Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa \ Kanisa Ulimwenguni

Patriaki Tawadros II amesema kielelezo cha mkristo ni uwajibikaji

Kama wakristo lazima kuwapokea wakimbizi kwa kufikiria kuwa ni kama baraka na zawadi kutoka kwa Mungu, na kwa kutambua kuwa sisi sote tumeumbwa kwa mfano wa Mungu - ANSA

07/09/2017 15:37

Shughuli ya ukarimu ni kielelezo cha  uwajibikaji wa mkiristo. Amayesema hayo  Patriaki wa Kiorthodox Tawadros II wa  Alessandria wakati akitoa hotuba yake kwenye Mkutano wa Kimataifa wa XXV wa tasaufi ya Kiorthodox, uliofunguliwa tarehe 6 Septemba katika Monasteri ya kiekumeni  huko Bose. Ni mkutano wenye kauli mbiu ya “zawadi ya ukarimu”. Katika hotuba yake, amesisitiza kwamba,Bwana ametufundisha kuwa wakristo tunalazimika kusikia wito na kutoa ukarimu wa upendo upeo kwa wengine na zaidi  wenye kuhitaji msaada zaidi kama wageni.

Tunaalikwa kuwapokea na kuwatunza kwasababu  kama mkristo hawezekani kuvumilia  madharau dhidi ya wageni, bali kinachotakiwa ni matendo halisi ya mshikamano, umoja na upendo.“Na hiyo ni amri ya Mungu kwa ajili ya watu wanaokuja katika nchi zetu kwamba wawe kama wazalendo na kuwapenda kama tunavyojipenda sisi”. Tawadros II anafafanua zaidi kwamba hiyo ni katika maana ya  kuonesha ukarimu, kushirikishana mali za ardhi zetu, kushirikishana safari yetu ya ubinadamu. Na hiyo ni kuonesha ukarimu wa dhati ambao siyo wa mtu kumuona kama mgeni bali kumuonesha uhusiano wa karibu ambao unapatika katikauhusiano wa ekaristi na Muumba wa Ulimwengu.

Kwa njia hiyo anasititiza kuwa, ukarimu ndiyo zoezi kubwa ambalo kama mkristo analazimika kujikita ndani yake, kwasababu ndiyo amri ya upendo wa jirani na Mungu. Akitafakari uzoefu wa ukarimu kwa kipindi cha sasa katika nchi za Ulaya anasema; leo hii nchi za Ulaya kuna  tishio na simanzi  mbele ya matukio ya wakimbizi na wahamiaji. Hayo anayatamka kutokana na kwamba anaishhi katika mipaka ya Afrika na Ulaya. Akigusia kuhusu uchungu wa bara la Afrika, Patriaki anaeleza hali halisi na mahitaji ya mamilioni ya waafrika katika chi za Rwanda , Burundi, Sierra Leone, Congo, Sudan ya Kusini na sehemu nyingine barani Afrika.

Anasema, watu wasio kuwa na makazi wanazidi kuteseka na kukimbia kutoka katika nchi zao. Unyonyaji na ukosefu wa haki za kijamii, vurugu , ukosefu wa ajira vita, ugaidi na uharibifu wa mazingira, ni matatizo makubwa ya kijamii yanayohusu jamii nzima. Amemalizia akisema kuwa, kama wakristo lazima kuwapokea wakimbizi kwa kufikiria kuwa ni kama baraka na zawadi kutoka kwa Mungu, kwa kutambua kuwa sisi sote  tumeumbwa kwa mfano wa Mungu,na  wote wanayo  haki sawa za kibinadamu kwa ajili ya maisha yao, ajira na uhuru; na ni lazima kushiriki  uchungu wa waathirika hawa. 

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

07/09/2017 15:37