2017-09-01 12:13:00

Ujumbe wa Papa na Patriaki kwa Siku ya Kuombea Utunzaji wa Mazingira 2017


Katika kuadhimisha mwaka wa 3 wa  Siku ya Kuombea utunzaji bora wa mazingira mwaka 2017, Baba Mtakatifu Francisko na Patriaki wa Kiekemeni Bartholomew I,  kwa mara ya kwanza pamoja wameandika ujumbe kwa waamini wote na watu wenye mapenzi mema kuwajibika katika utunzaji wa mazingira mbele ya kipeo cha majanga ya mazingira kwa sasa. Baba Mtakatifu na Pariaki wanasema, maelezo ya uumbaji yanatoa fursa ya mtazamo wa kina katika dunia. Maandiko Matakatifu yanonesha kuwan, mwanzo Mungu alitoa ishara kwa binadamu kushirikiana, kutunza na katika kulinda mazingira asili. Kama isemavyo kitabu cha (Mwanzo 2,5):” hapakuwa na mimea juu ya nchi wala miti haikuwa imechipua kwani Mwenyezi  Mungu hakuwa ameinyeshea nchi mvua na wala hapakuwapo mtu wa kuilima”.

Tumekabidhiwa ardhi kama zawadi yenye thamani kubwa na kama urithi ambao sisi sote tunashiriki uwajibikaji ili vitu vyote vilivyo mbiunguni na duniani viweze kurudi kwake Kristo. (Ef 1,10). Utu na utukufu wa kibinadamu umeunganishwa sana na uangalizi wa viumbe vyote. Hata hivyo, katika mtazamo, ujumbe unasema; historia ya dunia inaonesha hali utofauti sana; hasa kuonesha hali mbaya ya kuanguka maadili hayo ambapo mtazamo wetu na tabia zetu mbele ya kazi ya uumbaji imeleta upofu katika wito wa kuwa washiriki wa Mungu.Hiyo yote ni kutokana na tabia zetu za kuvunja mazingira yenye umaridadi na yenye usawa wa dunia, au hamu ya kupendelea kutawala na kudhibiti rasilimali ndogo za sayari , halikadhalika, uchoyo wa kufanya biashara na kupata faida zisizo na kikomo za ardhi;  vyote hivyo vimetutenganisha na  ishara za ubunifu wa msingi  wa hawali wa kazi ya uumbaji.

Ujumbe unabainisha pia kwamba;  hatuheshimu tena asili kama zawadi iliyogawanyika;  badala yake tunaiona kuwa ni milki binafsi. Hatuna uhusiano tena na asili kwa ajili ya  kuiunga mkono; badala yake ni kuitawala kwa mabavu na kuzidi kuongeza miundo mbinu mipya ya uharibifu.  Matokeo ya maono haya ya ulimwengu mbadala ni ya kutisha na ya kudumu. Mazingira ya kibinadamu  na ya asili yanazidi kuharibika pamoja, uharibifu huo unasababisha kuzorota na kurudi nyuma pia  madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa huathiri:kwanza kabisa wale wanaoishi katika mazingira magumu kwa kila kona ya dunia. Kwa namna hiyo Baba hawa wanaeleza kwa kina kwamba,wajibu wetu wa kutumia mali  ya ardhi kwa ufanisi huhusisha kutambua na kuheshima  kila mtu na viumbe vyote vilivyo hai. Kwa njia hiyo  wito na changamoto ya haraka ya kutunza kazi ya mazingira  ni mwaliko kwa wanadamu wote kujitahidi katika maendeleo endelevu.

Ili kuweza kupata ufanisa zaidi ni lazima kushiriki kwa pamoja  wasiwasi huo kwa ajili ya kazi ya uumbaji wa Mungu na kukubali kwamba dunia ni nzuri kwa pamoja. Baba Mtakatifu na Patriaki kwa pamoja wanaawalika watu wote wenye mapenzi mema katika Maadhimisho ya Siku ya Kuombea utunzaji bora wa mazingira tarehe 1 Septemba. Kwa tukio hili pia wanatoa shukrani kwa kazi ya utendaji wa Muumba mwenye huruma kwa zawadi nzuri ya uumbaji na kuwataka watu wote kujikita kikamilifu katika kujitolea, kulinda na kuihifadhi  vema sayari hii kwa faida ya vizazi vijavyo.
Aidha ujumbe huo unasema, wanatambua jinsi gani ilivyo kazi ya bure kuifanya bila kuwa na Bwana(Zab126/127 ); kwa maana ya kwamba,iwapo sala na maombi siyo kiini cha tafakari na maadhimisho. Lengo la maombi haya ni  kubadili njia tunavyo tambua ulimwengu na  ili  kuweza kubadilisha njia ya mahusiano yaliyopo na ulimwengu huo.Wanapendekeza lengo la kuwa na ujasiri katika kukubali maisha yetu kwa urahisi zaidi na ushirikiano.

Wito wa haraka kwa wale wote wanaojikita katika shughuli za kijamii , kiuchumi , kisiasa , na  utamaduni , kuwajibika katika kusikiliza kwa uangalifu kilio cha dhunia na kusubiri mahitaji ya wale ambao wamewekwa pembezoni na zaidi kusikiliza maombi ya wengi wanaoomba kuungwa mkono makubaliano ya kimataifa ili kurudisha hali inayostahili ya viumbe vilivyojeruhiwa.Ujumbe pia unasema kuwa wao binafsi  wanaamini kwamba haiwezekani kuwapo suluhisho la kweli na la kudumu mbele ya changamoto ya mgogoro wa mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa  bila kuwa na jibu halisi kwa pamoja, bila kuwajibika kwa pamoja na kuwa na uwezo wa kuelewa yaliyo fanywa; na mwisho  bila kutoa kipaumbele katika mshikamano na katika huduma.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.