Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Vatican \ Hotuba

Ziara ya Ask. Mkuu Paul R. Gallagher katika nchi ya Iran 5-9 Sept

Asubuhi ya tarehe 6 Askofu Mkuu Gallager na wengine walikutana na Waziri wa Biashara ya nchi za nje Zarif na baadaye kupata chakula cha mchana na waziri, - RV

11/09/2017 15:26

Chini ya mwaliko wa waziri wa Biashara ya nchi za nje wa  Jumhuri ya Kiislam nchini Iran Mohammad  Javad Zarif, Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican, alianza ziara katika nchi hiyo  kuanzia tarehe 5-9 Septemba. Askofu Mkuu Gallagher aliwasiri mjini Teharan Jumanne 5 Septemba akisindikizwa na Monsinyo Ionut Paul Strejac , mshauri wa Ubalozi katika kitengo cha Mahusiano ya nchi za nje. Alipokolewa katika kiwanja cha ndege cha  Iman Khoimeini na  Askofu Mkuu  Leo Boccardi na viongozi mbalimbali kwa mujibu wa Protokoli ya Wizara ya biashara ya nchi za nje.

Asubuhi ya tarehe 6 Askofu Mkuu Gallager na wengine walikutana na Waziri  wa Biashara ya nchi za nje Zarif na baadaye kupata chakula cha mchana na waziri, kilichoandaliwa kwa heshima yake. Mchana Askofu Mkuu alitembelea Wizara ya Utamaduni na mwongozo wa Kiislam, mahali ambapo walikutana na waziri Abbas Saleh wa wizara hiyo.  Katika salam na mazungumzo kati ya Askofu Mkuu Gallagher na waziri huyo yamegusia  mada ya mahusiano ya  siasa za kimataifa , migogoro inayoikumba nchi za Mashariki na hali halisi ya wakristo wa kanda hizo kwa namna ya pekee matatizo ambayo jumuiya ya wakristo wanakabiliana katika nchi. Hawakukosa kuzingatia hata umuhimu wa kukazia mazungumzo ya kidini ambayo Vatican na Iran imekuwa nayo wa muda mrefu. Kwa njia hiyo siku ya kwanza ilijikita katika mikutano ya kisiasa na kumalizika na chakula cha usiku kwenye Ubalozi wa kitume wakiwa na viongozi wa kidiplomasia . 

Tarehe 7 Septemba Askofu Mkuu Gallagher alifanya ziara fupi ya kwenda Qom katika Madhabahu ya Fatima Masuma, mahali ambapo alipokelewa nakiongozi Boroujerdi na  ambaye amesema  maneno ya sifa akimshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa jitihada zake  hasa  msisititizo na wito juu ya mazungumzo  ya kidini na utetezi wa wanyonge. Huko Ispahan katika jengo lautawalwa wa Srikali Askofu Mkuu alikutana na wajumbe wawakilishi wa kiislam kutoka katika wilaya mbalimbali. Baada ya mkutano huo  alikwenda kutembelea Jumuiya wa watawa wa Shirika la Upendo la Mtakatifu Vincenzo wa  Pauli , mahali ambapo aliadhimisha Misa Takatifu iliyoudhuliwa  na baadhi ya waamini wa eneo hilo.

Tarehe 8 Septemba Askofu Mkuu Gallagher alitembelea  Kituo cha wazee , mahali ambapo watawa wa upendo wanatoa huduma. Asubuhi hiyo pia alipata fursa ya kukutana na kuzungumza wajumbe wa Baraza la Maaskofu Katoliki Jamhuri ya watu wa Iran ambapo walizungumzia juu ya hali ya Kanisa mahalia, shughuli za kichungaji na changamoto wanazokumbana nazo katika nchi leo hii. Siku yake ya katibu Mkuu wa mahusiano ya nchi za nje  ilifungwa na misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Ispanah wakiwapo hata waamini wengine wa mji huo. Katika misa hiyo kulikuwapo hata wawakilishi wa jumuiya nyingine za kikristo.

Idadi kubwa ya watu wa Kanisa hili ni katika Armania na na kilatini kwa njia hiyo misa iliongozwa na nyimbo na masomo katika lugha tofauti. Katika mahubiri yake Askofu Mkuu Ghallager alisistiza juu ya umoja na ushuhuda katika maisha ya wakristo. Ameyasema hayo akikumbuka sura na mfano wa kuigwa wa sadaka ya kujitoa kwa mfia dini wa Ispanah Askofu Mkuu Gaicomo Emilio Sontag anayekaribia kufikisha miaka mia moja tangu kifo chake. Bada ya misa alipata fursa ya kukaa na jumuiya ya Isapanah kidogo katika ukumbi wa Kanisa Kuu ambapo aliweza kuwasalimia na kuwapa salam kutoka kwa Baba Mtakatifu anaye watia moyo na kukukata temaa. Askofu MKuu P. Ghalager alianza safari ya kurudi Vatican Jumamosi asubuhi ya tarehe 9 Septemba 2017.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

11/09/2017 15:26