Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Amani

Nigeria:Padre Ciriacus Onukwo aliyekuwa ametekwa nyara ameuwawa

Padre Ciriacus Onukwo aliyekuwa ametekwa nyara ameuwawa nchini Nigeria - RV

06/09/2017 16:56

Padre Ciriacus Onukwo aliyekuwa ametekwa nyara katika Serikali ya Kusini mwa Nigeria ameuwawa. Kwa mujibu wa Polisi tarehe 1 Septemba, Gari la Padre Onukwo ilisimamishwa katikati ya kona ya Bana na Amaifeke na watu wenye silaha ambao walimteka nyara.  Shirika la habari la Fides linasema, Padre huyo alikuwa akitoa huduma huko Orlu ambapo alikuwa anaelekea kijijini nyumbani kwao Orsina kuudhuria mazishi ya padre mmoja aliyeaga dunia tarehe 28 Agosti.

Mwili wa marehemu umepatika tarehe 2 Septemba katika kijiji cha Omuma. Paolisi wanathibitisha kuwahakuonesha  majeraha yoyote  au  mikato yoyote bali Padre Onukwo amekuwa kwa sababu ya kunyongwa. Kwa njia hiyo wapelelezi wanaendelea na uchunguzi zaidi. Aidha wanathibitisha wakisema ni dhahiri kuwa kesi  hiyo ni ya kutekwa nyara na kuwawa, kwa maana kama angekuwa ni kutekwa nyara tu, watekaji nyara wangesikika wakiita familia ya marehemu kutaka fidia.

Hali kadhalika kuwawa kwa wachungaji  ni vitendo ambacho kimeenea sana katika bara la Amerika ya Kusini ambapo nchini Brazili mwishoni mwa mwezi wa nane, Padre  Pedro Gomes Bezerra  mwenye umri wa miaka 50 ambaye alikuwa na utume wa kichungaji katika  Parokia ya Mama yetu wa Karmeli alikutwa ameuwawa katika nyumba yake. Taarifa inasema, tangu mwanzo wa mwaka 2017,wamefikia mapadre 7 walio uwawa katika bara la Amerika ya Kusini.

Aidha Paolisi  amethibitisha hayo pamoja na msemaji kutoka Jimbo la Guarabira Nchini Brazil kuwa mauaji  ya padre huyo  yalitokana katika harakati kutaka kufanya wizi ndani ya nyumba ya padre. Ni huzuni kubwa Katika jimbo na viongozi wa Kanisa, kama alivyo eleza msemaji wa Jimbo Monsinyo Jose Nicedomus. Hata hivyo upelelezi unaendelea wakiwa na matumaini ya kufikia kuwakamata waliotenda jambo hilo haraka iwezekanavyo.

Habari zaidi zinasemekeana kuwa tangu mwanzo wa mwaka huu wahudumu 15 wa kichungaji wamewawa duniani, miongoni mwao ni mapadre 11, makatekista 2 na mtu mmoja wa kujitolea katika Kanisa. Na kati ya mauaji hayo wanne ni kutoka nchi ya Mexico, Bolivia, Venzuela, Colombia na Brazil. Afrika ni waathirika saba kwa namna ya pekee katika nchi ya  Nigeria, Burundi, Sudan ya Kusini na Camerun mahali ambapo wameuwawa mapadre wawili wakati huo hup Barani Asia katika nchi ya Ufilippini tarehe 20 Agosti pia aliuwawa Katekista mmoja.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya radio Vatican

 

06/09/2017 16:56