2017-09-09 16:02:00

Marehemu Kard. Caffarra alikuwa na ibada Kuu ya Ekaristi


Tarehe 9 Septemba asubuhi saa tano, imefanyika misa ya mazishi ya Kardinali Carlo Caffarra iliyoongozwa na Askofu Mkuu Matteo Zuppi katika Kanisa Kuu la Bologna nchini Italia. Katika mahubiri yake amaenza na shukrani kwa dada zake, binamu zake na watawa wa kike walio msindikiza katika siku zake za mwisho hadi kufika siku ya kuitwa Bwana aidha wawakilishi wa Chuo cha Yohane Paulo II cha mafunzo ya ndoa na familia na pamoja na wawakilishi wote wa majimbo ambayo marehemu Caffarra alihudumia.

Akiongozwa na neno la  Mungu linaoelezea  karamu ya mwisho, mahali ambapo Yesu aliwambia wanafunzi wake kuwa ametamani kula nao Pasaka hiyo, Askofu Mkuu Zuppi amesema, Bwana anafanya kugundua utashi wake na ambao unajibu utashi wetu wa  kweli ulio andikwa ndani yetu na ambao daima unaukamilisho, na mapenzi hayo wakati huo yanatoa  maana ya siku zetu za baadaye kwa maana ya upendo usio kuwa na mwisho. Neno lilifanyika mwili ili kwamba, binadamu wote katika dunia hii wapate kufunguliwa njia ya mbinguni, kama anavyo andika Mt. Agostino kuwa, hatima yetu ni Yeye, maana yeye atakuwa shuhuku zetu, tutamtafakari bila kikomo, tutampenda  bila kusumbuliwa na kumsifu bila kuchoka.

Askofu Mkuu Zuppi amekumbuka maneno ya Kardinali Caffarra wakati wa sala yake ya mwisho anaaga kumaliza muda wake wa utume kama askofu kwamba alisali: Niongoze siku hizi zinazobaki ili siku yangu ya kufa niweze kuona  uso wa furaha wa mwana wako, ambaye daima nimemtamani na daima nimempenda. Kwa njia hiyo Kardinali Zuppi anasema leo  hii Kardinali Carlo Caffarra anaona uso wake wa furaha, mfufuka, mwanga kamili alio utamani. Lakini pia  hakosi  kuonesha masikitiko ya kumuaga, kutokana na pengo kubwa analoliach maana anasema,  ameacha mambo mengi nyuma yanaendelea wakati wao wakiwa katika kongamano la ekaristi na kwamba uwepo wake katika Kanisa lote ulikuwa bado unahitajika.

Katika kuadhimisha Ekaristi, yeye alitambua vema ukuu na kiini cha Ekaristi maana alikuwa anasema,  Ekaristi ni kilelezo cha utangulizi wa ufufuko ambapo wote tunatazamia. Na  tunda la Ekaristi ni muungano wa ndugu. Askofu Mkuu anasema urithi huo anauacha kwa watu wote maana yeye wakati wa kuadhimisha misa alikuwa na upendo mkuu na ibada ya kina. Kardinali Caffarra alipenda na kuhudumia binadamu wa Kanisa kwa akili yake wakati huo huo hata umakini na uwepo karibu kwa kila mtu na  alionesha furaha, wakati mwingine matani lakini yenye kujenga.

Wote wanatambua hili  anaendelea, alivyokuwa na roho ya kibinadamu, mpendwa na mkweli kama pia Baba Mtakatifu alivyo mwelezea.  Hakupenda hata kidogo mambo ya kuchanganya au mambo mengine yasiyo eleweka au yale ya kudhoofisha ubinadamu. Alikuwa mkweli na mwenye  upendo wake uliomfanya kutii daima kwa ajili ya Yesu na kwa ajili ya Kanisa. Alikuwa amejifunza  kumjua Yesi na kumpenda, akiongozwa na imani yake  ya nguvu aliyoirithi kutoka kwa wazazi wake na familia ambao walikuwa na uhusiano mkubwa wa kina.

Baada ya kuelezea kwa kirefu historia ya maisha yake, Askofu Mkuu Matteo Zuppi anamalizia akisema, kifo chake ni mwaliko kwetu wote  kwa mara nyingine tena kuona ni wapi hata sisi hatujaweza kupanda mbegu ili kuweza kuchagua kwa haraka mbegu ya kupanda sana  kwa kutambua kuwa matunda hayo yatakusanywa na wengine kwa wakati wake.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.