Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Vatican \ Hotuba

Kardinali Koch: umuhimu wa Wakristo kutembea pamoja katika uekumene!

Jumuiya ya Wamonaki wa Bose wameambiwa kuwa Ibrahimu alifanya uzoefu wa kukaribisha mgeni kwa njia hiyo ni binadamu anamkaribisha Mungu mwenyewe - RV

06/09/2017 16:21

Kardinali Kurt Koch kwa niaba  ya Baraza la Kipapa la kuhamasisha umoja wa Wakristo na yeye binafsi anapenda kuwatumia salamu wote wanaoshiriki  mkutano kuanzia kwa Patriaki Bartolomeo wa kwanza, Patriaki  Theodros wa Alesandria na Afrika nzima, maaskofu wamonaki wakristo wawakilishi wa makanisa ya Kiorthodox na washirki wote katika mkutano huo wa XXV wa Kimataifa wa Tasaufi ya  Kiorthodox.  Kardinali Koch  anasema katika kuadhimisha mwaka wa 25  wa Mkutano huo anapenda kumshukuru Mungu na kuwapongeza Jumuiya ya Monasteri ya Bose kwa kuanzisha  tukio hili ambalo kwa miaka mingi sasa imekuwa  muhimu katika mahusiano ya Kiorthodox na Wakatoliki; Pia yeye binafsi alivyo weza kufanya uzoefu huo mwaka jana alipoweza karibishwa mahali hapo. Kauli mbiu ya Mkutano huo ni zawadi ya kukaribishwa , ambapo anasema kuwa  inatokana na moyo wa taufi ya kikristo.

Kwani hiyo siyo kwa bahati mbaya kuona kwamba ni Fumbo la imani ya kikristo na Utatu Mtakatifu ambao  unawakilishwa na mgeni katika nyumba ya Ibrahimu , na ambayo wao wamechagua kama kauli mbiu ya mkutano huo. Katika ishara yake; Ibrahimu alifanya uzoefu wa kukaribisha mgeni,kwa njia hiyo ni binadamu anamkaribisha Mungu mwenyewe. Na hiyo ni kwasababu Yesu mwenyewe anasema anayenipokea mimi anapokea yule aliyenituma. Kwa ulinganifu  wa makaribisho hayo ni kusema kwamba yule anayepokea anafanya uzoefu wa kukaribishwa na  Mungu. Na ndiyo maana hiyo picha ya mgeni wa Ibrahimu haioneshi  tu makaribisho ya binadamu, bali hata makaribisho ya Mungu. 

Ni ishara ya umoja kwa maana ya ekaristi, mahali ambapo Utatu Mtakatifu unaalika kila mmoja kushiriki umoja na Mungu. Katika Karamu ya milele kwa wale waliokombolewa, Neno takatifu linasema; Bwana atajifunga mkanda  kiunoni atawaketisha mezani na kuwahudumia.
Utatu Mtakatifu  siyo jambo lisilokuwapo kwani  ni mpango  wa maisha ya kijamii . Leo hii suala hili la kukaribisha ni changamoto kubwa katika milango ya jamii zetu mahali ambapo watu wengi wanazidi kubisha hodi wafunguliwe maana wamelazimishwa na kulazimika kuacha nchi yao. 

Kardinali Koch anasema; mbele ya changamoto hizi, kwa mujibu wa maadili kama ilivyoandikwa na Max Weber, ineweza kufuata maadili ya aina mbili: maadili ya kukubali na maadili ya uwajibikaji. Siyo rahisi kudharau uchaguzi wa maadili mengine kwani kila maadili katika ngazi binafsi na hata kisiasa ni lazima kuwa sawa katika kuongozwa na msingi wa kukubali na kujikita kwenye uwajibikaji; mambo hayo mawili yanakwenda pamoja. Lakini ni jinsi gani ya kujikita katika kukubali na kuwajibika?:Kard, anatumia mifano hali a kuwa; Baba Mtakatifu Francisko, Patriaki Bartolomeo na askofu Mkuu Ieronymos katika hati yao ya pamoja iliyotia saini tarehe 16 Aprili 2016,  walionesha kwamba uwajibikaji wa kweli hauweki kizingiti cha kukaribisha; badala yake ni kinyume kwasababu ni kufungua mikono wazi kukaribisha wengine na wakati huo huo ni kijibu mahitaji ya kesi nyingi za binadamu  walizo nazo kutokana na kauacha  nchi zao ili kutafuta maisha bora .

Pamoja  na hiyo inayofanan nayo ni ile ya  Papa na Patriaki Cyril katika waraka wao wa pamoja wa tarehe 12 Februari 2016, walikuwa wametoa wito wa kutafuta suluhisho la sababu zinazowafanya wahamiaji kuondoka katika nchi zao, hata tofauti za migogoro au zile za ukosefu wa ugawaji rasilimali katika dunia hii.  Na hati hizi za hivi karibuni zinaonesha kweli suala  la wahamiaji  na makaribisho kwamba ni mada nyeti  na msingi  katika mahusiano kati ya wakatoliki na waorthodox kwa ujumla katika mahusiano ya kiekumeni. Kwa njia hiyo Kardinali anatoa shukrani zake kwa jumuiya ya kiekumene ya Bose kuandaa mkutano huo juu ya mada hiyo nyeti  ambayo yeye binafsi anasema; ni fursa kubwa ya kuweza kubadilishana mawazo, wakati huo huo  kuwawezesha washiriki wote  kufanya uzoefu wa kindugu katika ukarimu wa kukaribisha na kupokelewa.

Vilevile mkutano huo unaweza kuwa fursa kwa wote wakatoliki na waorthodox kama ahujaji wa  Emmau wakitembea pamoja na  wajadiliana wakisindikizwa na Kristo. Na kama mitume wa Emmau katika safari hiyo ya pamoja wanaweza kukaribiana kila siku, siyo tu kutambuana bali katika kupokea pamoja mwili na dam ya Yesu Kristo pamoja katika umungu wake na undugu wa milele.

Sr.  Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

06/09/2017 16:21