2017-09-13 16:53:00

Biashara haramu ya binadamu inaongezeka kwasababu ya kutojali


Vatican inashutumu kabisa juu ya aina mpya za utumwa kwa maana ni kidonda katika mwili wa binadamu wa kisasa, kama alivyoeleza Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba ya tarehe 10 Apili 2014 kwa washiriki wa  Mkutano wa Kimataifa kuhusu Biashara ya Binadamu. Kila mtu lazima awe  na ufahamu wa hali hizi za kutisha  na kufanya jitihada za  kuondoa aina mpya na mbaya ya utumwa wa kibinadamu.

Ni maelezo ya Askofu Mkuu  Ivan Jurkovič  Mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa huko Geneva Uswis, katika kikao cha 36 Cha  Baraza la Haki za Binadamu tarehe 12 Septemba 2016. Ni kikao ambacho kinazingatia sababu na matokeo ya uhalifu mkubwa sana. Askofu Mkuu Ivan anakumbusha kwamba Biashara ya binadamu  inayofanyika kuwanyonya watu katika maeneo kama vile ya ukahaba, kazi za kulazimishwa,  hutoa faida kubwa sana kwa wahalifu.

Katika makadirio ya mapato ya kila mwaka anasema, ni zaidi ya bilioni 150  dola za kimarekani na  zaidi pia zile zinazotokana na biashara ya madawa ya kulevya. Na miongoni mwa wahamiaji kwa ngazi ya dunia yote wengi ni wale walioathirika na biashara hiyo. Sababu anasema, mara nyingi umaskini na ukosefu wa kazi ndiyo imekuwa hoja kubwa ya kuwafanya watu wawe kwenye mtego wa biashara hizo. Pamoja na migogoro ya kibinadamu inayoenea, ikiwa ni pamoja ile inayosababishwa na migogoro ya silaha na maafa ya asili, inaongezwa na  na biashara ya binadamu ambayo huchochea aina mpya za bashara hizi.

Askofu Mkuu anakumbusha ujumbe wa Baba Mtakafu Francisko kuhusu hati ya “Sifa kwa Bwana” ambayo maelezo yake ni mengi yanahusu aina mpya za utumwa: yote hayo ni matokeo ya utamaduni wa mahusiano ambayo yanatoa msukumo wa mtu mmoja kutaka kujinufaisha kwa njia ya mtu mwingine na kumfanya kama kitu au kumliki , kulazimisha afanye kazi za kushurutishwa au kumfanya mtumwa wake kutokana na madeni na kwa mantiki hii ni sawasawa na inayoongoza kwenye unyanyasaji wa kijinsia wa watoto.

Askofu Mkuu Jurkovič  kwa njia hiyo anakumbusha pia kipengele cha ujumbe wa Baba Mtakatifu  kwa siku ya 48 ya amani ya Dunia ya tarehe 1 Januari 2015. “Mara nyingi ukitazama matukio ya biashara ya binadamum uhamiaji haramu na aina nyingine zinazojulikana na ambazo hazijulikani za utumwa, inaonekana kwamba jambo hilo linafanyika katika maeneo ya kutokujali kwa ujumla”. Kwa njia hiyo  ili kuondokana na utumwa na utofauti huo  kwa ujumla, inahitaji nguvu ya pamoja ya uhamasishaji zaidi , ushiriki na ushirikiano katika ngazi za kitaifa na kimataufa, aidha Askofu Mkuu anasisitiza na kila mtu binafsi anaitwa kushiriki kikamilifu .

Ni wakati sasa  wa  kuondoka kutoka katika sheria kufikia vitendo halisi. Utawandawazi wa kutokujali kama Baba Mtakatifu Francisko anavyandika katika Ujumbe wa Siku ya 48 ya Amani dunia, unatoa wito kwa wote kuwa mawakala  wa utawandawazi wa umoja na undugu , ambao unaweza kuwapa tumaini na kujikita kwa upya kuwa na ujasiri wa kutembea  katika shida mbalimbali za nyakati zetu  aidha kuwa na upeo mpya wa hali tulizo nazo.  Askofu Mkuu Ivan anahitimisha akisema; aina mpya za unyonyaji lazima ziondolewa kama vile  utumwa ulovyofutwa zamani. Na hili ni lengo ambalo linaweza kupata ufumbuzi  kwa kupitisha maono mapya ya mwandamu na heshima yake kwa njia ya sheria, elimu na uongofu wa kweli katika  roho za wengi.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.