Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa \ Kanisa Ulimwenguni

Patriaki Bartolomeo I anatoa wito wa ukarimu ambao ni zawadi

Patriaki wa kiekumeni Bartolomeo I amejikita kwa muda mrefu katika kuhamasisha na kutafuta suluhisho la kipeo cha mazingira ya sayari hii tunamoishi. - RV

07/09/2017 16:10

Zawadi ni ukarimu ni mada ya ambayo siyo wito unatolewa kwa Kanisa la Mungu peke yake, wala kwa waamini katika Kristo mfufuka, bni mada kwa watu wote wenye mapenzi mema ambao wanaishi katika kipindi cha kihistoria, mahali ambapo kuongea maana ya ukarimu inawezekana ikawa wengine bugudha, badala ya kutambua ukarimu ni zawadi.

Ni maneno ya Patriaki wa Kiekumeni wa Costantinopoli Bartolomeo I katika hotuba yake ya Mkutano wa Kimataifa wa XXV wa tasaufi ya Kiorthodox. Patriaki wa kiekumeni amejikita kwa muda mrefu katika kuhamasisha na kutafuta suluhisho la kipeo cha mazingira ya sayari hii tunamoishi. Kwa njia hiyo,hotuba yake imelenga zaidi mada ya ukarimu wa binadamu katika ardhi ya kuishi. Patriaki anasema, matendo ya kibinadamu yanakumbusha yale ya uumbaji ambayo hutoa uhusiano wa uwajibikaji. Mungu ni mwajibikaji kwa ajili ya kazi yake ya uumbaji, ambayo amemkabidhi binadamu kutunza kila kiumbe kwa jina lake. 

Baada ya kuzungumzia kazi ya uumbaji na uhusiano wa Mungu anasema, katika kuhama hama kwa binadamu ni kama kuonesha uhusiano mbaya ambao kwa wakati fulani wa kihistoria ulikuwa na maono ya mwanadumu  kwamba umeonekana kama ardhi ni mahali pa rasilimali ya kutumia kwa ajili ya ustawi wa mwanadamu ambaye anatofauti na viumbe wengine. Lakini licha ya dhambi ya Adamu na Eva, Mungu hakuvunja agano na mwanadamu, uhusiano wake unaendelea hata sasa baada ya kuanguka dhambini. Nchi bado inabaki kuwa ya kuishi kwa vizazi vilivyopo na vijavyo, hivyo ukarimu ni kushirikisha,ni kujifungulia   kila mmoja na wengine, ni kujibidisha  kuwatunza wengine. Katika mfano wa Msamaria Mwema, kuna  tendo la kuwakaribisha wageni lakini na  hakuna wahamiaji  isipokuwa wageni, kwakuwa mwenyeji wa mgeni na mgeni, inamaanisha kumkaribisha  Kristo mwenyewe.

Sr Angela Rwezaula
 Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

07/09/2017 16:10