2017-09-19 13:57:00

Ufilippini:Padre Chito ameachiwa huru baada ya kutekwa nyara na magaidi


Padre Tersito Chito Soganub , katibu wa Mkuu wa Jimbo la Marawi aliyekuwa ametekwa nyara na kikundi cha magaidi wa Serikali ya kiislam nchi Ufilippini, ameachiwa huru kwa njia ya operesheni ya  wanajeshi wa ufilippini kwenye usiku wa tarehe 16 Septemba 2017, kwa mujibu wa habari zilizoenea katika vyombo vya habari huko Manila.

Padre alitekwa nyara pamoja na kundi la waamini tarehe 23 Mei 2017 huko Marawi Kusini mwa  Ufilippini. Pade Chito amewekwa huru kwa njia ya operesheni kali ya wanajeshi karibu na Msikiti wa Bato moja ya ngome kubwa ya kikundi cha magaidi cha Maute wanao husika na utekaji nyara huo.
Taarifa zinasema, pamoja naye, alikombolewa hata na mateka mwingine ambapo mamlaka wameweza kumtambua ni nani japokuwa hawakutaja jina lake. Hali ya vurugu  huko Marawi Ufilippini imekuwa ni uwanja wa michezo ya kivita kati ya jeshi na magaidi kwa miezi hii ambapo imesababisha maelfu ya watu kukimbia pia uwepo wa uharibifu mkubwa wa maeneo ya mji huo. 

Na kwa njia operesheni kali  ya mgogoro huo inaonesha kuwa mwisho kwa njia ya maaskari wanahusika katika shughuli ya kuwasaka magaidi. Pamoja na hayo viongozi wa Serikali wanasema ili kuweza kufanya ujenzi wa mji wa Marawi, utahitaji mabilioni ya mapesa ya Ufilippini. Naye Rais wa nchi ya Ufilippini Bwana Duterte amesema, mfuko wa fedha za kwanza uliokuwa umepangwa  wa euro 820,000 hazitaweza kutosha katika ujenzi wa mji huo.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.