Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Katekesi siku ya Jumatano

Papa: Maisha ya Utakatifu na kila mateso yanapitia katika Msalaba

Kuadhimisha Sikukuu ya Kutukuka kwa Msambala unakumbusha kuwa ni kwa njia ya msalaba wa Yesu Kristo, ubaya wa shetani umeshindwa pamoja na mauti - RV

13/09/2017 16:20

Mara baada ya Katekesi yake amewasalimia waamini wote na makundi kutoka sehemu mbalimbali za dunia, ambapo amewakumbusha kwamba tarehe 14 Septemba Kanisa Katoliki linaadhimisha Sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba:Baba Mtakatifu anasema, kumbekeni daima kwamba, ni kwa njia ya msalaba wa Yesu Kristo ubaya wa shetani umeshindwa pia  na kushindwa mauti.Kwa njia hiyo tumepata maisha na kurudishiwa matumanini. Tambueni daima kugundua na kupokea ujumbe huo wa upendo na wokovu wa Msalaba wa Yesu.

Halikadhalika amesisitiza kuwa sikukuu hiyo inatukumbusha kuwa maisha ya utakatifu yanapitia katika Msalaba. Kwa mtazamo huo tunapaswa kuangalia kila mateso kama vile ya : ugonjwa, udhalimu, ukosefu wa haki, umasikini na kushindwa. Msalaba umekuwa sala yake  Yesu Kristo na hivyo Baba Mtakatifu anasema, uwe kwetu chemi chem ya utakaso wa maisha na nguvu katika roho. Kuubeba Msalaba wetu kila siku na shida tunajifunza kutoka kwakwe ule uwezo wa kuelewa na kukubali mapenzi ya Mungu.

Mwisho amewageukia  vijana , wagonjwa na wanandoa wapya kwamba: vijana waimarishe mazungumzo yao na Mungu katika kueneza mwanga wake na amani yake. Kwa wangonjwa; wajaribu kupata nguvu kupitia  msalaba wa Yesu Kristo  ambaye anaendelea na kazi yake ya ukombozi katika maisha ya kila mtu. Na kwa wana ndoa wapya;  wajitahidi kudumisha uhusiano  wa mara kwa mara pamoja na Kristo aliye wambwa Msalabani ili upendo wao  uweze kuwa  wa kweli daima na uweze kuzaa matunda ya kudumu.

Halikadhalika Baba Mtakatifu Francisko ameonesha masikitiko yake na uwepo wake kiroho kwa watu wengi wanao teseka kutokana  mafuriko yaliyo tokea huko Livorno nchini Italia siku ya Jumapili 10 Septemba 2017 . Anawaalika watu wote kusali kwa ajili kuwaombea   walio fariki dunia kutokana na maafa hayo , majeruhi na familia ambazo zimekumbwa na janga hilo.
Kuhusiana na mafuriko hayo huko Livorno mchana wa tarehe 13 septemba 2017, itafanyika mazishi ya watu saba walioathiriwa na mafuriko hayo. Mazishi hayo yatafanyika katika makanisa tofauti kulingana na maombi ya wanafamilia wao. Hadi sasa katika mji wa Livorno operesheni za kuokoa  zinaelendelea, watu wa kujitolea na vikundi maalumu kama zima moto na wengine.


Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

13/09/2017 16:20