Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Amani

Jamh. Afrika ya Kati walalamikia Kikosi cha kulinda amani cha UM

Jamh. ya Afrika ya Kati ya walalamikia Kikosi cha kulinda Amani kutokujali maisha ya watu. - ANSA

29/08/2017 11:25

Yapo mashtaka kuhusu kikosi cha wanajeshi wa kulinda usalama cha Umoja wa Mataifa katika nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, kwamba hawalindi raia kutokana na mashambulizi ya wanamgambo wenye silaha katika vijiji vya kusini mashariki.Wamekuwapo kwa ajili ya kulinda amani lakini badala yake wameacha mji na kuondoka. Huu ni ujumbe wa Padre Jean-Alain Zembi , paroko wa Kanisa la Mtakatifu  Yohane mbatizaji huko Zemo, Parokia iliyoko mpakani na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, akielezea jinsi gani Kikosi cha kulinda usalama cha Umoja wa Mataifa hawajali watu na kwamba wanahusika na watu waokufa pia wale wanaojiandaa kufa kutokana na ukosefu wa ulinzi.

Ujumbe ulio tolewa mapema mwezi huu,Padre amesema karibia wazalendo 30 wameuwawa na vikundi vya wanamgambo  wenye silaha waliposhsmbulia kituo cha polisi na hopitali na nyumba nyingi kuchomwa moto na kuiba vitu vyenye thamani. Wanajeshi wa Kikosi cha Umoja wa Mataifa kutoka nchi ya Morocco mwanzo wali weza kuwalinda raia mahalia, lakini hawakuweza kuwalinda na kuwatete watoto na wanawake wasio kuwa na hatia anathibitisha.
Hata hivyo wanajeshi wa kikosi cha Ulinzi wa Umoja wa Mtaifa kutoka nchi ya Morocco wamefunguliwa mashtaka na siyo tu kukosa kulinda raia, bali hata kuwaua rai wasio kuwa na hatia. Vilevile Imam Oumar Kobine Layama, kiongozi wa Umoja wa madhehebu ya Kidini nchi ya  Jumhuri ya Afrika ya Kati hivi  karibuni alikuwa ameomba waondoke katika eneo hilo mwaka huu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya radio Vatican
 
 

 

29/08/2017 11:25