2017-08-31 17:39:00

Papa Francisko awaombea walio pata maafa ya nguvu ya asili Marekani


Baba Mtakatifu Francisko ametuma barua yake kuonesha ukaribu wa kiroho kwa watu wote walio pata maafa kutokana na nguvu za asili  huko Texas na Louisiana. Ujumbe wake uliotiwa sahini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican kwa kupitia Askofu Mkuu wa Jimbo la Galveston- Houston ambaye ni Rais wa Baraza la Maaskofu wa Marekani, Baba Mtakatifu anasema anao uchungu kutokana na janga hilo ambalo limepoteza maisha ya watu na maafa mengi ya mali zao kutokana na nguvu za kutisha za asili.

Anawakikishia maombi yake kwa Mungu waathirika na familia zao na wote ambao wamejikita kwa sasa katika shughuli za uokoaji wa maisha ya watu. Anaamini kwamba wimbi kubwa la mshikamano katika mahitaji makubwa ya haraka na msaada kwa  watu walio athirika utaendelea kuhamasika kutokana na ubora wa utamaduni wa Taifa la Marekani .

Pamoja na hayo taarifa zinasema idadi kubwa ya waathirika inazidi kuongezeka katika mkondo huo wa Harvey, ambao ni kimbunga kikubwa kilichotokea tarehe 25 Agosti na kukumba mji wa Texas kwa mvua kubwa na mafuriko pamoja na upepo mkubwa.
Kwa mujibu wa Shirika la habari la CNN linasema hadi sasa ni vifo vya watu 37 wakati huo uo maafa ni mengi sana yenye kufikia mamilioni ya dola za kimarekani 160. Aidha baada ya Harvey  ambao ni upepo wa nguvu wa kitropiki kubadilisha mkondo wake,kuna kupungua nguvu zake kwa mujibu wa wataalam wa hali ya hewa huko Marekani.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.