2017-09-20 15:27:00

Ask. Zuppi:Tazama wakati endelevu kwa urahisi,ujasiri na tumaini


Lazima kuendelea kuzungumza mambo ya Mungu kwa watu na kwasababu hiyo tendo la kuwasili kwangu mwaka jana Jimboni Bologna imekuwa kwangu mwafaka wa kugundua kwa ufasaha tendo hili. Ni maneno ya utangulizi wa Askofu Mkuu Matteo Maria Zuppi wakati akizinduza tamasha la tisa la Kifranciskani mwaka 2017.Tamasha hilolitaanza tarehe 22-24 Septemba jijini Bologna likiwa ndani ya  shamrashamra za maandalizi ya kumpokea Baba Mtakatifu Francisko tarehe 1 Oktoba 2017.

Askofu Mkuu Zuppi akielezea juu ya tukio la Tamasha la Kifranciskani 2017, anasema kufurahishwa na tukio hili ambalo ni utumaduni wa kufanyika nje katika kufuata karama za mwanzilishi wa Shirika la kifranciskani, ambaye hata leo anawaalika wafuasi wake  waende katika mitaa na barabarani. Hilo siyo suala la kuchagua mahali pa kufaa au vifaa, lakini ni chaguo la kukutana, kuzungumza, kuelezea, kuelewa, kujadiliana na kufurahi kwa pamoja.
Askofu anaelezea historia fupi ya matembezi ya Mtakatihu huyo na kusema, huo ndiyo uchaguzi unaotimilika  katika matendo ya Mtakatifu Francisko wa Asizi kwa sababu mara ya kwanza alikupofika mji wa Bologna,hakutaka kuingia katika mji sababu Wafranciskani walikuwa wamejenga nyumba kubwa iliyokuwa imejaa vitabu. Yeye akasema sitaweza kukaa hapo, bali nitakwenda mitaani, na alipofika kwa mara ya pili, Mtakatifu Francisko alihubiri katika uwanja mkubwa.

Bada ya kusikiliza mahubiri yake maoni ya watu yalikuwa kwamba, anazungumza vizuri na kuhubiri vizuri kwasababu hakuhubiri kama kuhani, maana hakuzungumza kwa lugha ngumu bali alitumia lugha rahisi ambayo kila mtu alielewa. Kwa njia hiyo Askofu Mkuu anasema  ni  matumaini yake kuwa tamasha hilo la kifranciskani litaendelea kuongea  mambo ya Mungu kwa watu kwa kutumia lugha rahisi.
Akuzungumzia juu ya kauli mbiu ya tamasha isemayo “wakati ujao rahisi”, Askofu Mkuu Zuppi anaeleza: ndiyo, wakati ujao unaleta wasiwasi mkubwa wakati mwingine na hiyo ni kutokana na  kushikilia mambo ya  zamani au kukujaribu kuyatunza  kwa wakati uliopo. Lakini njia pekee ya kuweza kuhifadhi ya sasa ni kuangalia wakati ujao kwa njia rahisi, ambayo Mtakatifu Francisko wa Asizi aliweza kuishi bila kuepuka matatizo ya wakati ule bali kuyakabili na kuweza kuyatatua.

Mtakatifu Francisko alikuwa mtu rahisi, lakini alikumbana na kukubali mambo magumu na changamoto za wakati ule,  kwa maana  hiyo  kuzungumzia suala la siku zijazo rahisi ni kusaidia kutazama ulimwengu huu kwa ujasiri, lakini siyo kwa sababu ya kwamba tunaangalia kitu ambacho hakipo la hasha!  ni kutazama changamoto ambazo zinatusubiri na kwa njia ya hizo   tunaweza kupata ufumbuzi. Askofu Mkuu anamalizia akisema, ni kwa njia ya matumaini  tu yatasaidia kuona wakati ujao, wakati huo hayapunguzi au kumtolea kitu kwa wale walio vijana endelevu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.