Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Papa Francisko: Ninakuja kwenu kama mjumbe wa amani na matumaini!

Baba Mtakatifu katika ujumbe wake wa video kwa watu wa Colombia anasema, Ninakuja kama muhujaji wa matumaini na amani kuadhimisha na ninyi imani katika Bwana - EPA

05/09/2017 15:21

Ninakuja kwenu kama hujaji wa matumaini na amani kuadhimisha na ninyi imani katika Bwana, hata kujifunza upendo na uvumilivu wenu katika njia ya kutafuta amani na maridhiano. Ni katika maneno haya Baba Mtakatifu Francisko amefungua ujumbe kwa njia ya Video unao wahusu watu wa Colombia, nchi ambayo anaitembelea kuanzia Jumatano 6 -11 Septemba 2017. Akitamka kauli mbiu ya ziara  yake, tupige hatua ya kwanza, Baba Mtakatifu anawaalika kutengeneza madaraja ya kindugu pia kuunda njia mpya ya amani ambayo yeye mwenyewe amekuwa akihamasisha na kuwatia moyo. Amani ni ile ambayo nchi ya Colombia imekuwa ikiitafuta na ambayo imechukua safari ya muda mrefu. Amani thabiti na ya kudumu ili kuweza hatimaye wote wanaishi kama ndugu na siyo maadui. Baba Mtakatifu anaongeza; amani hiyo inatukumbusha kuwa sisi sote ni ndugu wa Baba mmoja anaye tupenda na kututia nguvu.

Baba Mtakatifu anasema ni baada ya utambuzi wa jitihada za wale waume na wake ambao wamefanya kazi kwa ujasiri  na uvumilivu ili kuweza kuifanya nchi ya Colombia iwe sehemu ambayo inatawaliwa na umoja na undugu au mahali ambapo Injili imefahamika na kupendwa. kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anatoa wito hata kwa Kanisa kuhamasisha  lakini siyo tu mapatano ya Bwana na ndugu bali hata uhamasishaji wa huduma ya mazingira ambayo yametumika vibaya na kunyonywa. Ujumbe unamalizika kwa kusema, mwezi wa sita mwaka huu umehitimishwa mchakato wa amani kati ya Serikali na Farc ambapo ni kwa miaka zaidi ya 50 wamekuwa katika vita ambavyo vimesababisha zaidi ya vifo 260,000  na zaidi ya watu 60,000 kupotea katika mazingira ya kutatanisha, pia na kusababisha wakimbizi milioni saba.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

05/09/2017 15:21