2017-08-31 17:50:00

Barua ya Papa Francisko katika mwaka 10 wa Mwenye Heri Zeffrino nchini Argentina


Baba Mtakatifu Francisko ameandika barua kwa Askofu wa Jimbo la Viedna Argentina Esteban Maria Laxaque kwa ajili ya tukio la kuadhimisha miaka 10 tangu kutangazwa kwa Mwenye heri Zeffrino Namuncura, mtoto mzalendo wa Mapuche nchini humo  aliyekumbatia imani katika Yesu na familia ya Shirika la Wasalesian, alikufa  mwaka 1905 mjini Roma akiwa na miaka 19 tu kutokana na ugonjwa Kifua kikuu. Baba Mtakatifu Francisko anandika , Padri daima atambuliwe na watu kwa jinsi  anavyojitoa  maisha yake kwa ndugu.

Kwa namna ya pekee anakumbuka furaha aliyo ionja  miaka 10 iliyopita katika tukio la kutangazwa mwenye heri  Zeffrino, ambaye ni mfano bora wa kuigwa na kupendwa na watu nchini Argentina, anasisitiza kwamba hatasahau watu wake na utamaduni wake. Kuhusiana na suala la huduma, Baba Mtakatifu anasema, Padri lazima ahudumie watu  na vijana wanatambua kujibu kwa ukarimu  hasa pale ambapo Yesu anajionesha katika maisha yao wao hufanya  ushuhuda wa maisha halisi , kama alivyofanya Zeffrino. Anamalizia barua yake akisema. Na utashi wake ni kuona vijana wanakutana na upendo wa Yesu katika maisha yao na kuwatia moyo ili waweze pia kuwasaidia wengine.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.