Hotuba ya Askofu Mkuu Bernardito Auza Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa New York kwenye Kikao kuhusu Utamaduni wa Amani tarehe 7 Septemba 2017. Askofu Mkuu ameanza na shukrani kwa kupata fursa hiyo ili kubadilishana mawazo juu ya kukuza Utamaduni wa Amani hasa kuhusiana na maendeleo ya watoto. Askofu Mkuu Auza anasema kuhusu mada ya watoto na utamaduni wa Amani, kwa upande wa Vatican wanaona kwamba bado haijaweza kufikia wakati mzuri , kwa sababu hivi Karibuni Kanisa Katoliki limeadhimisha miaka mia moja ya kutokea Mama Maria wa Fatima huko Ureno.
Sauti kuu kuhusu umwagaji damu wa Vita ya kwanza ya dunia, ujumbe wa Fatima ulikuwa
unaelezea juu ya Amani na ulikabidhiwa kwa watoto watatu ambao walikuwa na umri wa
miaka saba,tisa na kumi.Ujumbe huu wa Amani ni muhimu hata leo hii kama vile miaka
mia moja iliyopita. Vinasikika hata leo vilio katika dunia nzima mahali ambapo zinasikika
sauti za vita vya dunia kupigania Amani. Ni kama Baba Mtakatifu Francisko alivyosema
kuwa mahali ambapo kuna migogoro ya vurugu, vitendo vya ugaidi, ikiukwaji wa haki
za msingi wa binadamu,na umaskini unaokithiri hunakwamisha juhudi za Amani.
Kukuza utamaduni wa amani kati ya watoto ni jambo muhimu kwa ajili ya Amani endelevu.
Umuhimu wa kuhamasisha thamani hii kwa watoto ni kuwaelimisha katika utamaduni wa
kukutana na ambao unahusisha hali halisi ya heshima , kisikiliza kwa makini na ushirikiano
bila haja ya kuvuruga au kupunguza utambulisho na hadhi ya mtu. Utamaduni huo utawawezesha
watoto kijibu kikamilishi na kwa ufanisi katika kukabiliana na aina nyingi za vurugu,
umaskini, unyonyaji, ubaguzi na aina aina nyingine zinazokumbwa mwanadamu.
Askofu Mkuu Auza anabainisha, kwa njia hiyo Taasisi za elimu lazima kuwapa watoto
mafunzo ya maana ya sarufi ya majadiliano ambayo kama Baba Mtakatifu Francisko anavyothibitisha
hivi karibuni kuwa ni msingi wa kukutana na kuwapa maana ya njia ya kuunganisha
tamaduni na tofauti wa kidini. Kuimarisha vijana na watoto katika masomo ya sarufi
hii ya kiakili katika mazungumzo na kwa lengo la kugundua ukweli pamoja , utawaacha
wakiwa na sababu ya kusisistiza kujenga madaraja na kupata ufumbuzi wa kutafuta Amani
dhidi ya aina mbalimbali zinazoleta vurugu za wakati wetu.
Askofu Mkuu auza anasema Vatican inaamini kuwa hali ya kwanza katika kukuza utamaduni
wa amani ni ulinzi na kukuza maono kamili ya mtu na utu wa kibinadamu. Kupunguza maono
ya binadamu hufungua njia ya kuenea kwa udhalimu, ukosefu wa haki , ukosefu wa usawa
kijamii na rushwa. Utamaduni wa amani inamaanisha kupambana na udhalimu na kuong’oa
mizizi yake nje, Kufundisha njia isiyo ya ukatili kwasababu ukosefu wa maelewano na
ugomvi unasababisha vita. Amani inahusisha kukataa vurugu katika kuthibitisha haki
za mtu. Kukabiliana na vurugu kwa kutumia vurugu kunaongeza Vifo na uharibifu zaidi.
Katika suala hili, kuimarisha utamaduni wa amani unajumuisha jitihada za kudumu
dhidi ya silaha na kupunguzwa kwa kutegemea silaha katika uendeshaji wa masuala ya
kimataifa. Kila juhudi katika mwelekeo huu, hata hivyo ukiwa ni wa kawaidia husaidia
kujenga utamaduni wa amani.
Vatican inaendelea kutoa wito wa kuongeza nguvu zaidi katika kusisitiza uhusiano mkubwa
kati ya kukuza utamaduni wa amani na kuimarisha jitihada za ukomeshaji wa silaha na
kuenea kwake. Kuenea kwa silaha hizo huongeza wazi hali ya migogoro na matokeo yake
ni gharama kubwa za binadamu na ambazo hudhoofisha maendeleo na utafutaji wa amani
ya kudumu.
Akifafanua zaidi juu ya hilo anasema,utamaduni wa amani unaweza kustawi tu katika utamaduni wa msamaha. Msamaha ni muhimu kwa upatanisho na kujenga amani, kwa sababu unafanya uponyaji na upyaji wa mahusiano ya binadamu iwezekanavyo. Kusamehe siyo kinyume na haki lakini badala yake ni kutimiza, hivyo msamaha unahukumu maovu kwa maovu na kuongoza njia ya uponyaji mkubwa wa majareha yanayotokea ndani ya mioyo ya kibinadamu. Kwa hiyo, utamaduni wa amani unahusisha uamuzi wa ujasiri wa kuruhusu majeraha ya siku za nyuma utoweke ndani kwa sasa na baadaye. Katika Ujumbe wake wa Siku ya Amani Duniani tarehe mosi Januari mwaka huu, Baba Mtakatifu Francisko anathibitisha kwamba amani ni zawadi, ni changamoto na kujitoa. Ni zawadi, kwa sababu inatoka katika moyo wa Mungu. Ni changamoto kwa sababu ni vema kwani ni ambayo haiwezi kamwe kuchukuliwa kwa lazima lakini inapaswa kupatikana daima. Na ni kujitoa kwa sababu inahitaji juhudi ya dhati kwa watu wote kwa lengo la kuitafuta na kuijenga Amani hiyo.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |