2017-09-15 15:35:00

Mama Maria wa Mateso ni mfuasi wa kwanza,jasiri na mwenye nguvu


Ijumaa tarehe 15 Septemba, kwa mara nyingine tena mara baada ya kufungua misa zake za kawaidai katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta Baba Mtakatifu Francisko, anawaalika wote kutafakari juu ya Mwenye Heri Bikira Maria mama wa mateso, akiwa chini ya msalaba. Anasema hayo kutokana na kwamba Kanisa Katoliki kila tarehe 15 ya mwezi Septemba inaadhimisha kumbukumbu ya mama Maria wa Mateso. Lazima kutafakari Mama wa Yesu, na kutakafakari ishara hiyo ya kupingwa maana Yesu ni mshindi juu ya Msalaba. Ni jambo la kupingwa  kutokana na kutoweza kutambua fumbo hili. Ili kuweza kutambua inahitaji imani kubwa, angalu kuwa na chembe ndogo ya  utambuzi huo ili kukaribia katika fumbo hili.

Baba Mtakatifu Francisko ansema, Mama Maria alitambu jambo hili na ndiyo maana aliishi maisha yake yote katika moyo ulichomwa mkuki . Alimfuata Yes una alikuwa akisikia maneno mengi kutoka kwa watu, hata waliokuwa wakimpinga japokuwa  walikuwa daima wakamfuata nyuma yake. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anasisitiza kuwa, kwa maana nyingine unaweza kusema Maria alikuwa mfuasi wa kwanza. Maria Maria alikuwa na uchungu  kama wa upanga ambao uliunda ishara ya kupingwa ndani ya moyo wake. Lakini yeye alivumilia  katika ukimya wake chini ya Msalaba akimtazama mwanae. Anaongeza, labda hata aliweza kusikia maneno ya kejeli kama vile: tazama mwanamke yule ni mmojawapo wa majambazi hao waliosulibiwa. Lakini yeye aliendelea kuelekeza uso wake kwa mwanae aliyetundikwa msalabani.

Baba Mtakatifu anathibitisha: ndiyo maneno ni madogo nisemayo lakini lengo lake  ni kutaka kusaidia kutafakari kwa kina fumbo hilo. Kwa maana Mama Maria muda ule alizaa Kanisa kwa ajili wote. Inathibitisha katika maneno ya Yesu akisema, “mwanamke tazama wanao”, kwa maana yeye  hakutamka mama bali alitamka mwanamke. Huyo ni mwamke mwenye nguvu, jasiri, ni mwanamke  aliyekuwa pale msalabani ili aseme  huyo ni mwanangu bila kumkana. Anamalizia kwa kusisitiza juu ya kutafakari zaidi Injili ya siku, na kwamba Roho Mtakatifu asaidie kila mmoja   kusema kile ambacho anahitaji.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.