Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Mama Theresa wa Calcutta ni shuhuda wa upendo na huruma ya Mungu!

Tarehe 5 Septemba ni siku ya kukumbuka miaka 20 tangu kifo cha Mtakatifu Teresa mama wa Masikini - EPA

05/09/2017 15:59

Kama Mama Theresa , tufungue upeo wa furaha na matumaini kwa watu wengi walio kata tamaa na wenye kuhitaji kuguswa na huruma ya Mungu. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko aliyotolewa tarehe 5 Septemba 2017 katika Tweet ya Pontifex kwenye lugha 9. Ni siku ambayo inakumbuka miaka 20 tangu kifo cha Mama wa Maskini  wakati huo, tarehe 4 Septemba ilikuwa ni kumbukumbu ya  mwaka wa kwanza tangu  kutangazwa kuwa mkakatifu na Papa Francisko katika viwanja vya Kanisa kuu la Mtakatitu Petro.  Mama Theresa ni mwanzilishi wa Shirika la Wamissionari wa Upendo na mwenye tuzo ya amani  ya Nobel ya mwaka 1979.  Ni mtawa ambaye ni mfano wa pekee katika maajabu ambayo yanaweza kujikamilisha ndani ya kujitoa kwake Yesu Kristo.

Tarehe 26 Oktoba 1985 akiwa katika Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa wakati huo  Pérez de Cuéllar alimwelezea mama Theresa kuwa ni mwanamke mwenye nguvu zaidi katika dunia. Licha ya Mtawa huyo mdogo katika mavazi yake rahisi, alipendelea kujiita kuwa yeye ni kalamu ndogo ya risasi katika mikono ya Mungu. Karamu ndogo ya risasi lakini yenye uwezo wa kuandika kurasa nyingi kuhusu huruma na ambaye kwa nguvu ya imani yake aliweza kufungua nyumba nyingi za wahitahi hata katika maeneo yasiyoelezeka, kuanzia Quba hadi katika muungano wa nchi za Kisovietiki. Na kila mmoja aliyeuliza siri yake ni ipi alijibu  kwa urahisi kwamba anasali.

Katika tukio la kutangazwa mtakatifu tarehe 4 Septemba 2016, hata  Baba Mtakatifu alisema, tutakuwa na shida kidogo ya kumwita Mtakatifu Theresa, kwa sababu utakatifu wake uko karibu sana na sisi  kiasi cha kuona kwamba yeye  ni mwema na amekwishatoa  matunda na hivyo kwa urahsi tutendelea kusema Mama Theresa. Aidha aliongeza; mtu huyo asiyechoka katika jitihada za huruma , atusaidie kuelewa zaidi na zaidi kwamba kigezo kimoja tu cha matendo ni upendo wa bure, bila kuwa na itikadi yoyote na dhamana yoyote, kutokuwa na ubaguzi na bila utofauti wa lugha , utamaduni, rangi au dini. Na kwamba Mama Theresa alipenda kusema hata kama sizungumzi lugha yao, lakini ninaweza kutabasamu.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

05/09/2017 15:59