2017-08-23 16:17:00

Ni zaidi ya watu 400 elfu waathirika wa mafuriko huko Sierra Leone


Hali ya waathirika wa mafuriko yasiyoelezeka nchini Sierra Leo inazidi kuwa mbaya kuzunguka mji mkuu wa Freetown. Kwa mujibu wa Caritas ya  Italia inasemekana kuwa ni waathirika 400 elfu kati yao 100 elfu ni watoto na zaidi ya watu 600 wamepotea na maelfu ya watu walio songamana kutokana na ukosefu wa mahali pa kulala. Mamlaka ya ndani ya nchi wanayo wanatoa  takwimu zao  kuwa ili  ni zaidi ya janga kubwa la asili lilowahi kutokea katika historia ya  nchi hiyo ambayo tayari ni maskini katika ulimwengu, ambapo watu wanaishi katika mazingira magumu.

Taarifa zinasema kuwa katika Hospitali ya Connaught mjini Freetow, hakuna hata nafasi ya kulaza mihili ya marehemu. Hiyo ni nchi iliyokumbwa na ugonjwa wa Ebola na sasa mafuriko hayo tena , lakini matumaini ya kwamba wataweza ushinda japokuwa inahitajika nguvu ya pamoja kwa ajili ya kuokoa watu sasa ambao wanazidi kuteseka. Kwa mujibu wa Caritas ya Italia wanasema watu wa Sierra leone wanahitaji msaada mkubwa na haraka kutokana hofu ya magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu kutokana na msongamano uliopo na ukosefu wa sehemu za kujisitiri pia mvua ambazo inasemekana bado ziatendelea kunyesha kwa wiki kadhaa.

Hata hivyo Caritas ya Sierra leone, imejikita  zaidi katika maeneo hayo yaliyo kumbwa na mafuriko ili kusaidia familia nyingi wasio kuwa na makazi. Pamoja na hayo pia  mashirika mengine yasiyo ya kiserikali yakisidiana  na serikali ya ndani wamekuwa mstari wa mbele kufanya kila liwezekanalo japokuwa hali bado ni mbaya sana. Pamoja hayo,wanaungana hata na sala ya Baba Mtakatifu Francisko kwa ajili ya waathirka hao na  Caritas ya Sierra leone inaendelea kuwa na mawasiliano na Caritas ya kimataifa kwa ajili ya kusaidia janga hili.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.