2017-08-26 15:33:00

Ziara ya Papa nchini Colombia ni ishara ya mapatano kwa wote


Bado siku chache kabla ya ziara ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Colombia. Ratiba ya ziara hiyo inaonesha kwamba hija hii ya kitume itakuwa kuanzia tarehe 6 hadi  11 Septemba 2017. Ni safari yenye lengo la kutaka kuhamasisha mapatano  kama inavyojieleza katika kauli mbiu  iliyochaguliwa ya ziara “Hebu tufanye hatua ya kwanza”. Ni safari ya kutaka kuanza kwa  upya kutafuta  amani ya nchi ambayokwa miaka mingi  imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Ili kuweza kupata ushuhuda jinsi gani waamini wa Colombia wanajiandaa kumpokea Baba Mtakatifu Francisko, Mwandishi wa habari wa Radio Vatican  amefanya mahojiano na Monsinyo Fabio Suescún Mutis Mkurugenzi mtendaji wa maandalizi ya safari ya kitume ya Papa nchini Colombia.

Yeye anasema, kufika kwake Baba Mtakatifu Francisko, ni furaha kubwa kwasababu ziara yake inaweza kuwa fursa ya  kuleta matumaini ya wakati ujao katika mioyo ya watu wa  taifa la Colombia. Katika kauli mbiu ya mapokezi ya Baba Mtakatifu kuhusu kufanya  hatua ya kwanza ule  ni utashi  wa watu sasa kutaka kufanya uamuzi wa kuchukua katika maisha . Aidha kauli mbiu hiyo inamlenga yule  anaye fanya hatua ya kwanza  katika kufanya maamuzi na kuacha  hali ambayo haistahili ili ajikite kwa upya katika hatua za  safari kuelekea wakati ujao wa imani na matumaini.

Hiyo ni kwasababu nchi ya Colombia inahitaji kufanya hatua ya kwanza  kwa upya na kuacha hali ya migogoro ya ukosefu wa haki ambapo kwa sasa watu wote wako tayarikufanya  upatanisho  na kujenga nchi mpya na Kristo mwokozi. Monsinyo Monsinyo Fabio Suescún Mutis kadhalika anaeleza kuwa ni umuhimu kufanya  safari hiyo ya amani na mapatano kwa bara zima la Amerika ya kusini ambayo inateseka na migogoro mingi katika maeneo mengi, kwa kufikiria mfano wa kiel kinachotendeka nchi ya Venezuela. Ziara ya Baba Mtakatifu ni kipindi cha neema ambacho Mungu anapenda kuwazawadia watu wa amerika ya Kusini ili waweze kufanya uzoefu wa kuishi imani waliyoipokea hapo hawali, ambayo ni kama tunu lakini, ambayo wanalazimika a kuifanya iweze kuwa halisi kwa kutafuta haki na katika mapatano , wakati huo huo wakijibidisha katika kutafuta wema wa pamoja.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.