Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa \ Kanisa Ulimwenguni

Marekani: Siku ya sala ya amani Kitaifa katika kupambana na ubaguzi

Siku ya maombi ya kitaifa kwa ajili ya amani Marekani ina lengo la kupambana na dhambi kubwa ya ubaguzi wa rangi katika jumuiya za Marekani.

09/09/2017 10:06

Tarehe 9 Septemba nchini Marekani ni siku ya Maombi ya kitaifa kwa ajili ya Amani katika jumuiya. Ni siku  iliyo andaliwa na Kanisa Katoliki la Marekani kutokana na tukio la kumkumbuka  Mtakatifu Peter Clever Padre wa Shirika la Yesu ambaye alitoa huduma yake kati ya watu watumwa wa nchi za Amerika ya Kusini. Shirika la Habari la Oservatore Romano linaeleza kuwa, lengo kubwa la kuanzisha maombi hayo ni kutokana na kutaka kupambana na dhambi kubwa ya ubaguzi wa rangi katika jumuiya za Marekani. Siku ya maombi  ya kitaifa kwa ajili a amani ilianzishwa mwaka jana na aliyekuwa  rais wa Baraza la Maaskofu wa Marekani wakati huo Askofu Mkuu Joseph Edward  Kurtz wakati wa maandano makubwa yaliyotokea ya kupinga marudio ya vifo vya waafro vilivyosababishwa na polisi. 

Kwa mujibu wa Askofu wa Jimbo la Youngstown Gorge V. Murry, ambaye sasa ni Mwenyekiti  wa Kamati mpya ya kupinga ubaguzi wa rangi, iliyo undwa mwezi agosti mwaka jana mara  baada ya mapambano na vurugu za Chalottesville, anasema, siku ya maombi itakuwa inafanyika kila mwaka tarehe 9 septemba sambamba na  tukio la maadhimisho ya Mtakatifu Petro Claver. Ni Mtakatifu Mjesuiti kutoka huispania aliye jitoa maisha yake ya hutumea kuhudumia watu waliokuwa watumwa na kupambana bila kuchoka katika hatua za mchakato wa kukomesha utumwa na  biashara ya binadamu ambayo ni aibu kubwa.

Askofu Murry anasisitiza kuwa, kwa upande wao Mtakatifu Peter Claver ni mfano wa kuigwa hata leo hii na kuwa na  utambauzi wa kazi ngumu aliyoifanya bila kuchoka,vilevile kuona ulazima wa kupambana na dhambi hiyo ya ubaguzi wa rangi katika ujenzi wa jumuiya yenye amani na huru. Kwa njia hiyo anamalizia akiomba watu wote kujiunga katika maombi ya pamoja ili kuweza kutekeleza kwa dhati  mapambano ya ubaguzi huo. 
Kwa maelezo zaidi bonyeza: www.usccb.org .

Wakati Kanisa Katoliki lijishughulisha na juhudi za mapambano ya ubaguzi wa rangi, nchini Marekani yameonekana maandamo ya kupinga hatua ya rais Trump kufuta kinga ya wahamiaji.Taarifa kutoka vyombo vya habari vinaripoti kuwa wanasiasa nchini Marekani wamemjia juu rais Donald Trump baada ya kutangaza kufuta msamaha wa kinga iliyokuwa imetolewa na mtangulizi wake Barack Obama kwa raia zaidi ya laki 8 walioingia nchini humo wakiwa na umri wa chini ya miaka 16.

Wafanyabiashara, mashirikisho ya wafanyakazi, viongozi wa dini, wanasiasa wa upinzani kutoka chama cha Democrats na wengi kutoka chama cha rais Trump cha Republican wameungana kukosoa uamuzi wake. Raia hao ambao wengi ni wa latino wana umri wa miaka 20 hivi sasa watakuwa na muda wa miezi sita hadi 24 kabla ya kutambuliwa kama raia wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria na huenda wakarudishwa kwa nguvu nchini mwao.
Vijana wengi ambao waliingia Marekani wakiwa watoto wanasema wanashangazwa na uamuzi huu wa rais Trump waliosema ni kinyume na utu na kuapa kutoondoka nchini humo bila kupigania haki. Baadae rais Trump alijitokeza na kudai kuwa ana upendo kwa raia hao na kulitaka bunge la Congress kupitisha sheria kadhaa za mabadiliko kuhusu wahamiaji jambo ambalo watunga sheria hao wameshindwa kufanyia marekebisho sheria hiyo kwa miongo kadhaa.

Rais Trump ameandika kwenye mtandao wao wa Twitter kuwa analenga kufanya kazi kwa pamoja na wanasiasa wa pande zote mbili ili kuleta sheria ambazo zitawalinda kwanza raia wa Marekani kabla ya wageni. Trump kwenye amri yake amesema kuwa msamaha huo uliotolewa na rais Barack Obama mwaka 2012 ulikuwa kinyume cha katiba na ulivuka mipaka ya madaraka ya rais. Na kwa upande wake rais Barack Obama hakupendezwa na uamuzi huo na anaupinga na utawala wake kwa kutengua amri aliyokuwa ametangaza ya kuwalinda vijana walioingia nchini humo wakiwa watoto bila kuwa na nyaraka.


 Msamaha huo uliokuwa unafahamika kama Daca umetenguliwa mapema wiki hii na rais Trump katika uamuzi ambao huenda ukaathiri zaidi ya watu lakini nao ambao waliweza kupata msamaha huo. Akitoa wito kwa wabunge wa Congress rais Obama amesema uamuzi wa rais Trump “hauna utu na “hauko sahihi”, huku akiwataka wabunge hao kutupilia mbali muswada huo pindi utakapowasilishwa bungeni.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

09/09/2017 10:06