na baada ya salama zilifutiwa nyimbo za mataifa mawili, pia hotuba fupi ya Balozi wa Armenia nchini Italia. Kwa upande wa wa katibu wa Vaticana amewakilishwa na Monsinyo Paolo Borgia  na Mkuu wa Protokolo za Vatican Monsinyo Bettancour .Pamoja na hao wamekuwapo idadi kubwa ya wawakilishi wa kidiplomasia, wengine kutoka mamlaka ya serikali ya Italia na viongozi wakuu wa majeshi.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.