2017-09-14 15:49:00

Papa ametoa hotuba kwa Maaskofu wapya waliowekwa wakfu mwaka huu


Kwa furaha kubwa ninawakaribisheni muda huu mkiwa ukingoni mwa hija yenu katika maeneo ya Roma, iliyo andaliwa na Baraza la Kikapapa kwa ajili ya Maaskofu na Makanisa ya Mashariki.  Shukrani pia zimwendee Kardinali Marc Quellet na Kardinali Leonardo Sandri ambao ni Wenyeviti wa mabaraza hayo ya kipapa kwa jitihada zao za kuwezesha tukio hili ambalo ninalitambua  binafsi, kutokana na hawa wachungaji wapya wa Kanisa kuweza kujikita kwa undani na kutafakari neema na wajibu wa kitume tulio upokea.

Ni utangulizi  wa maneno ya Baba Mtakatifu Francisko  tarehe 14 Septemba 2017 alipokutana na Maaskofu waliowekwa wakfu kwa siku za hivi karibuni wakiwa katika hija ya pamoja mjini Vatican. Kwa hakika anasema, siyo katika mashaili  yao bali ni kwa neema ya Mungu ambaye amewakabidhi ushuhuda wa Injili ya neema ya Mungu  na utume wa Roho yake. Mpango wa hija yenu  mwaka huu Roma Baba Mtakatifu anasema, umejikita katika kutafuta na kuingia kwa undani zaidi wa fumbo ambayo ni mojawapo ya wajibu msingi ule wa kujitoa kabisa katika zizi kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye aliwaweka kama walinzi (At 20,28), katika mang’amuzi ya kiroho na ulazima wa uchungaji  ili kuwa na utambuzi  na kutimiza kwa njia ya mapenzi ya Mungu ambaye ni kisima cha neema.

Baba Mtakatifu Francisko anaomba kushirikisha zaidi  juu ya mambo kadhaa ya tafakari kuhusu mada hiyo ambayo ni muhimu sanakwa nyakati hizi. Anasema, nyakati hizi ni zile zinazoenekana alama ya binadamu kupenda kujitegemea na kujitosheleza na kutangaza mwisho wa kipindi cha ualimu  katika upweke wake. Lakini hiyo inaonekana wazi kuwa, binadamu kamili bado anaendelea kupiga kelele ili aweze kusaidiwa kukabiliana  na matazizo yanayo msonga, na ili aweze kuongozwa katika njia ambayo kwa dhati ni changamoto kwake na  hatimaye aweze  kuandaa utume wake katika kutafuta maisha yake ya furaha. Hiyo ni dhahiri ya mang’amuzi ambayo Mtakatifu Paulo anawasilisha kama mojawapo ya zawadi za Roho Mtakatifu, na Mtakatifu Tomas wa Aquinas  anaita  uadilifu mkuu ambao  unahukumu kwa mujibu wa misingi mikuu na ambayo tunaweza kujibu mahitaji ya binadamu wa leo.
Roho Mtakatifu ni kiongozi wa kila aina ya mang’amuzi ya dhati, kwasababu siyo siku nyingi zilizopita , Kanisa limesali kwa ajili yenu kwake Roho wa Bwana ambaye ni msingi na nguvu ambayo Baba  alimpatia mwanae na yeye mwenyewe akawapatia mitume wake, maana yake ni Roho ambaye anasisimamia na kuongoza.

Kwa njia hiyo ni lazima kutambua zawadi hiyo  ambayo daima wote ni wahudumuwake na  daima tumepokea  juu ya mabega yetu dhaifu. Baba Mtakatifu anaongeza kusema, labda ndiyo maana Kanisa wakati wa sala ya kumweka wakfu Askofu,  waliweza kuchukua Zaburi ya huruma ambayo mzaburu anaelezea historia yake mara baada ya kushindwa kabisa kutokana na dhambi zake, anasali kwake Roho Mtakatifu amjalie wema katika utii na Mungu. Lakini huo ndiyo  msingi kwa yule anayeongoza jumuiya yoyote anasisitiza Baba Mtakatifu
Anayeweza kufundisha na kukua katika ufahamu ni yule tu anayejifunza kutoka kwa  mwalimu, ni mwalimu wa ndani kama dira. Ni yule anatoa  vigezo vya kutofautisha kwa ajili yake na wengine nyakati za Mungu na za neema yake. Anauweza kuwa kuonesha nyenzo halisi za  kumpendeza Mungu ili kukamilisha mema ambayo Yeye hutangulia katika mpango wake wa ajabu wa upendo kwa kila mmoja na kwa wote. Ni wale ambao wanaongozwa na Mungu wana cheo na mamlaka ya kupendekezwa kama viongozi wa wengine. Hekima hii  ni hekima ya msalaba pamoja na kujumuisha sababu na busara, inapita zaidi kwasababu inaongoza kwenda katika kisima cha maisha yenyewe ambayo hayafi  tena na kumjua Baba Mungu pekee wa kweli na yule aliyetumwa Yesu Kristo.

Askofu hawezi kujishughulisha kutoa hivi hivi zawadi kubwa kutoka juu kama kwamba alikuwa na haki ya kuipata, bila kuangukia katika huduma isiyo zaa matunda. Ni muhimu kuendelea kuomba kwa  jambo msingi katika kuangaza kila mtu hekima. Hekima ya kijamii , hekima ya maadili, hekima ya kisaikolojia ambayo inaweza kutumika katika kazi ya utambuzi  wa njia za Mungu kwa ajili ya wokovu wa wale ambao tumepewa.
Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko anasema, ni lazima kurudia kuomba   tukikumbuka Bwana anavyosema, ni kama watoto ambao hawajuhi kujipima, kuomba siyo siku chache za kuishi, siyo utajiri  na wala maisha ya maadui wetu , bali ni lazima kuomba hekima ya maang’amuzi ya kuhukumu kati ya watu wake. Bila neema hii, hatuwezi kuwa wataalamu wa vipima joto ambao wanaweza kuona kile kitakachoonekana katika hanga, lakini hawna uwezo kutathmini wakati wa Mungu.

Mang’mauzi kwa njia hiyo yanatoka katika moyo na akili ya Askofu kwa njia ya sala na kujikita kwa kina, aidha kuwasiliana hata ma watu ambao tumepewa kuwaongoza na kwa njia ya Neno la Mungulitokanalo  na Roho. Ni katika urafiki huo kwamba Mchungaji anakomaa kwa uhuru wa ndani na kumfanya awe imara katika uchaguzi na tabia  na mwendendo wake binafsi kama ule pia wa  Kanisa .

Katika utulivu wa maombi unaweza  kujifunza sauti ya Mungu, kutambua matukio ya lugha yake, upatikanaji wa ukweli wake, ambao ni mwanga tofauti sana. Baba mtakatifu anatoa mfano kuwa haupo  juu ya akili kama mafuta yanayoelea juu ya maji na wala zaidi lakini ni yule anaye jua ukweli wa Mwangu huu. Ni katika utulivu wa sala unaweza kujifunza sauti ya Mungu na kutamba neema ya Roho Mtakatifu katika Kanisa ambaye anasikiliza.
Baba Mtakatifu francisko amemaliza hotuba yake akiwaomba wawe karibu sana na Yesu na  kuwatunza kondoo wao waliopewa.  Wawe na nafasi ya kukutana na Mungu  na kuchagua njia zake wakiendelea mbele na upendo wake. Aidha akikumbuka sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba, anasema wadumu na kuwa na ufahamu wa Mungu kwa kutafakari kwa kina juu ya mwili  wa mwanae Yesu Kristo, zaidi katika kigezo cha kutokumsadiki kila mtu asemaye kwamba ana roho wa Mungu, bali wachunguze kwa makini kama huyo mtu anaongozwa na Roho wa Mungu au la maana manabii wengi wa uongo wamezuka ulimwenguni. (1 Yohana 4: 1) . Amemaliza hotuba yake akiwabariki na kubariki Makanisa yao wanakotokea.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya  Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.