2017-09-02 14:01:00

Safari ya mapatano kwa watu wa Colombia ni lazima kuifanya kila siku


Kutia sahini  katika  hati haitoshi  kwa ajili ya mchakato wa mapatano na amani bali ni kufanya zaidi ya safari ndefu  kuanzia sahini ya kusisitiza mkataba. Ni safari ambayo lazima kuitimiza kila siku, na safari hiyo lazima ifanywe na watu wote bila kubakiza mtu hasa katika akili na moyo. Kati ya tarehe 6 -11 Septemba, Baba Mtakatifu atakuwa katika ziara ya kitume nchini  Colombia kuimarisha mchakato kwa upya wa mapatano ya nchi baada ya miaka mingi ya umwagaji  damu na migogoro. Ziara ya Baba mtakatifu itakuwa katika mji mkuu wa Bogota,Villavincezio, Medellin na Cartegna. Hiyo ni taarifa kutoka kwa Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin aliyoiwakilisha Ijumaa 1 Septemba katika Sekretarieti ya Mawasiliano maana ya ziara ya 20 ya kitume ya Baba Mtakatifu ikiwa na kauli mbiu Hebu tufanye hatua ya kwanza. 

Aidha ni ziara ya kitume ya kutangaza Injili na siyo ziara ya kisiasa. Ni maneno ya msemaji wa Vatican Greg Burke aliyewakilisha naye katika vyombo vya habari Vatican, kuhusu ziara ya 20 ya kitume ya Papa Francisko. Injili inawaalika watu katika amani , msamaha na mapatano Baba Mtakatifu Francisko anapeleka ujumbe wa amani. Huo ni ujumbe muhimu katika kipindi hiki  nchini  Colombia katika mchakato mzima wa maridhiano na mapatano ya amani.
Baada ya Mwenye heri Paulo VI mwaka 1986 na Mtakatifu Yohane PauloII mwaka 1986 Papa Francisko atakuwa wa tatu kukumbatia nchi hiyo ya America ya kusini. Pamoja na mada zilizochaguliwa katika vituo vinne ambavyo baba Mtakatifu Francisko atakuwapo vinagusia juu ya  mfanyakazi wa amani, mwamasishaji wa maisha , mapatano na Mungu na wakolombia , katika mazingira, maisha ya kikristo kama utume, adhi ya kila  mtu na haki za binadamu.

Baada ya kufika mchana wa tarehe 6 katika uwanja wa ndege wa Bogotha, atawasalimia watu na kuanza msafara kuelekea katika makao ya Ubalozi wa kitume kwa kutumia usafiri ulioandaliwa . Inasadikika watu 700 elfu watakuwapo. Utume wa  Baba Matakatifu utaanza rasmi tarehe 7Sept  ambapo atakutana na Taasisi mbalimbali na kutembelea rais wa nchi Juan Manuel Santos. Atasimama katika Kanisa Kuu mahali ambapo atatoa heshima katika picha ya Mama Maria wa Chiquinquirá msimamizi wa nchi ya Colombia. Baada ya kuwabariki waamini, atakutana na maaskofu, pia kukutana na Kamati ya utendaji wa Baraza la maaskofu wa Amerika ya Kusini (Celam). Mchana ataadhimisha ibada ya misa  katika uwanja mkubwa wa Simon Bolivar na jioni atawasalimia watoto, wazee  na watu wasiojiweza watakao kuwa wamekusanyika katika ubalozi wa kitume.

Tarehe 8 ni siku ambayo Baba Mtakatifu atakuwa  Villavicencio kusini mwa mji wa Bogotha upande wa mashariki ya  Andes. Asubuhi hiyo ataadisha ibada ya misa itakayokuwa na tukio la kuwatangaza wenye heri wafia dini wa Colombia, Askofu wa Arauca  Jesús Emilio Jaramillo Monsalve na Padre Pedro María Ramírez Ramos. Ratiba elekezi inasema atawasalimia watu 10 walio nusurika  kutokana na maporomoko ya hatari ya Mocoa. Mchana anatazamia kufanya mkutano mkubwa wa maombi  kwa ajili ya mapatano ya nchi. Baba Mtakatifu Francisko amependelea mantiki ya maadhimisho ya kiliturujia, kama wanavyosisitiza mkurugenzi wa habari wa  Vatican kwamba ni muhimu kwasababu ni mkutano wa sala ya mapatano: siyo tu mkutano kwa ajili ya kukutanisha watu.

Ni mkutano wa sala ambao Baba Mtakatifu amependelea kuwa hivyo katika mantiki ya kiliturjia. Aidha msemaji wa Vatican Greg Burke anasema, katika tukio hilo watakuwapo hata waathirika na hata wanamgambo wapiganaji walio hasi kikundi chao. Hapa amesisitiza kwamba hawa ni wale ambao walihasi kikundi cha kupigana na sasa tayari wameisha wmekwisha shiriki na jamii, kwa njia hiyo ni wapiganaji wa muda mrefu na siyo wa jana au miezi kadhaa, wengine bado wanalindwa na usalama, aidha wengine  wamebaki hapo, kwasababu ni mambo mawili tofauti. 

Tarehe 9 Baba Mtakatifu Francisko atakuwa huko Medellini ambao ni mji wa pili kwa idadi kubwa ya watu baada ya Bogotha. Ataadhimisha misa katika uwanja wa ndege  wa mji, mahali ambapo hata Mtakaifu Yohane Paulo II aliadhimisha. Kwa njia hiyo atatembelea Hogar San Jose ambayo ni kituo kinachokaribisha watoto yatima na wenye matatizo. Badaye katika uwanja wa Mpira wa Macarena atakutana na mapadri, watawawote, wasemnariani na familia zao.

Tarehe 10 Septemba ambayo ni siku yake ya mwisho ya Baba Mtakatifu Francisko atakuwa Cartegna Kaskazini mwa nchi. Katika mji wa huo wa Karibien ndipo waliweka sahini ya  mkataba wa amani wa Avana Septemba 2016. Lakini pia inakukubkwa sana mji wa Cartegna na  Mtakatifu Yohane Paulo II aliyesma  kwamba ni mji ulio mkaribisha kwa miaka 40 Mtakatifu Petro Claver 1581-1654; na kwamba yeye ni mtume aliyetoa maisha yake yote kutetea waathirika na wanyanyaswaji wa utumwa. Hivyo Baba Mtakatifu Francisko baada ya kubariki jiwe la msingi wa nyumba ya wasiyo kuwa na makazi Talitha Quam atasali sala ya Malaika wa Bwana na kutembelea madhabahu ya Mtakatifu Petro Claver. Na baadaye ataadhimisha misa takatifu ambayo itakuwa ya mwisho katika ziara yake na kuwaaga watu wote tayari kuanza safari ya kurejea Roma .

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.