Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa \ Kanisa Ulimwenguni

Kukarimu Wahamiaji na Wakimbizi ni kumpokea Yesu mwenyewe

Enzo Bianchi anakumbusha hukumu ya mwisho ambayo Yesu anasema kuwa alikuja kama mgeni, mwenye njaa, mgonjwa na mfungwa lakini hakusaidiwa

07/09/2017 15:08

Katika dunia hii tunamoishi milioni ya watu wanalazimika kuacha nyumba na ardhi yao kwasababu ya vita, mateso manyanyaso  na njaa. Wahamiaji na wakimbizi wanaobisha hodi katika milango yetu wanachangamotisha dhamiri za binadamu hasa  wakristo kila siku ili watafakari kama wameweza kumtambua mgeni ambaye ni Yesu Kristo Mfufuka. Ni maneno  ya Enzo Bianchi mwanzilishi na Mkuu wa Jumuiya ya  Monasteri ya Bose wakati wa kufungua Mkutano wa Kimataifa wa XXV wa Kiekumeni juu ya tasaufi ya Kiorthodox ikiwa na kauli mbiu ya Ukarimu ni zawadi. 

Akiwakilisha ratiba ya mkutano huo ambao  umeanza tarehe  6 Septemba na utamalizikia 9 Septemba, Enzo Bianchi amebainisha  kuwa kabla ya ukarimu kuwa fadhira ya kuweka katika matendo, hawali ya yote ukarimu ni zawadi tunayopokea. Katika ripoti yake amekumbusha kuwa, wakristo wote katika historia na duniani tunao uwajibu wa kutimiza, hawali ni kusoma ishara za nyakati, yaani kuwa makini katika dharura mbalimbali na matukio ya uwepo wa Bwana katikati ya Binadamu.

Katika uhusiano wetu kati ya maskini, mgeni na mahitaji, amesema Bianchi , ipo   haja  kwanza kuuweka katika makundi mawili  ya kijamii na kitaalimungu. Hiyo ni kwasababu uhusiano wetu kati ya  maskini, mgeni na mahitaji  haupo  katika nafasi ya maadili lakini  upo katika nafasi ya ufunuo kwasababu Mungu wetu  anajionesha kwa njia yao. Kwa hiyo hatima ya mgeni siyo upendo, huruma na msamaha tu, bali ni mahali pa maonesho ya Mungu na Yesu Kristo ambapo kwa njia ya mafundisho ya Kanisa yanaeleza.  Kutokana na maandiko hayo Bianchi anaonesha hukumu ya mwisho akisema;  katika ufunuo wa mwisho  kwa uhakika utaoneshwa kwamba Mwana wa Mtu katika historia alikuwa na kiu na njaa, mgeni, mgonjwa, mfungwa ambaye kila mtu alikutana naye lakini akabaki bila kuguswa naye au bila kufanya lolote la kumwonea huruma.

Katika uchaguzi huo, kila mmoja wetu atahukumiwa;  Bianchi ameonya akinyoshea kidole chake kwa hali ile ya ubaridi wa  roho za watu wengi ambao unaweza kusababisha hata ugonjwa wa kugandamana mwili na kwamba siyo mfano wa Mungu anaye ishi kati yetu.
Anaongeza Bianchi kwa kumaliza hotuba yake kuwa, katika tukio la ukarimu wa mgeni unaweza kuwa fursa ya kukutana na Kristo mwenyewe , kwasababu kukaribisha mgeni ni mojawapo ya vigezo vya hukumu ya mwisho. Imani na ukarimu ni mambo mawili yenye  nyuso mbili katika sarafu moja, kwa njia hiyo Imani inakarimu na ukarimu unaongeza imani ya upendo wa Mungu na jirani.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

07/09/2017 15:08