Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Habari \ Habari za Kimataifa

Umoja wa nchi za Ulaya kushirikiana na Afrika kupambana na uhamiaji

Viongozi kutoka Ujermani, Ufaransa,Italia, Uhispania,Chad,Niger na Libia wamekutana mjini Paris 28Agosti 2017 - AFP

29/08/2017 10:59

Ni mipango kabambe ya kujikita katika matendo kwa haraka iwezekanavyo  ili kupambana na wafanya biashara haramu ya maisha ya binadamu, vitendo vya uhalifu, madawa ya kulevya, silaha, makundi ya kigaidi, ambao wamesababisha bahari ya Meditrranea na Afrika kuwa makaburi ya watu. Hayo ni maelezo yanayotokanayo na Mkutano uliofanyika mchana tarehe 28 Agosti 2017 mjin Paris Ufaransa, kati ya viongozi wa Ufaransa, Ujermani, Italia, Uhispania, Libia, Chad, Niger na viongozi wengine wawakilishi wa Umoja wa Ulaya katika sera za siasa za nje.

Washiriki wote waliweza kuonge na vyombo vya habari katika kutoa maoni yao kuhusu Mkutano huo. Akingea na vyombo vya habari  Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitoa kwa ufupi kuhusu  mambo matatu msingi aliyoeleza ya kutekeleza il kuweza kupambana na mitandao ya wafanya biashara haramu na kusisitizia juu ya mipango ambayo tayari imekwisha anza katika baadhi ya nchi za Afrika kwa maana ya kuimarisha usalama na kusaidia uchumi mahalia, pia suala utelezaji la hali ya kisiasa nchini Libia na kusaidia kazi ambayo Umoja wa Mataifa na Shirika la kusaidia wakimbizi katika mantiki thabiti. Vilevile ameelezea juu umuhimu wa uwepo wa mshikamano wa kibinadamu ambao ndiyo msingi na mantiki inayo ongoza shughuli hiyo. Amesisitiza pia rais wa Ufaransa juu ya ulazima wa kujikita zaidi katika siasa ya Umoja wa Ulaya kwa kipindi cha muda mrefu kwa ajili ya maendeleo endelevu ya nchi za Afrika.

Suala muhimu ni maamuzi ya kuwa na nguvu za pamoja katika uwanja huo mpana kwa kutoa kipaumbele kwenye upembuzi  na kung’amua  mahitaji nyeti kwa upande wa mataifa matatu ya Afrika na kuhakikisha uamuzi huo kwa sasa unafanyika. Hata hivyo taarifa zinasema kuwa viongozi saba watakuwa na mkutano tena siku chache zijazo kabla ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa nchi za Ulaya na Umoja wa nchi za Afrika unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu huko Abidjan nchini Ivory Coast. Naye Chansela wa Ujerumani Angela Merkel mara baada ya mkutano huo amesema umekuwa mkutano mpya na wa kufaa kwasababu wamefanya kazi kwa mtazamo sahihi wa hali halisi ya sasa.

Hata hivyo kila nchi ya  Ulaya  kama vile Umoja wa Ulaya, kiuchumi wao tayari na wamejiuhusisha na mipango kuhusu nchi mbili ya  Niger na Chad, ili kuweza kuendeleza maendeleo, mojawapo ya mpango madhubuti ni ule wa kutaka kusitisha wimbi la watu wanao acha Afrika wajiingiza na  kuamini mitandao ya wafanya biashara haramu, ambao kwa hakika ndiyo wanao kuza ugaidi. Ni kwa mujibu wa maneno ya rais wa Chad Idriss Deby. Aidha anasema, kipeo hiki cha ugaidi kinaweka mbele yao kuwajibika na kukabiliana na matatizo ya umaskini  katika nchi za Afrika.
Sambamba na maneno ya Rais wa Chad hata rais wa Niger Mahamadou Issoufou anasema, kupambana na uhamiaji usio halali, na kusitisha wimbi hilo ni jambo la kimaadili ili kuweza kuokoa vifo vingi vya watu vinavyotokea, pia ni pamoja na  kuweka kanda za nchi  katika hali ya usalama. Kwa njia hiyo anasema nchi ya Niger imezindua mpango ya kupambana na uhamiaji usio halali kwa kuongeza nguvu katika ngazi za ulinzi na usalama nchini mwao, lakini pia kusaidia maendeleo ili watu waweza kupata njia mbadala ya kuondokana na uhalifu katika kutatua matatizo yao ya  umaskini.

Washiriki wa Mkutano huo wamekubaliana wote kwamba changamoto hiyo ni ya pamoja, kwanjia hiyo lazima kishirikishana. Naye Waziri Mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy amewashukuru wote kwa mshikamano wao mara baada janga kubwa la shambulizi la kigaidi lililotokea Barcellona; kwa upande wake anasema, ugaidi na wahamiaji  kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni ndiyo wasiwasi mkubwa wa wazalendo wa Ulaya. Hayo ameyasema wakati akiwakilisha matarajio ya mipango katika vipengele vitano vya kuweza kukabiliana na kupambana na changamoto kubwa la ugaidi.
hata hivyo  Mataifa ya ulaya yako tayari kutoa misaada ya maendeleo kwa washiriki wake Barani Afrika ili kusaidia kupunguza wimbi la wakimbizi barani ulaya wanaokimbilia barani humo kwa sababu za kiuchumi pamoja na kutafuta hifadhi.

Hata hivyo taarifa mapema mwezi huu zinasema kuwa idadi ya wakimbizi na wahamiaji waliowasili Ulaya katika nusu ya kwanza ya mwaka huu kupitia moja ya njia tatu zinazotumika,  imepungua ikilinganishwa na kipindi kama hiki mwaka jana.Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR iliyotolewa mapema wiki tarehe 24 Agosti 2017 ikiangazia njia tatu za kuvuka kuingia barani humo kupitia bahari ya Mediteranea. Sababu kuu ni kupungua kwa asilimia 94 ya idadi ya watu wanaotumia njia ya bahari kutoka Uturuki kwenda Ugiriki. Hata hivyo ripoti inasema kwa wale wanaosafiri kutoka Afrika ya Kaskazini bado idadi imesalia kama mwaka jana ambapo wakiwa safarini au wakifika Ulaya bado wanakumbwa na ukatili mikononi mwa wasafirishaji haramu au hata polisi, wengine wakikabiliana na mbwa wa polisi.

Kamishna Mkuu wa UNHCR Filipo Grandi amesema kuchukua hatua kudhibiti idadi ya wakimbizi na wahamiaji wanaoingia Ulaya bila kuimarisha amani na maendeleo na njia salama za kusafiri haikubaliki kimaadili. Bwana Grandi ametaka jamii ya kimataifa iazimie upya kuchukua hatua kuimarisha ulinzi na usalama wa wakimbizi na wahamiaji na kuweka mpango rahisi kwa wakimbizi kupata makazi na kuungana na familia zao.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

29/08/2017 10:59