2017-08-30 15:00:00

Swaziland: Inahitajika umoja kupambana na biashara ya binadamu hasa watoto


Mapambano dhidi  ya wafanya biashara wa binadamu unachangiwa hata familia,hiyo ni kwasababu ya  umaskini na hofu ya kukosa usalama. Huo ni ujumbe uliotolewa na Askofu Manzini Jose Luis Gerardo Ponce de León, wakati wa kutoa  hotuba yake  katika tukio la maandano ya kupinga biashara ya binadamu hivi karibuni wakati wa  maadhimisho ya Siku ya kupambana na biashara ya binadamu mwaka 2017, ambapo Kanisa Katoliki limekuwa mstari wa mbele kushiriki kikamilifu maandamano hayo pamoja na viongozi wa kisiasa, wanajeshi na wawakilishi wa kidiplomasia nchini Swaziland.

Gazeti la Osservatore Romano limenukuu kuwa, wamahamasishaji wa maandamano hayo wanasisitiza kwa namna ya pekee juu ya kuzuia matukio haya ambayo sasa yanazidi kuongezeka katika nchi ya Swaziland. Askofu Ponce de Leone amethibitisha kuwa, matendo haya yamezidi kuongezeka na waathirika zaidi ni watoto wadogo, ambapo umaskini, ukosefu bora wa matunzo, na kuenea kwa ujinga zaidi katika hali za  utamaduni ndiyo sababu kubwa za kuchangia  zaidi kuongezeka kwa matukio hayo. Anasema, ni lazima kuzungumzia juu matukio haya, kwa ajili ya kuwasaidia watoto na vijana wawe na utambuzi zaidi wa matukio haya halisi  ya kutisha kwa kiasi kisichoelezeka.

Ulinzi wa wadogo unapitia kwa njia ya familia;  kwa njia hiyo sera za kisiasa na mipango inapaswa kuwasaidia wanafamilia wapate nyenzo muhimu kwa ajili ya kulinda na kuwatunza watoto wao wanaojikuta katika hali ya kuathirika wenyewe. Hiyo ni pamoja na kwamba wanakaa katika nyumba ambazo hazifahi, aidha ukosefu wa bima ya afya na elimu ambvyo ni vitu msingi. Kwa namna hiyo Askofu anasema wote wanapaswa kurudia kwa upya uwajibikaji na pia kwa njia ya caritas ya Swaziland, hasa majengo yao ya shule yaweze kutumika kwasaidia watoto. Yeye binafsi anasema kuwa, anaamini kwamba hakuna yoyote yule anayeweza kukabiliana na tatizo peke yake. Kwa njia hiyo ili kupambana na uhalifu dhidi ya biashara ya maisha ya Binadamu,inahitaji nguvu ya binadamu wote , kwa pamoja ili kuweza kukabiliana na changamoto hiyo ya kutisha.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.