Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Vatican \ Hotuba

Kuna changamoto kubwa zinazoikumba familia mijini na vijijini

Askofu Mkuu Bernadito Auza anatafakari pamoja juu ya utekelezaji bora wa Ajenda mpya ya miji na kujadili ripoti ya kupanuka na kuimarisha ufanisi wa UN- Habitat. - RV

08/09/2017 14:42

Hotuba ya Askofu Mkuu Bernadito Auza Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa New York kwenye Mkutano wa Mkuu unaohusu ufanisi wa utekelezaji wa Mipango ya miji na nafasi ya Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Makazi uliofanyika tarehe 5 Septemba 2017. Majadala wa Mkutano huo ulikuwa ni  kuhusu maendeleo yaliyomo katika ripoti ya Jopo la kujitegemea ili thathimini na kukuza ufanisi wa Shirika la Umoja wa mataifa la makazi duniani UN-Habitat 2017.

Ameshukuru kwa fursa hiyopewa  Askofu Mkuu Bernadito Auza, na  kutafakari  pamoja juu ya utekelezaji bora wa Ajenda mpya ya miji na kujadili ripoti ya  kupanuka na kuimarisha ufanisi wa UN- Habitat. Ajenda yoyote ya miji  endelevu lazima kwanza ipewe mazoezi  ya  kanuni  msingi ya watu kwanza. Ikiwa ni katika mazingira ya vijijini au mijini. Serikali na wadau wote wana jukumu la kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha kuwa, wote wanaweza kuwa na njia ndogo zinazohitajika ili kuishi kwa heshima na kwa njia inayowawezesh  wale wanaohitaji na siyo wale wanaofaidika tu kwasababu na wao pia ni mawakala wa maisha yao yenye heshima. Katika suala hili, ni kama Baba Mtakatifu Francisko alivyothibitisha, juu ya mipango ya miji kwamba, lazima na daima kuzingatia maoni ya wale wanaoishi katika maeneo hayo.

Changamoto kubwa katika utekelezaji wa Agenda mpya ya Mjini, ni lazima kuiwezesha ili kuifikia upya wa miji na mipangilio ambayo ni msingi wa mwanadamu katika kujenga na kuunda miji endelevu, jumuishi,salama na amani inayoweza kutoa mazingira mazuri kwa wenyeji wote.
Pamoja na mwelekeo huu, ujumbe wake  kuhusu  kipengele namba  kumi cha  ripoti hiyo anasema,inahitaji kuzingatia mikoa ya miji, ikiwa ni pamoja na miji, maeneo ya pembeni na vijiji ambavyo vinaweza kuongezeka kwa idadi kubwa ya watu hadi kuwa miji na kusabisha ushindani  au uhaba wa rasilimali na maendeleo. Kuhusu onyo dhidi ya uhaba mkubwa wa utawala mzuri wa vijiji-mijini, Baba Mtakatifu Francisko anathibitisha kuwa, kwa njia ya ushawishi wa vyombo vya habari, maeneo ya vijijini wanaathiriwa na mabadiliko ya kitamaduni, hasa  yanayoathiri maeneo ya mijini na kubadilisha maisha yao ambapo kuna hali ya kuathiri malengo ya agenda ya maendeleo endelevu 2030 ambayo hayataki kuacha mtu nyuma.

Wakati uwekezaji na huduma zimezingatiwa katika maeneo ya mijini na kuharibu vijiji, hii inaweza kusababisha,  kuondoka kwa watu  vijijini kuelekea  mijini na kusababisha vijiji vilivyoachwa,kuundwa kwa makazi yasiyo rasmi ambayo yanazunguka miji na hasa kama hakuna utawala na mapendekezo mazuri. 
Kiini cha msingi cha maendeleo yoyote ya kijamii, ikiwa ni pamoja na maendeleo ya mijini, ni familia. Changamoto nyingi zinazokabili familia wakati wetu zinaweza kuongezeka hata  katika mazingira ya mji mkuu.Kwa kuzingatia jambo hili, utekelezaji wa Agenda mpya ya mjini, inapaswa kujitahidi kuhakikisha kwamba familia, hasa wale walioachwa nyuma, wanafurahia haki zao za msingi, kama vile haki ya makazi ya kutosha, ambayo ni sehemu ya haki ya kiwango cha kutosha ya kuishi. 

Zaidi ya hayo, maisha ya mijini yanahitaji mwelekeo wa jamii na jirani. Ili kukuza viwango vya kijamii vya maisha ya mijini na kuepuka ubaguzi. Kuna haja ya kuunda na kulinda nafasi jamii, kuwa na  mtazamo wa  miji ambapo kuna uwezekano wa wenyeji wanapata hali nzuri na kujisikia kama wako ndani ya miji yao. Hata hivyo Askofu Mkuu anasema, hii ni changamoto ya kusisimua, hasa katika miji ya ndani na na pembeni mahali ambapo unapfanyika uchaguzi ni kubomoa na kuhifadhi nafasi na alama ili kuweza kuupyaisha mji na utambuzi wa watu.Hisia ya kushirikisha nafasi na urithi wa kawaida katika vitongoji inaweza pia  kusaidia kuungana na kuunganisha wakazi.

Kuishi katika jiji kubwa kuna changamoto nyingi. Miji huunda aina fulani  ya kudumu kwa sababu, wakati wanataka kuwapa  wakazi uwezekano mkubwa, wao pia  huwapa vikwazo kutokana na  kuongezeka kwao. Hata hivyo miji bado ni kitu kimoja ambapo ni utajiri mkubwa katika ulimwengu wetu. Miji ni kama sufuria uliyowekwa ndani pamoja mkusanyiko wa utamaduni, mila, uzoefu wa kihistoria, lugha, mavazi na vyakula ambavyoo wanakijiji huleta pamoja. Kwa hiyo basi hebu tufanye maeneo yetu yawe  makuu ya kusisimua ambayo sisi sote tunaishi.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

08/09/2017 14:42