2017-09-14 16:30:00

Msalaba bila Kristo na Kristo bila msalaba siyo fumbo la upendo


Baba Mtakatifu Francisko asubuhi ya terehe 14 Septemba , ameanza tena maadhimisho ya Misa Takatifu katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta, mjini Vatican mara baada ya kipindi cha mapumziko. Ikiwa Kanisa Katoliki linaadhimisha Sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba, Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri yake ametazama kwa namna ya pekee vishawishi viwili vya kiroho mbele ya msalaba wa Kristo.  Kishawishi cha kwanza ni kile cha kufikiria Kristo bila kuwa na msalaba maana yake, kumfanya kuwa  mwalimu tu wa kiroho  na sehemu ya pili ni ile ya kutazama msalaba bila kuwa na Kristo, kwa maana ya kutokuwa na matumaini naye .

Moyo wa Baba Mtakatifu Francisko umejikita kutafakari fumbo la upendo utokanao na msalaba. Liturujia ya siku ilikuwa inaeleza juu ya mti mzuri na mwaminifu. Na kwa njia hiyo nasema wakati mwingine  siyo rahisi kuelewa masalaba. Lakini ni wazi kwamba  tunaweza kutambua msalaba huo kwa kutafakari kwa kina na kuingia kwa kwa kina katika fumbo la upendo. Anatoa mfano wa Yesu na Nikodemu alipomwendea  kwamba, alitumia maneno mawili kufafanua yaani neno la kupanda na kushuka. Yesu alishuka kutoka mbinguni ili kuweza kutupeleka hata mbinguni. Na hilo ndilo fumbo la msalaba. Katika somo la kwanza Mtakatifu Paulo anasema, Yesu alijinyenyekeza  akawa mtii hadi mauti ya msalaba. Bba Mtakatifu anaeleza kuwa, hiyo ndiyo maana ya kushuka kwake Yesu hadi chini kwa unyenyekevu  na kutoa upendo wake wote , na ndiyo maana Mungu alimfanya apaetena  mbinguni.

Kwa Maana hiyo iwapo hata sisi tunaweza kutambua jinsi ya kushuka kwake hadi mwisho, tunaweza kutambua hata ukombozi ambao unatolewa na fumbo la upendo. Lakini hata hivyo Baba Mtakatifu anasisitiza kuwa, siyo rahisi kwasababu daima kuna vishawishi vya kufikiria nusunusu na siyo kwenda mbele zaidi ya hayo. Na ndiyo maana hata Mtakatifu Paulo anatumia neno kali kuelezea kuwa, walipoangushwa na kishawishi hawakuweza kuingia katika fumbo la upendo bali kueelezea tu. 

Na kama vile nyoka aliyekuwa amemdanganya Eva au  katika jangwa nyoka waliwatia sumu  waisraeli wakadanywa na ndivyo hivyo walindanyanywa kwa kufikiria  Kristo bila msalaba au msalaba bila Kristo.Hivyo ndiyo vishawishi viwili anavyosisitiza Baba Mtakatifu, yaani Kristo bila msalaba maana yake  kujifanya mwalimu wa kiroho na kuendelea katika safari yako kwa utulivu, kwa maana ya kusema kwamba, Kristo bila msalaba siyo Bwana; labda ni mwalimu wa kawaida hakuna cha zaidi. Na ndiyo labda alikuwa akitafuta Nikodemu. Hiyo ni mojawapo ya kishawishi; yaani Yesu mwema na mwalimu lakini asiye kuwa na msalaba.

Na kishawishi cha msalaba bila kuwa na Yesu anafafanua kuwa ni kuwa na uchungu na kubaki nao ndani yakoumeinamia tu na kuelemewa na dhambi bila ya kuwa na matumaini, ni kuwa na msalaba lakini  bila ya kuwa na  matumaini na bila kuwa na Kristo. Msalaba bila ya kuwa na Kristo ni fumbo la janga, Baba Mtakatifu anaeleza ,ni kama vile janga la kipagani, na kwa njia hiyo, msalaba ni fumbo la upendo, msalaba ni uaminifu, msalaba ni mzuri. Leo hii kila mmoja aweze kupata fursa ya kutakari angalau kwa dakika moja kujiuliza kama Kristo msulibiwa ni fumbo la upendo kwake, na je unafuata Yesu bila msalaba, mwalimu wa kiroho anayekujaza utulivu , na mashauri mema?

Je unafuata msalaba bila kuwa na Yesu , ukilalamika daima na moyo huo usio kuwa na Mungu kiroho. Je unaruhusu kupelekwa na fumbo hili kwa kujinyenyekeza hadi chini ,kama Yesu mwenyewe?. Amemalizia Baba Mtakatifu akiwatakia wote kwamba, Bwana aweze kutoa neema ya kutambua na kuingia kwa undani katika fumbo hili la upendo , kwa njia hiyo katika moyo , akili na mwili wote unaweza kutambua chochote.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.