2017-09-04 09:27:00

Papa:Tusiogope kubeba misalaba maana mateso ya Yesu ni matunda ya ufufuko


Ni wito wa kutokuwa na hofu ya kubeba msalaba, na siyo kubeba msalaba bila kuwa na Yesu  maana ni Yesu aliye wambwa msalabani akateseka kwa ajili ya upendo wa Mungu na ndugu; kwa hakika yale mateso kwa neema ya Yesu ni matunda ya ufufuko. Ni maneno aliyo tamka Baba Mtakatifu Francisko  katika sala ya Malaika wa Bwana Jumapili 3 Septemba 2017, kwa mahujaji wote walio udhuria kusali naye sala katika viwanja vya Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Kutumia taranta binafsi, nguvu binafsi na wakati wako binafsi kwa ajili ya kuokoa, au kuhifadhi na kujikalimisha binafsi, inapelekea hali halisi ya kuishi kwa huzuni na kutozaa matunda. Badala yake tunapoishi kwa ajili ya Bwana na kuweka maisha yetu yote katika upendo kama alivyo fanya Yesu, tunaweza kuonja furaha ya kweli. Maisha yetu hayatakuwa tasa bali yatazaa matunda. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko anakumbusha kannuni ya dhahabu ambayo Mungu aliandika katika asili ya binadamu aliyeumbwa katika Kristo kwamba, upendo unatoa maana na furaha katika maisha.

Tafakari la Baba Mtakatifu inatokana na Injili ya Jumapili iliyosomwa ambapo Mtakatifu Matayo anaeleza juu ya Mtakatifu Petro alivyotambua kuwa Yesu anapaswa kuteseka, kuwawa pia kufufuka. Alikamkatalia kuwa hayo matukio  hayatamtokea. Lakini Yesu alimkaripia kwa nguvu na kumwambia kwamba hafikiri kwa mujibu wa Mungu bali anafikiri kama wanadamu. Katika kufafanua zaidi Baba Mtakatifu anasema, ni katika jiwe la msingi na nguvu ambalo Yesu anataka kujenga juu yake Jumuia, lakini wakati huo huo, Mtume Petro anakuwa kizingiti, yaani ni jiwe lakini ambalo huwezi kujenga juu yake na  jiwe la kujikwaa katika njia ya Masiha; kwa njia hiyo papa anaeleza, Yesu anatambua kuwa Petro na wafuasi wengine bado wanayo safari ndefu ya kutembea kabla ya kuwa mitume wake

Njia aliyoelekeza Yesu, Baba Mtakatifu anasema, ni ile ya kujikana binafsi, kuchukua msalaba na kumfuata. Daima hata leo hii kishawishi ni kile cha kutaka kumfuata Yesu bila msalaba,na mbaya zaidi ni ile ya kutaka kumfundisha Mungu njia ya kweli ya kupitia. Lakini Yesu mwenyewe anakumbusha kwamba njia yake ni njia ya upendo, lakini hakuna upendo wa kweli bila ya kujitoa sadaka.
Wote tunaalikwa kutokufuta au kusikiliza ulimwengu huu, bali daima kuwa na utambuzi muhimu wa ugumu wa ukristo katika kutembea kwenye  kilima na kupinga hisia za ulimwengu huu.

Mara nyingi Yesu anatamka maneno yanayoeleza hekima kubwa, kwasabau daima inafaa kwamba anayekubali hisia za ulimwengu na mwenendo wa ubinafsi au anayetaka kujikoa binafsi maisha yake anapoteza, lakini atakayepoteza maisha yake kwa ajili ya Yesu  atarudishiwa maisha mapya.
Katika maadhimisho ya Ekaristia, Baba Mtakatifu anaendelea, tuishi fumbo la msalaba katika kukamilisha kumbumkumbu ya sadaka ya ukombozi, ambapo mwana wa Mungu anapoteza kabisa maisha yake mwenyewe kwa ajili ya kupokea maisha mapya kutoka kwake  Baba ili nasi sote tuweze kupokea maisha mapya kwakuwa tulikuwa tumepotea. Kushiriki ibada ya Misa Takatifu, upendo wa Kristo msulibiwa na mfufuka unakuwa kwetu sisi chakula na kinywaji kwasababu tunaweza kumfuasa katika safari yetu ya kila siku na katika ukamilisho halisi wa huduma kwa ndugu.

 Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.