Kardinali Ferdinando Filoni Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uinjilishaji wa watu tarehe 28 Juni 2017 alimteua Gombera wa Seminari ya shirikisho la Majimbo ya Mtakatifu Josephine Bakhita na Majimbo makuu ya Ngaundere nchini Cameruni, Padre Andre Pekeu aliyekuwa Padre la Jimbo la Yagoua.
Gombera mpya alizaliwa tarehe 27 Mei 1974 katika kijiji ka Mindjil. Amefanya mafunzo ya falsafa na Taalimungu katika Seminari Kuu ya Maroua na kupata daraja Takatifu la upadre tarehe 25 Juni 2005. Aliendelea na masomo yake ya usimamizi wa fedha katika Chuo Kikuu Katoliki cha Afrika huko Yaounde. Baada ya kupata daraja la upadri alikuwa Paroko katika maparokia mbalimbali pia utume mwingine kama mchumi wa jimbo,huduma ya Kanisa dogo huko Codas – Caritas na Katibu msaidizi wa Askofu.
Hali kadhalika nchini Zimbabwe, Kardinali Filoni, tarehe 1 Juni
2017 alimteua Gombera mpya wa Seminari Kuu ya Shirikisho ya Majimbo Harare, Padre
Andrew Lastborn Foto padre wa Jimbo la Masvingo.
Gombera mpya alizaliwa tarehe 10 Desemba 1976. Baada ya shule ya msingi alijiunga
na Seminari ndogo ya Chikwingwizha na baadaye kuendelea na Seminari Kuu kupata diploma
ya mafunzo ya Falsafa na Taalimungu.Aliendelea na mafunzo ya dini katika Chuo Kikuu
Zimbabwa 1997-2001 na kupokea daraja Takatifu la upadre tarehe 23 Juni 2003. Mnano
mwaka 2005-2011 aliendelea na masomo ya uzamivu wa Biblia katika Chuo Kikuu cha Kipapa
Urbaniano mjini Roma.
Katika maisha yake ya kichungaji amewahi kuwa paroko msaidizi katika jumuiya tofauti
za parokia na kusimamia Kanisa dogo katika shule na vyama vya kitume vya wanafunzi.
Amewahi kuwa Katibu wa Askofu na tangu mwaka 2015 alikuwa Gombera wa Seminari ndogo
ya Mt. Kizito pia muhamasishaji wa miito katika jimbo.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |