2017-09-08 15:16:00

Ask.Mkuu Jurkovic: Kuna athari zaidi za waathirika wa mabomu ya hatari


Askofu Mkuu Ivan Jurkovič, mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Umoja wa mataifa ametoa hotuba katika kwa mashirika mengine ya Kimataifa huko Geneva katika Mkutano wa 7 wanachama wa  Mkataba wa Kimataifa wa kupiga marufuku mabomu yenye kusababisha maangamizi makubwa .
Ameanza kwa shukrani za dhati kumruhusu kutoa ujumbe wake kwa wakurugenzi wa ulimwengu kwa jitihada zao zinazofanywa  katika Mkutano wa Mkataba wa Kimataifa wa kupiga marufuku mabomu yenye kusababisha maangamizi makubwa. Anathibitisha ushirikiano wao huo kuwa , hakuna swali la kujiuliza kwamba, tangu  Mkataba wa Kimataifa wa kupiga marufuku mabomu yenye kusababisha maangamizi makubwa  kuanza kutumika ni mambo mangapi yametendeka kwasababu, kumekuwapo michango ya pamoja na ushirikiano kati ya wadau mbalimbali  na imefanikisha maendeleo muhimu na kufanya utofauti halisi duniani, hasa kati ya waathirika walioathirika pia miongoni mwao wale ambao wamesaidia kuzuia.

Hata hivyo,anasema,  tunapoadhimisha mwaka wa 7 wa kujikita  kwa nguvu katika mkataba huo wa Kimataifa wa kupiga marufuku mabomu yenye kusababisha maangamizi makubwa,  bado kuna wito unaokumbusha  nguzo hii kwamba inendelee kutumiwa katika badhi ya migogoro mingine leo kwasababu kuna hatari za kuenea na kuongeza waathirika wapya. Ni lazima kujikita zaidi katika mkatabu huo uliopitishwa kwani ni muhimu kushikilia wajibu wetu wa kimaadili na kulinda heshima ya waathirika, kurudia kupiga marufuku chini ya Mkataba kupitia mboni ya kibinadamu.
Sio tu kwamba suala la ulimwengu lemye kuwa na  matokeo ya moja kwa moja juu ya uendeshaji na utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa kupiga marufuku mabomu yenye kusababisha maangamizi makubwa lakini pia njia ya kupunguza mabomu hayo yanyoe leta athari, ili hata binadamu aweza kufurahia jitihada hizo za kimataifa katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu kwa ufanisi zaidi.

Utekelezaji wa kimataifa kwa Mkataba huo kwa  kuzingatia viwango vyake, utachangia kufikia maendeleo endelevu ya kawaida ya mwanadamu. Na hasa ufunguzi wa maeneo yaliyochafuliwa, ushirikiano wa kimataifa na usaidizi kwa waathirika ni muhimu kwa  kufikia maendele endelevu ya  2030 na kuzuia majeraha ya baadaye. Askofu Mkuu Ivan anasema, Vatican  bado ni thabiti katika kujikita na kuamua kuchangia ili kuleta ufanisi dhidi ya changamoto hii ya kibinadamu. Kwa njia hiyo ni wito kwa majimbo yote na nchi zote  hata wale walio nje ya Mkataba huu ili kuzingatia kujiunga na jitihada za kimataifa katika  kufikia  lengo la wote  pamoja katika kujenga zaidi dunia iliyo bora, salama na ushirikiano zaidi.

Amemaliza akisema,hebu tuongeze  jitihada zetu mara mbili  na tuwe na nia ya kuunga mkono ulimwengu huu katika utekelezaji kamili wa mkataba wa kupunguza mabomu ya maangamizi makubwa  kama ilivyoelezwa katika mpango wa utekelezaji wa Dubrovnik na kuhakikisha kuwa, baadaye vituo vya makundi hayo haviwezi kuwa sababu ya mateso ya wanadamu. Tuna deni hili kwa waathirika wengi wa zamani na kuzuia waathirika wengine zaidi.

Ikumbukwe kwamba Mkataba wa Kimataifa wa kupiga marufuku mabomu yenye kusababisha maangamizi makubwa ulianza kutumia rasmi tarehe 1 Agosti 2010.Mabomu hayo yajulikanayo kama cluster yakilipuka hufuatiliwa na milipuko mingine kadhaa yenye uwezo wa kusababisha maafa katika maeneo makubwa. Wanaharakati wanaopinga silaha hizo wanasema mabomu hayo kwa kawaida yanashindwa kulipuka na kubaki hivyo kwa miaka kadhaa , na hivyo kuwa hatari kwa raia kwa muda mrefu baada ya mapigano kumalizika.Ni zaidi ya mataifa mia moja yaliyotia  saini mkataba wa kupiga marufuku matumizi ya mabomu hayo. Lakini baadhi ya mataifa yenye nguvu duniani,na mengineyo  kama vile Marekani, Urusi, na Pakistan na nyinginezo bado yamekataa kusaini mkataba huo, wakisisitiza kuwa silaha hizo kisheria zinaweza kutumika kwa shughuli za kijeshi.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.