Kuanzia tarehe 11 hadi 21 Agosti wanaume na wanawake 72 wa Chama cha Kitume cha Wakatekumeni wapya nchini Afrika ya Kusini, katika kujibu wito wa Baba Mtakatifu Francisko wametumwa katika utume wawili wawili , wakiwa na Biblia mikononi kwa ajili ya kutangaza Habari njema nchini Afrika ya Kusini, Swaziland, Botswana na Lesotho. Aliye wabariki katika kuanza utume huo ni Askofu Mkuu wa Jimbo la Cape Askofu Brislin ambaye ni Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kusini mwa Afrika(SACBC), na wakati wa maadhimisho ya misa alirudia maneno haya “ kwa njia ya ubatizo tunashiriki kama mitume kwenye huduma ya Yesu Kristo katika kutangaza Ufalme wa mbingu.Uinjilishaji katika nyakati za kisasa , siyo tu kupeleka Yesu kwa wale ambao hawajawahi kusikia juu ya Yesu, bali hata kwa wale ambao kwa nyakati za sasa Yesu siyo muhimu kwao il kuweza kuwasha imani yao kwa upya.
Utume huo upo kwa sasa katika mchakato wa dunia nzima, kama vile Baba Mtakatifu
Francisko alivyowatangazia Vijana zaidi ya 150,000 Chama cha Kitume cha Wakatekumeni
wapya walio kuwa wameudhuria Siku ya Vijana Duniani huko Poland wakiwa katika mkutano
wao kuhusu wito.
Utume huu siyo kwa watu tu walio wekwa wakfu, hayo ni maneno ya Msimamizi wa wa
chama cha Kitume cha Wakatekumeni wapya Kusini mwa Afrika, Padri Dino Furgione, kwa
maana ya kwamba utume huo umefanywa na wana ndoa, wasio kuwa na ndoa, vijana, wazee,
mapadre na waseminari. Hiyo ndiyo moyo wa Baraza Kuu la Mtaguso Mkuu wa II wa Vatican,
ni mwili wa Kanisa na kama uwepo halisi wa Kristo.
Aidha anaongeza kusema, wamefanya uzoefu ya kwamba Kristo mwenyewe anawasindikiza. Kwa kujibu swali ambalo anaweza kuuliza kama isemavyo Injili ya Luca; Je nilipokutuma kwenda nje bila mfuko wala viatu, je ulikosa kitu chochote? Tunaweza kutoa ushuhuda kwamba hatujakosa kitu chochote kile pamoja na kwamba wengine ndiyo wameteseka kwa ajili ukosefu wa mambo fulani lakini pia wamefanya uzoefu wa furaha kamili kama ile ya Mtakatifu Francisko wa Asizi,kwani hata yeye alitumia njia hiyo ya kuwatuma ndugu wadogo wawili wawili.
Sr Angela rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |