Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa \ Kanisa Ulimwenguni

Patriaki Bartholomew asema ni kipindi cha kutafakari nguvu ya kutisha ya asili

Uharibifu mkubwa unaoendelea katika Ghuba ya Texas hasa huko Houston umesasababishwa na kimbunga cha Harvey ambayo ni dhoruba ya kitropiki - AP

30/08/2017 14:45

Uharibifu mkubwa unaoendelea  katika Ghuba ya Texas hasa huko Houston ambao ni mji wa nne kwa ukubwa nchini Marekani umesasababishwa na kimbunga cha Harvey ambayo ni dhoruba ya kitropiki. Huo  ni wito mkubwa wa kukumbusha nguvu kali za asili isiyoelezeka. Ni mwanzo wa maelezo ya waraka wake Patriaki wa Kiekumenu Bartholomew I anajulikanaye duniani kwa harakati za shughuli za utetezi wa Mazingira hadi kubatizwa kama Patriaki Kijani. Barua hiyo ikiwa inawalenga waathirika wa maafa yaliyotekea huko Marekani kwa kimbunga cha Harve; Patriaki anawawahikishia maombi yake kwa Mungu kwa wote waliopoteza maisha yao, kwa ajili ya familia zilizo athirika na msiba huo, halikadhalika wahusika wote wa vikundi vya kutoa msaada wakati huu. Mungu awape nguvu  katika dakika hizi za mahitaji. Pamoja na ujumbe huo wa Patriaki anawaalika kutafakari juu ya wajibu  walio nao binadamu wote kwa ajili ya kututea na kulinda mazingira, ikiwa ni katika maandalizi ya kuadhimisha Siku ya kuombea utunzaji bora wa mazingira mwaka 2017 tarehe Mosi Septemba.

Ni wakati wa kutafakari juu ya nguvu ya kutisha ya asili, unasema ujumbe; na wajibu wetu wa kibinadamu kuwa watendaji bora na wenye busara wa mazingira. Sisi sote tumeitwa kushiriki katika ukombozi na usimamizi wa dunia yetu, kufanya kazi ili kuzuia nguvu ya uharibifu utokanao na vimbunga, vilevile kuwa na mipangilio bora wa  mazingira; Ni lazima kushiriki kikamilifu katika kukabiliana na shida kubwa ya mabadiliko ya tabia nchi na jinsi inavyoathiri dunia yetu. Ni lazima kila mtu binafsi kushuka na kujikita katika uwanja mpana na katika mipango ya upendo ambayo yaweza kusaidia na kuunga mkono wale ambao maisha yao yamebadilika kwa kiasi kikubwa kutokana na mabadiliko ya mazingira mbele ya macho yetu. Ujumbe wa Patriaki Bartholomew I unahitimishwa kwa kukumbuka agano kati ya Mungu na kila kiumbe duniani kutoka kitabu cha Mwanzo kwamba hakutatokea  gharika kuu kuharibu mwili wa Binadamu.  

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

30/08/2017 14:45