2017-09-14 09:39:00

Padre Tom Uzhunnalil aliyetekwa nyara nchini Yemen 2016 ameachiwa huru


Mara baada ya kungia ndani na kukutana na Baba Mtakatifu, ameinama chini na kubusu miguu ya Baba  Mtakatifu Francisko lakini mara moja alisaidiwa kuamka na kumbusu mikono. Hiyo ndiyo picha halisi iliyojitokeza wakati Padre Thomas Uzhunnalil alipokutana na Baba Mtakatifu Francisko. Ni padre wa Shirika la Wasalesiani kutoka India aliyetekwa nyara na magaidi miezi kumi na nane iliyopita katika nchi ya Yemen. Baba Mtakatifu Francisko amempokea katika nyumba ya Mtakatifu Marta, asubuhi ya tarehe 13 Septemba mara baada ya kumaliza katekesi yake. Amemkubatia na kumtia moyo, na kumweleza kuwa ataendelea kumsindikiza katika sala zake hata sasa kama vile ilivyokuwa wakati wa  kipindi chote alichokuwa matekani. Kwa hakika Baba Mtakatifu alionekana wazi kuguswa sana na padre na hivyo amembariki.

Kwa upande wa Padre Thomas amemshukuru Baba Mtakatifu na kumsimulia jinsi alivyokuwa akisali sana kila siku kwa ajili yake na kutoa mateso yake kwa ajili ya wema wa utume wake na wa Kanisa pia. Ni manen ambayo yamemgusa Baba Mtakatifu kwa namna ya pekee. Padre Thomas pia amelezea  ni jinsi gani hakuweza kuadhimisha Ekaristi Takatifu, lakini kila siku alikuwa akisali moyoni na kutafakari kwa kuadhimisha misa  akirudia maneno ya Ibada kimoyomoyo. Na sasa baada ya kupata uhuru kutoka mikononi mwa magaidi hao , ameahidi kusali zaidi na zaidi kuwaombea wote waliosali kwa ajili yake katika kipindi chote alichokuwa matekwa. Aidha anawakumbuka kwa namna ya pekee watawa wanne wa Shirika la upendo walio uwawa kipindi cha utekaji nyara huko Yemen.

Gazeti la Osservatore Romano,limemkariri pia Padre Tom akitoa shukrani za dhati kwa kiongozi wa serikali ya Omani ambaye amefanya jitihada kubwa yakupata uhuru kutoka mikononi mwa magaidi hao. Kwa upande wa Vatican tayari walikuwa wamekwisha toa shukrani zao , kwa wote waliokuwa wanafanya jitihada zote za kuweza kumpata na kuwa huru,  kwa namna ya pekee Sultan wa Oman na viongozi wote wenye madaraka katika imaya yake ya kisultani. Pamoja na walio msindikiza Padre Tom kukutana na Papa alikuwa Kardinali Oswald Gracia, Askofu Mkuu wa Bombay.

Kwa mujibu wa maneno ya Askofu Mkuu  anasema, baadaya ya uzoefu huo wa kutisha, ujumbe muhimu ambao Padre Tom anautoa ni kwamba Yesu anatupenda. Akiongea kwa niaba yake anasema, ni hakika kwamba Padre Tom alijisikia kila siku uwepo  wa Yesu karibu na kwamba alijisikia kabisa ndani ya moyo wake ya kuwa yeye hayuko peke yake. Kwa sasa Padre Tom atabaki mjini Roma, katika nyumba yao ya shirikia kwa ajili ya kuangalia afya yake kabla ya kurudi nchini kwao, japokuwa anasema askofu nkuu kuwa, afya yake siyo mbaya , kwa maana ya watekaji nyara wake hawakumpa shida yoyote zaidi ya kumweka kifungoni tu.

Ikumbukwe,Padre Thomas alitekwa nyara tarehe 4 Machi 2016 huko Aden  nchini Yemen, katika shambulizi ya magaidi kwenye nyumba ya kutunza wazee wa Shirika la wamisionari wa Upendo. Padre Thomas ni mwenye umri wa miaka 5, kutoka jimbo Kuu la Kerala India. Amezaliwa katika familia Katoliki mahali ambapo alikuwa na Mjomba wake Padre naye wa Shirika la Wasalesiani ambaye alikuwa amefungua nyumba ya Shirika la kimisionari la Wasalesiani  huko Yemen. Mwaka 2015 aliaga Dunia, kwa njia hiyo, wakati wa kutekwa nyara Padre Tom alikuwa tayari ameishi miaka minne katika utume wa kimisionari huko Yemen.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.