2017-09-21 16:05:00

Kwa mujibu wa Ripoti ya Unicef, Milioni 27 ya watoto hawaendi shule


Watoto milioni 27 wameacha shule katika nchi 24 duniani zikiunganishwa na nchi zenye migogoro. Ni takwimu zinazo oneshwa katika ripoti ya Unicef wakati wa tukio la Mkutano wa Umoja wa mataifa mjini New York mapema tarehe 19 Septemba 2017. Kwa mujibu wa utafiti  kuhusu mafunzo ya watoto na vijana wahamiaji walio na elimu kidogo,  inaonesha hatari kubwa iliyopo pia unyanyasaji wa watoto.Kwa mujibu wa ripoti ya Unicef ya utafiti iliyofanywa kati ya watoto wanaohama kupitia  bahari ya Mediterranean kwenda Ulaya ni  asilimia tisini ya vijana wasio kuwa na elimu. Ripoti hiyo inaonesha kuwa watoto na  vijana wamekosa elimu kutokana na kutumiwa na kunyanyaswa  ikilinganishwa na asilimia 77 ya watoto wenye elimu ya shule ya msingi na asilimia 75 wa elimu ya sekondari.

Kwa mujibu wa Unicef, wakimbizi, wana uwezekano mkubwa zaidi  mara tano ya  kutohudhuria shule kulinganisha na  watoto wengine. Ni matokeo dhahiri kuwa ni asilimia hamsini tu walio jiandikisha shule ya msingi na chini ya asilimia 25 kwa wale wa shule ya Sekondari. Ripoti hiyo inaeleza kuwa  wasichana wahamiaji wanakabiliwa na hatari ya kipekee: hiyo ni kwasababu ya ongezeko kuwa la kuathirika kijinsia kwa mujibu wa ripoti ya Unicef. Na ni sawa sawa na picha halisi ya nchi zilizoathiriwa na mgogoro ambapo kuna uwezekano wa asilimia 25 zaidi wasio kwenda shule kuliko wavulana.

 Wakati huo huo,  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres anathibitisha kuwa dunia inakabiliwa na janga la kielimu na bila jitihada za hivi sasa, zaidi ya vijana milioni 825 kati ya vijana bilioni 1.6 wataachwa nyuma ifikapo mwisho wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) mwaka 2030. Akizungumza kwenye kikao mbashala wa mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu ufadhili kwa ajili ya elimu, mapema wiki hii, Bwana Guterres amesema yeye binafsi alishuhudia jinsi hatua za kuweka elimu kama haki ya msingi zilivyochochea maendeleo uendelevu na amani.

Kwa njia hiyo Bw, Guteres ameyataja  maeneo manne ambayo yanahitaji kuimarishwa na kwamba, hawali ya yote ni katika ufadhili ili kuwekeza katika elimu kwa ajili ya kuimarsiha maendeleo kiuchumi, pili, kulenga wasichana ambao wanakabiliwa na vikwazo ikiwemo ukatili wa kijinsia na tamaduni potofu, tatu kuhakikisha elimu ya muda mrefu kwa ajili ya stadi za kazi kwa siku zijazo na mwisho  kulenga watoto na vijana walioathirika na mizozo mingi na  ambao wanakosa fursa kwa ajili ya mazingira waliyomo.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.