2017-09-12 16:02:00

Mkutano wa 21 wa Baraza la Makardinali Washauri wa Papa unafanyika


Tarehe 11 hadi 13 Mjini Vatican umefunguliwa Mkutano wa 21 wa Baraza makardinali Washauri  Vatican . Ni kiungo cha makardinali 9  kilichoanzishwa na Baba Mtakatifu Francisko terehe 28 Septemba 2013, kwa lengo la kumsaidia Baba Mtakatifu katika Utawala wa  Kanisa zima la Ulimwengu na kufanya marekebisho ya rasmi ya Katiba ya Kitume Vatican. Kulingana na shuguli za kiungo hicho na kwa jinsi  gani Baba Mtakatifu anashiriki katika mchakato wa mageuzi,mwandishi wa habari wa radio Vatican amemhoji Katibu Mkuu wa Baraza la Makardinali washauri wa papa, Askofu Marcello Semeraro .

Anaeleza kuwa kwa upande wa Baba Mtakatifu hajisikii kuwa mwenye mageuzi, kwasbabu kama marekebisho yametokana na msukumu wa mapendekezo yalitokea kabla ya mkutano wa uchaguzi wa Papa. Na ndiyo maana kati ya wale aliyo wapendekeza mwanzoni ni kati ya makardinali ambao ni maaskofu wakuu wa majimbo yaliyogawanyika kutoka pande zote za dunia. Katika kueleza jinsi ya kufanya kazi katika baraza la makardinali washauri wa papa anasema,  ni kufanya kazi kwa kupitia hawali ya yote katika vilelezo viwili ya kwanza ni Baraza la Makardinali walisikilizia na wanasikiliza. Na hiyo ni kwasababu kila kitu kilianza mwaka 2013 kwa kutoa ripoti ya michango mbalimbali iliyotoka katika mabaraza ya maaskofu wote, mabaraza ya kipapa na hata kwa watu wengine ambao waliandika na kutoa machango wao.

Kielelezo cha pili anasema, baraza linasikiliza na kutafakari. Kutafakari maana yake ni kuonesha juu ya mapendekezo na jinsi gani ya kuendelea, hata kufanya tathimini. Baada ya kusikiliza , kutafakari na kutathimini, wanafanya mapendekezo, na mapendekezo hayo yanawekwa mbele ya Baba Mtakatifu kwasababu Baraza la Makardinali halitoi uamuzi, shughuli yao ni kutoa mapendekezo kwake Baba Mtakatifu aliye na uamuzi wa mwisho.
Kwa njia hiyo Baraza la Makardinali la  ushauri ni kiungo muhimu kwake Baba Mtakatifu kwani aliwachagua wajumbe hawa wa Baraza la Maaskofu  ili waweze kwa namna moja au nyingine antena za kuwasilisha  habari  za Kanisa mahalia katika ulimwengu kwa mapana zaidi. Kwa maana hiyo Baraza la Makardinali, muundo wake ni wa kisinodi kwasababu umeundwa bado na maaskofu, pia ni muundo unaofanya kazi ndani ya Baraza la maaskofu . Kadhalika ni utume ambao siyo tu kwa ajili ya kumsaidia Baba Mtakatifu tu bali ni utume hata wa huduma ya Kanisa mahalia.

Akielezea jinsi gani baba anashiriki naye mkutano huo, Askofu Semeraro anasema, kwa kawaida Baba Mtakatifu huwa anasikiliza, anaweza kuingilia kati iwapo anataka kutoa uzoefu binafsi wa wakati ule bado anafanya utume wake huko Buones Aires, au katika hali ya sasa ya maisha ya Kanisa. Zaidi ya hayo Baraza la makardinali halikuundwa tu kwa ajili ya mageuzi ya Vatican, lengo kuu msingi baadaya kumaliza mchakato huu wa mageuzi Vatican , inatabaki kazi kuu kwa  Baraza lililoanzishwa yaani kushirikiana na kutoa maoni ya baraza, pia mapendekezo kwa Baba Mtakatifu katika hali ambazo zitaoneaka ni muhimu kufanya ushauri huo.

Anatoa ushuhuda kuwamba baada ya mikutano mingi katika Baraza hili la Makardinali washauri kumejengeka hali ya familia. Na kwa upande wake kama Katibu Mkuu wa Baraza, shughuli yake ni kuhakikisha mambo yanakwenda barabara kwa kuzingatiza mawasiliano kati yao na katika makutano wakati wa mapumziko ya chai. Makardinali wana fanya matani machache, vichekesho katika habari fulani , lakini kila kitu katika hali ya kifamilia na utulivu na ndiyo maana ya kufanya kikundi cha watu, wajibu wao,lakini pia katika mantiki ya kifamilia.

Na juu ya mchakato wa magezui umefikia wapi anasema, sasa ni kama vile zaidi ya robo tatu ya mchakato ni karibu kukamilika lakini  hata hivyo mapendeke mengine Baba Mtakatifu ameisha yatoa kwa mfano hivi karibuni alitangaza hata kuunganisha baadhi ya Baraza la kipapa ya Baraza la walei, familia na maisha kuwa kitu kimoja;  Baraza la kipapa la kuhakamisha maendeleo ya binadamu ambayo inatokana na mpango wa hati ya Gaudium et Spes. Kadhalika kuundwa kwa Baraza jipya la Sekretarieti ya Mawasiliano Vatican ambayo inajihusisha sana na  kazi ya kutoa kipaumbele cha kichungaji, ambayo mwanzo ilikuwa chini ya  Baraza la Kipapa la  Mawasiliano ya kijamii. Lakini pamoja na mwongozo wa kazi ya kichugaji , Sekretarieti ya Mawasiliano  ina jukumu kubwa  katika utawala kwa upanda wake lakini pia kwasababu ya umuhimu wa mada ya masiliano Baraza hili ni kiini cha mpango wa mageuzi ya Vatican.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.