2017-09-16 16:39:00

Msiogope kushirikisha utajiri wa tasaufi ya Shirika lenu kwa walei


Ninawakaribisheni kwa furaha katika fursa yenu ya Mkutano Mkuu wa Shirika pia kumshukuru Mama Mkuu wenu kwa hotuba yake. Mmeunganika kwa pamoja kutafakari juu ya maisha ya Shirika, kusali na kuchangua pamoja njia ambazo Bwana anawaelekeza ili kuziweka kwenye matendo mapya katika hali hali ya karama ambayo Roho Mtakatifu  alizawadia Kanisa na ulimwengu kwa njia ya Mwanzilishi wenu Padre Jean Jules Chevalier.
Ni maneno ya utangulizi wa Baba Mtakatifu Francisko, asubuhi ya tarehe 16 Septemba 2017 mjini Vatican, alipokutana na watawa wa kike na kiume wa Shirika la Kimisionari la Moyo  Mtakatifu wa Yesu wakiwa katika tukio la Mkutano wao Mkuu. 

Baba Mtakatifu anasema kuwa,kauli mbiu walio ichagua wakati wa maandalizi ya mkutano huo ina maana kubwa kwasababu inasema, “Lakini wewe umeiweka divai nzuri mpaka sasa! (Yh 2,10). Iwapo lakini kwa kiasi kikubwa mnatambua na kushukuru thamani ya urithi wa mpango  na shughuli za kitume ambazo karama yenu hadi sasa zimejikita kwa undani kwa nusu muhongo wa maisha ya Shirika lenu na shukrani na uaminifu wa ndugu walio watanguliwa,kwa upande mwingine pia ni utambuzi vema ya kuwa utajiri wake na nguvu za Kanisa na ulimwengu bado zinahitajika kwa dharura.

Baba Mtakatifu anasema, katika kusikiliza Roho anasema nini leo hii katika Kanisa lake na kujifungua katika maombi ya kibadamu,wataweza kuchota katika kisima kitakatifu  kisichoisha karama mpya ya kuanza upya na kufanya utachaguzi kijasiri, kujieleza katika mambo mengi na mapya ya kimisonari ambayo wamekabidhiwa. Na hiyo ni kutokana na kwamba hali ya dunia ya sasa ikilinganishwa na wakati uliopita imebadilika kutokana na changamoto mpya za kazi ya uinjilishaji wa Kanisa ambapo inatakiwa kujikita katika uwezekani zaidi wa kutoa aina mbalimbali za divai mpya ya Injili ili kuwezesha kutoa furaha na matumaini kwa wengi.

Akielezea juu ya karama ya mwanzilishi wao wa Shirika, Baba Mtakatifu anasema, iwapo yeye alikuwa na lengo la kutangaza Moyo Mtakatifu wa Yesu, leo hii wao wanatambua vema karama hiyo na wanaweza n azidi kuwa kielelezo katika matendo yao  kwenye shughuli kutoa ushuhuda wa upendo mkuu na huruma ya Yesu kwa wote. Zaidi Baba Mtakatifu Francisko anasema kuwa mara nyingi amekuwa akiwaisitizia watawa kuwa, ni lazima kurudi  katika  kiini  cha upendo kwanza, kumtazamo Bwana Yesu Kristo ili kujifunza kutoka kwake namna ya kupenda kwa moyo wa Kibinadamu, kutafuta na kuwasaidia kondoo waliopotea na wenye majaraha, aidha kujikita katika kutafuta haki, mshikano na wadhaifu,masikini kuwapa matumaini na adhi kwa wale waliotengwa.

Kadhalika kwenda mahali ambapo binadamu anasubiri kusikilizwa na kusaidiwa. Kutumwa kama wamisionari katika ulimwengu ndiyo Injili ya kwanza ambayo Kanisa linawawakabidhi. Kwenda  kujionesha kwa watu kwa njia ya vitendo vya dhati na upendo upeo wa Mungu mkarimu kwa walio wadogo, wadhaifu, na waliobaguliwa katika ardhi hii. Pamoja na kwamba Shirika lao limeteseka kwa miaka ya mwisho kutokana na upungufu wa miito kama hata ilivyo kwa mashirika mengine,Baba Mtakatifu anasema  lakini pia kuna ongezeko kwa miito katika Bara la Amerika ya Kusini , Australia na Barani Asia, ambapo shrika lao linpata matumaini hai kwa wakati endelevu. 

Kutokana na hili, Shirika leo anasema, linaweza kuongeza mafunzo zaidi ya kikristo kwa vijana ili kutambua karama ya Shirika lao  na hata kwa kutoa matumanini mapya ya kuendeleza huduma za ya Shirika katika dunia. Baba Mtakatifu anasisitiza pia jinsi gani ilivyo dharua leo hii kazi ya kuelimisha na kuwasindikiza kizazi kipya katika utambuzi wa thamani ya kibinadamu na kutoa ushuhuda mkubwa wa upeo wa Injili ya maisha na historia. Hiyo ndiyo kweli kinachoitwa dharura ya kuelimisha, zaidi ya hayo baba Mtakatifu anaongeza, na hiyo ndiyo mojawapo ya mipaka ya utume wa kuinjilisha ambayo Kanisa na jumuiya nzima ya kikisto inapaswa kutoka nje na kufanya. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko anawatia moyo kuendela  kujieleza utume wao kwa matendo katika mataifa .

Pamoja na hayo anawasifu uwepo wa wanashirika wengi katika Shirika hilo lakini pia anatoa onyo kubwa ya  kuepuka mabaya ya ulimwengu huu wa watawa kujiingiza katika mawazo ya kiulimwengu huu ambapo hautoi mfano hai wa Kristo na kusababisha  watu waende mbali na Kanisa na hasa kwa upande wa vijana. Kwa hiyo anawakumbusha, kwa kusisitiza  mara nyingi juu ya suala hilo, kwa njia hiyo anawasihi waishi maisha ya kindugu katika jumuia, wakikaribishana wote na kuthaminiana utajiri wa kila mmoja alio nao. Wasiwe na hofu ya kushirikiana na walei ambao wanaweza kuchota utajiri wa tasaufi ya karama ya shirika lao. Kwa njia hiyo watawa wote wa kike na kiume wa Shirika hilo wawe daima kitu kimoja  kama familia ya kiroho ambayo inajiunda kwa upya na zaidi katika karama ya mwanzilishi wao.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.