"Natoa salam kwenu wote maprofesa na vijana ambao kwa furaha kubwa Sekretarieti Kuu ya Sinodi ya Maaskofu inawakaribisheni katika mwanzo wa Semina ya Kimtaifa ya mafunzo kuhusu hali halisi ya Vijana, iliyoandaliwa kwa malengo ya maandalizi ya Sinodi ya XV ya Kawaida ya Maaskofu itakayo kauli mbiu “Vijana, Imani na maang’amuzi ya miito”. Ni maneno ya Kardinali Lorenzo Baldisseri, Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu aliyoanza nayo wakati wa ufunguzi wa Semina ya Kimataifa kwa maprofesa na wawakilishi wa Vijana kutok Mabara matano, kwa lengo la maandalizi ya Sinodi kuhusu vijana 2018 na semina hiyo imaeanza tarehe 11 hadi 15 Septemba mjini Vatican.
Kardinali Baldisseri anasema, ni zaidi ya miaka hamsini ya shughuli hizi ambapo
Sinodi imeundwa kwa mantiki ya aina yake ambayo ina utajiri mkubwa kutokana na mafundisho
ya Mtaguso wa II wa Vatican na kwa namna ya pekee umekuwa kiungo na kuimarisha zaidi
sura ya Kanisa leo hii. Sinodi ya Maaskofu mwaka 2018 haiwakilishi jambo la kushangaza
zaidi ya kuwakilisha ujumbe wa mwisho wa Mtaguso wa binadamu ambao uliwalenga vijana,
maana mababa wa mtaguso walikuwa na lengo na mawazo ya kuwakabidhi Vijana usukani
wa Kanisa la baadaye.
Ujumbe wa mababa ulikuwa unasema:”Ni nyinyi vijana wa dunia nzima ambao mtaguso unawalekeza
ujumbe wake wa mwisho. Ni nyinyi ambao mnaupokea mwenge huo katika mikono yenu kutoka
kwa mababa ili uwezea kuangaza dunia katika kipindi cha mabadiliko ya kihistoria.
Ni nyinyi ambao mnapokea vema mifano na mafundisho ya wazazi wenu, walimu wenu na
kuunda jamii endelevu: Kwa maana ni nyinyi mtakao okoa au kupotea ndani yake”.
Kwa miaka minne Kanisa linafanya kazi kwa ajili ya kudumisha na kukuza uso wake uwe bora kulingana na ishara za mwazilishi wake, yaani yule anaiyeishi ambaye ni Kristo daima kijana. Na baada ya kutazama kwa upya maisha yake, mababa wanawageukia kwamba ni nyiny vijana hasa katika mtaguso wake ulitoa mwanga na kuangaza wakati ujao na wakati wenu endelevu. Kanisa ambalo linalotamani kuona jamii inayo wazunguka kuijenga na kuheshimu hadhi yake, uhuru wake , haki za watu ambao ni nyini wenyewe. Kardinali Baldisseri anasema, maneno ya mababa wa mtaguso yote yanabaki hata leo ya kufaa kwasababu bado ni bahati na fursa ya njia ya Kanisa na zaidi katika muhongo wa mabadiliko tunayoishi kwa wakati huu. Kwa njia hiyo mwaka kesho mababa wa Sinodi wataunganika Roma na Petro chini ya Petro , kutafakari pamoja juu ya suala la utume wa kichungaji kwa kizazi kipya, kwa kutambua vema na akili yake ya ufunguo wa somo uliotolewa na Baba Mtakatafu Francisko, akiwataka mababa wa sinodi wajikite zaidi kwa namna ya pekee katika imani na maang’amuzi ya vijana.
Kwa upande wa mantiki ya Semina, inawapa fursa ya kuchangia na kuwaruhusu watazame
vema na kupiga picha ya hali halisi ya vijana katika kugundua na kutambua sifa msingi
zinazowashirikishwa na vijanale wakati huo huo kwa kuzingatia wingi wa mazingira ya
kijiografia na utamaduni,na idadi kubwa ambayo uwafanya dhana ya vijana .Mwisho wa
seminari hiyo ambao siyo tu kwa lengo la mkutano wa wa kimataifa, bali hata ni fursa
ya nafasi nyingi iwezekanavyo ya kufanya mahusiano kati ya wataalamu kutoka katika
mabara yote, lakini pia ni kuhamasisha na kukuza mazungumzo na viongozi katika taaluma
mbalimbali ya elimu jamii, saikolojia , uchumi, komputa , falsafa na taalimungu ya
huduma ya kichungaji.
Zaidi ya wataalamu waliopo, hawakosekani wawakilishi wa vijana wenye ujuzi , waliotambuliwa
kwa ushirikiano wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Walei, familia na maisha. Hawa ni
wajumbe wa huduma ya kichungaji kwa vijana katoka katoka mataifa mbalimbali na makanisa
mahalia , aidha Shirikikisho la wanachama Vijana na Wawakilishi vyama vya kitume
vya Wanafunzi.
Katika mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko kwenye maandalizi ya Siku ya vijana duniani mwaka huu kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu alisema: Katika sinodi ijayo kuwa hakuna kijana yoyote ambaye ajisikie kubaguliwa , na wakati huo sinodi ya vijana siyo kwa ajili ya wakatoliki tu, bali ni sinodi ya vijana wote ambao ndiyo wako mstari wa mbele. Kwa njia hiyo sinodi ni kwa ajili ya vijana wote, wavivu , wasio kuwa na imani walio na imani, walio mbali na Kanisa , wasio mjua Mungu, wote ni lazima kusikilizwa, kwa maana kila kijana analo jambo la kusema kwa wengine wakubwa kwa wadogo, mapadre , watawa na maaskofu na papa mwenyewe.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |